Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Wakuu,

Muda huu M/Kiti wa CHADEMA na viongozi waandamizi 9 wa chama hicho wapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Tutarajie jambo gani jipya? Ndo ukurasa mpya wa Siasa za Tanzania?

UPDATE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.

View attachment 2232248View attachment 2232250
View attachment 2232257View attachment 2232258View attachment 2232259

View attachment 2232260
Mbowe anafanya kila njia ili kuizuia ile kesi ya kina Mdee maana inaenda kukiumbua Chadema.

Ndio maana ya hizi ziara.
 
Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.

- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.

- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.

- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Tatizo mbowe huwa hatoi feedback yoyote
 
Mbowe awe makini, CCM sio wa kuamini kuwa wanaweza kuweka mazingira yatayoruhusu wao kuachia dola kwa amani.

Anyway, inawezekana strategy ya CHADEMA ni kwanza kutumia meza ya mazungumzo(wasije kulaumiwa kuwa walikataa hiyo fursa), ili kesho na keshokutwa wakitumia mbinu mbadala, wasilaumiwe.

Kwa maneno mengine, watayokubaliana yatakuwa documented na kuwa public, hivyo ataenda kinyume, ndio atalaumiwa.

Ni mtazamo wangu.
Umeyaweka vyema kabisa.

Ujanja ujanja nao una mwisho wake. Watu wataona wenyewe na kuamua nani wa kulaumiwa mambo yasipokwenda sawa.
 
To open up a new chapter as a nation haijawahi kuwa dhambi...

Hili kama ni kweli bac ni jambo jema kwa kila mwenye pumzi..

Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara lenye umoja na nguvu kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.

Nchi haiwezi kujengwa na mawazo ya upande mmoja.
Tunahama kutoka kwenye siasa za zama za mawe za kale kwenda kwenye siasa za maendeleo uhuru na demokrasia.👏👏👏👏
 
Katiba mpya itoke wapi? We endelea kufanywa mpira wa dana dana huku mwenyekiti na genge lake wakiendelea kuupiga mwingi kupitia mialiko ya raisi. Mmeshaambiwa siku zote hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Jamaa anatengeneza pesa ndefu kupitia siasa uchwara, huku akiwaacha watu wenye misimamo thabiti na chama wakiendelea kutokwa mapovu huko belgium na canada. Endelea na kazi ya kuwarubuni wana mbeya ili itapokuwa inaanzishwa michango ya chama wawe mstari wa mbele kukichangia.
Dudumizi lazima unune sana ukimuona Heche Ikulu🤣🤣

Muachage dharau.
 
Mkuu chadema ya sasa chini ya mwenyekiti wake itakupa presha ya bure. Jamaa anaangalia kwanza masilahi yake na ya familia yake, nyinyi wengine mmeachwa mtetee chama tu mitandaoni. Wengi mtaishia kulalamika tu lakini hamna ujanja wa kumfanya chochote.
Limewashuka leoooo
 
To open up a new chapter as a nation haijawahi kuwa dhambi...

Hili kama ni kweli bac ni jambo jema kwa kila mwenye pumzi..

Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara lenye umoja na nguvu kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.

Nchi haiwezi kujengwa na mawazo ya upande mmoja.
Vigezo na masharti ya ROYO TUWA!
Rudini njia kuu. Rejesheni demokrasia. Tambueni na thamini wapinzani. Shirikianeni kuikwamua nchi yenu!

Next move - kick Covid-19 out!

NB: Sijui ZZK na genge lake wanajisikiaje tu?!
 
Mbinu ya Chadema ni kuionyesha Dunia kwamba Mazungumzo yalishindikana
Usiende mbio hivyo.

Kuna njia nyingi za kuonyesha mazungumzo yalifana, hata kama kiukweli hapakufanyika lolote la maana.

Vuta subira kidogo, picha kamili itaonekana tu haiwezi kujificha.
 
Wanafuata nini ikulu kila mara kama sio kupotezeana muda?
Wanatumia akili kutafuta kinachotakiwa ambacho wewe na wenzako mngetumia zaidi mabavu na kauli chafu za kutweza utu na kuogopesha raia.
Watanzania ni waoga sana na bado wapo usingizini... mkitumia harakati za kuwashurutisha waandamane au watukane tukane hamtotoboa!
 
Chadema mkae macho sana na hawa watu, wanazitaka sana hizi picha za pamoja kwaajili ya kuwarubuni wafadhili, wakati hali halisi uwandani haiko hivyo na matendo yao yamejaa uhuni huni tu. Kama wananchi tunataka baada ya vikao vyenu mnatoka na statement ya pamoja kwa wwatanzania na siyo hizo picha zenu. Pia statement inayotolewa ifanane na matendo yatakayofuata baada ya kikao. Kama vipi achaneni nao hao Ccm nanyi mrudi kwa wananchi kwani walishawaelewa longtime.
Na kama hamjagundua joto la siasa lipo juu sana sasa hivi tena bila hata mikutano ya hadhara, hivyo wanatumia mbinu ya kuwaita na kupiga picha ili kusafiria nyota ya Chadema na kushusha temper ya wananchi. Lakini wanasahau baada tu ya siku mbili tatu unakuta wameshachafua hali ya hewa. Wameshazoea vya kunyonga hao.
Nimekusoma mkuu 'majege'. Hakuna litakalojificha milele hata wakiamua kutosema, mwisho yatatoka tu na tutajua.

Ngoja tuvute subira kidogo kabla ya kuhukumu.
 
Badala ya kuboresha maisha ya watanzania mnakutana na Chadema.
 
Malaika wale, akienda Lipumba Ikulu basi matusi kila kona na kuita wenzao wasaliti..

Akienda mwenyekiti wao, basi burudani kabisa kwao....
Tangu hapo Lipumba ni msaliti kwani ni siri, kufa kwa CUF mpaka kuwa replaced na ACT ni mazao ya usaliti wa Lipumba.
Hivyo msaliti anapoenda huko moja kwa moja ni agenda ya kuendeleza usaliti wake, once a snake always a snake.
 
Dudumizi lazima unune sana ukimuona Heche Ikulu[emoji1787][emoji1787]

Muachage dharau.
JamiiForums-480002814.jpg
 
Back
Top Bottom