Freeman Mbowe kung'atuka uongozi wa CHADEMA mwaka 2023

Freeman Mbowe kung'atuka uongozi wa CHADEMA mwaka 2023

Mimi kwangu nimeridhika kabisa na maamuzi haya ya Mbowe, na cdm wanapaswa kurekebisha kipengele cha mtu kutokukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Hiki kimekuwa kilio changu cha muda mrefu sana. Mimi sio muumini wa kiongozi kukaa kwenye nafasi moja ya kuchaguliwa zaidi ya miaka 10. Namshauri Mbowe wala asikubali kushauriwa na yoyote kuendelea kukalia kiti hicho zaidi ya muda aliosema.
Swala ni mtu wa kuaminika kumkabidhi kiti kama bado hajapatikana basi Mbowe aendelee kama yupo anayetosha basi wanachama wamuone na waridhike naye nje ya mipaka ya mashaka.
Mbowe amekuwa kiongozi bora sana wa upinzani hapa Tanzania.
 
All the best kwake, mchango wake I can't explain hapa; nia yake, dhamira, utashi, hekima, uvumilivu (kakoswa na mabomu Soweto Arusha, risasi Mkwajuni Dsm). damn the list is endless. I am really proud of this guy.

Chadema ilipata Mwenyekiti the best ever, wamepiga kelele mwizi, sijui nini... but hakuna yeyote kati yao aliyethubutu kwenda mahakamani, Mbowe aliwaburuza wakaburuzika, walitaka kumuondoa kwa namna zote wakashindwa, leo ameamua kuondoka mwenyewe.

#Mwambahalisi.
Hana mfano,,the best ever!
 
Hakuna kipindi Mbowe anahitajika kwenye siasa za upinzani kama hiki.
Baada ya Mwendazake kulikoroga na kutangulizwa mapumzikoni,Mama ana match na Mbowe.Siasa zinaendeshwa kwa ustaarabu wa hali ya juu.
Hii ndio Tanzania tuitakayo
Ni kawaida yenu kusema mbowe anahitajika chadema zaidi. Chadema imeweka wagombea tofauti tofauti lakini mwenyekiti hajabadikishwa. Hivi ni kipi kikubwa Kati ya Tanzania na Chadema.
 
Ni kawaida yenu kusema mbowe anahitajika chadema zaidi. Chadema imeweka wagombea tofauti tofauti lakini mwenyekiti hajabadikishwa. Hivi ni kipi kikubwa Kati ya Tanzania na Chadema.
CCM Chadema haiwahusu, yaangalieni mambo yenu wenyewe huko Lumumba!
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza kuachia uongozi wa chama mwaka 2023

Pia, amewataka viongozi wa chama hicho Kanda ya Magharibi kutodumazwa na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi uliopita bali wajipange upya kudai na kusimamia haki
Biya anaachia madaraka siamini, muda ukikaribia utasikia wanachama wa SACCOSS wameniomba niendelee, hakawii kugeuza gia angani.
 
Hahahaha...kama nilivyosema awali...Mbowe ni master na kacheza kama Pele na wala sikubishii mkuu
Kama Mbowe alikuwa vizuri kuliko wote chadema kwanini hakuwa mgombea wa kudumu kwa uraisi kupitia Chadema. Au uraisi ni mdogo kuliko uenyekiti wa Chama?
 
Bila Mbowe miaka mitano ya Magufuli, CHADEMA ingekuwa ni historia wakati huu

Bila Mbowe wakati wa Zitto chama kingevurugika sana hata kisitambulike kinaelekea wapi.

Ukiona watu kama akina Slaa wanapoteza mwelekeo, lakini Mbowe bado kasimama, ujuwe hapo kuna mtu asiyeyumbishwa kirahisi.

Mashinji; kama CHADEMA ingekuwa na siri ambazo Magufuli angezipata kutoka kwake na ukawa ushahidi wa kukiua chama, CHADEMA ingeishia hapo. Lakini hapakuwa na siri, hata ya kutunga tu ambayo ingemwezesha kukifuta.

Lakini, katika yote ninayoweza kumsifia nayo Mbowe, ni jinsi alivyoepusha damu za waTanzania kutiririka, alipohifadhi "operation" UKUTA.

Huo ulikuwa ni mwanzo dhahiri wa Magufuli kumwaga damu, tena angeimwaga huku akichekelea. Huenda Mbowe mwenyewe wakati huu angekuwa ni historia tu ya watu kusimuliwa kwamba ndiye alikuwa mwenyekiti wa chama, ambacho nacho kingekufa pamoja naye hapo hapo na kumwacha Magufuli akitamba.
Onesha mafanikio ya mbowe baada ya Slaa kuondoka Chadema?
 
Jibu swali kati ya mwenyekiti wa Chama na raisi wa nchi ni nafasi gani inahitaji mtu makini zaidi?
Kila kimoja kikae kwenye nafasi yake kwa umuhimu wake.

M'kiti wa Chama ana nafasi kubwa ya kukiandaa Chama kushika uongozi wa nafasi mbalimbali ikiwemo ya Urais.

Rais anasimamia ilani ya chama kinachoongozwa na M'kiti.

CCM mna RAIS M'kiti, hamuwezi kuelwwa haya.mambo!
Najua mtasema Rais ndio inahitaji mtu makini kuliko M'kiti wa Chama.
 
Hoja zako ni dhaifu sana huwezi kufananisha kiongozi wa taifa na kiongozi wa chama. Haiwezekani kiongozi mzuri aachiwe Chama halafu kiongozi dhaifu apewe nafasi ya kugombea uraisi wa nchi.
 
Bora kabisa ili hicho chama kishikwe na wasukuma sasa.

Wachaga wamekidumaza hicho chama.
Inawezekana mbona? Si wasukuma wote wabaya.
Wabaya ni wachache sana kulinganisha na wengi
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza kuachia uongozi wa chama mwaka 2023

Pia, amewataka viongozi wa chama hicho Kanda ya Magharibi kutodumazwa na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi uliopita bali wajipange upya kudai na kusimamia haki
Mbowe yupi huyo?
 
Onesha mafanikio ya mbowe baada ya Slaa kuondoka Chadema?
Bado huelewi unachosoma?

Mafanikio; si hayo hapo CHADEMA inadunda hadi sasa? Huyo Slaa ilikuwa ni mpango wa kuiua CHADEMA, lakini ikashindikana, bado wewe huoni kuwa hayo ni mafanikio makubwa?
 
Bado huelewi unachosoma?

Mafanikio; si hayo hapo CHADEMA inadunda hadi sasa? Huyo Slaa ilikuwa ni mpango wa kuiua CHADEMA, lakini ikashindikana, bado wewe huoni kuwa hayo ni mafanikio makubwa?
😂 😂 😂 saaahv slaa alikua anaiua chadema
 
Kwahiyo Lissu hafit hiyo nafasi maana sioni kupigiwa debe?
 
Wajipange sasa kupata mwenye weledi kama wake la sivyo by 2025 chama kitakuwa tayari kishapotea
 
Back
Top Bottom