Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Wakuu
Hizi ni juhudi za mama
Kuiokoa SERIKALI yake
Namna pekee ni kuwabembeleza CHADEMA washiriki uchaguzi 2025!
Ngoja Tuone!!
Wakati wa uchaguzi CCM hawanaga urafiki, wanaingia kwa four wheels
 
Rais SSH ni mpango wa Mungu. Hakika baada ya yule Shetani wa Chato ambaye alikuwa anatugawa kiitikadi na kikabila, akiua na kutudanganya, tumepata kiongozi mwenye upendo, mcha Mungu na anayeipenda nchi yetu kwa dhati. Tanzania Iko salama sana mikononi mwa Samia.

Sanasana Magufuli angewapiga risasi au kuwateka
 
Wakuu
Hizi ni juhudi za mama
Kuiokoa SERIKALI yake
Namna pekee ni kuwabembeleza CHADEMA washiriki uchaguzi 2025!
Ngoja Tuone!!
CCM ya kina makonda na Musica inaona huu ni kama uchafu..CCM gani inakaa na wapinzani...fagia woote dadadeq.

Mama ana mapambamo makubwa sana ndani ya chama chake.

Njia pekee ni kuwa na waoinzani....I also see the only way.

CCM ina makundi mabaya na maovu.
 
Binafsi wanasiasa sijawahi kuwaamini, labda kugawana kakeki ka taifa tu...... sababu ya mtu yeyote kuanzisha Chama Cha Siasa ni kushika dola, siamini kama Kuna mtu anaweza kutamani kuachia dola......japo kukutana hivi Kuna mrahisishia aliye madarakani kuongozo
 
Wanasiasa wote lao moja, labda kama hujui tu.....
 
Hii mbinu waliitumia kwa Maalim Seif (Mwafaka) kule Zanzibar. Maalim aliposhinda uchaguzi wakafuta matokeo. Ni hivyo hivyo itakuwa kwa CHADEMA. Wanawapumbaza ili waongoze kwa amani hadi 2025 watakapoiba uchaguzi tena. Mbowe asiwe mjinga.
Mbowe awe makini, CCM sio wa kuamini kuwa wanaweza kuweka mazingira yatayoruhusu wao kuachia dola kwa amani.
 
denooJ kwani unataka mwisho wa siku afanyeje? Aache kukutana na Rais?

Maridhiano ni mchakato (process). Unaweza usiyaone matunda ya kazi hii njema mara moja na papo kwa papo...

Let's be patient..

Surely, I personally see bright future ahead..

It's very difficult. But, surely there's hope..
 
Hivi Chadema wote mna ukosefu wa afya ya akili? Reconciliation on what? Kuna nn kilitokea hadi mtake reconciliation? Hivi mna mdekea nani? Mmeshindwa uchaguzi, kila mahali CCM inawapiga vibaya, mnataka reconciliation kwa lipi? Alafu acheni ujinga, nendeni mkafanye kwanza hiyo reconciliation kwenye Chama chenu ambapo Mwenyekiti dictator hatoki ni yeye tu, yaani mkajadiliane wenyewe huko, mtatue matatizo yenu huko.
 
Mara ooh hatumtambui Rais na serikali yake iliyotokana na uchafuzi mkuu, shenzi taipuuu..!!
 
Wana CCM radical hawatapenda kabisa hii kitu mama Samia anafanya.

Kwangu mimi na kwa faida ya watoto wangu wadogo nasema hibi Mama Samia upo sahihi..Sauti za wengi ndiyo huwa ni sauti ya Mungu.

Mama usije kuhukumiwa ukiwa hai, mwenyezi Mungu anaweza kufanya lolote kuzinusuru sauti za wengi.

Upo sahihi, tena sahihi sana sana...waandikq legacy tunawamudu mbona.
 
Naona sasa hivi Mbowe karudisha vizuri mirija yake ya kula akipuliza iliyozibwa zama zile sasa ameizibua na usitegemee changes ni danadana
 
Chadema mkae macho sana na hawa watu, wanazitaka sana hizi picha za pamoja kwaajili ya kuwarubuni wafadhili, wakati hali halisi uwandani haiko hivyo na matendo yao yamejaa uhuni huni tu. Kama wananchi tunataka baada ya vikao vyenu mnatoka na statement ya pamoja kwa wwatanzania na siyo hizo picha zenu. Pia statement inayotolewa ifanane na matendo yatakayofuata baada ya kikao. Kama vipi achaneni nao hao Ccm nanyi mrudi kwa wananchi kwani walishawaelewa longtime.
Na kama hamjagundua joto la siasa lipo juu sana sasa hivi tena bila hata mikutano ya hadhara, hivyo wanatumia mbinu ya kuwaita na kupiga picha ili kusafiria nyota ya Chadema na kushusha temper ya wananchi. Lakini wanasahau baada tu ya siku mbili tatu unakuta wameshachafua hali ya hewa tena. Wameshazoea vya kunyonga hao.
 
Mama yuko kazini

MUNGU ametubariki kuwa na Rais mzalendo

2025 njia nyeupe..👋
 
Angekuwa Zitto na ACT yake angeitwa msaliti

Hii nchi ngumu sana aiseeee

Tujifunze kuupa muda nafasi ili tujiridhishe.
 
Wanafuata nini ikulu kila mara kama sio kupotezeana muda?
Wanalambishwa asali, hao wote ni wafanyabiashara wa siasa.
JokaKuu
Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.
Wanaridhiana kitu gani?...matokeo ya uchaguzi wa 2020 au Lile zuio la kufanya mikutano ya hadhara ? zitto junior
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…