Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Siasa ni process mkuu, hata huko Ukraine kuna watu wanachapwa lakini kuna watu wapo underground kuhakikisha vita inakwisha.

Mandela alikuwa akifuatwa na helicopter kwa siri gerezani na kwenda kuzungumza na De clerk ikulu kwa miaka kadhaa mpaka wakakubaliana.

Msione vitu tu vinatokea, leo uhuru Kenyatta na Odinga damu damu ulitegemea hilo?

Hebu jifunzeni modern politics, radical politics hazilipi.

Mkuu mimi sio muumini wa hivi vikao. Hili sio kosa lako ni langu. Muda utaamua.
 
Kama haujui dhuruma alizofanyiwa Maalim Zanzibar basi wewe ni kichaa wa kulazwa. Haufai hata kutembea na hawa tunaona barabarani wakitafuta mabaki ya vyakula majalalani.
Katiba ya Zanzibar utafananisha na JMT? Uko sawa kichwani wewe?

Maalim Seif amefariki akiwa ni makamu wa kwanza wa Rais.
 
Hauko mwenywe mkuu. Vikao hivi tuliviona kule Zanzibar miaka ya 2000 na hawa CCM na "mwafaka" ukafikiwa. Maalim walipowapiga chini kwenye sanduku la kura 2015, wakafuta matokeo ya uchaguzi!! Na samia amekwishasema ni mpaka 2030. Hataki kusikia mtu akiongelea urais huko CCM wala nje ya CCM mtu aongelee katiba mpya.
Mkuu mimi sio muumini wa hivi vikao. Hili sio kosa lako ni langu. Muda utaamua.
 
Wakuu,

Muda huu M/Kiti wa CHADEMA na viongozi waandamizi 9 wa chama hicho wapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Tutarajie jambo gani jipya? Ndo ukurasa mpya wa Siasa za Tanzania?

UPDATE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.

View attachment 2232248View attachment 2232250
View attachment 2232257View attachment 2232258View attachment 2232259

View attachment 2232260
Mungu zidi kuibariki CHADEMA
 
Mbowe awe makini, CCM sio wa kuamini kuwa wanaweza kuweka mazingira yatayoruhusu wao kuachia dola kwa amani.

Anyway, inawezekana strategy ya CHADEMA ni kwanza kutumia meza ya mazungumzo(wasije kulaumiwa kuwa walikataa hiyo fursa), ili kesho na keshokutwa wakitumia mbinu mbadala, wasilaumiwe.

Kwa maneno mengine, watayokubaliana yatakuwa documented na kuwa public, hivyo ataenda kinyume, ndio atalaumiwa.

Ni mtazamo wangu.
We salary sleep had muda huu hujui ishu ni covid 19
Mbona unaniangusha mzee
Mengine ni uwanja wa siasa sio ya kuachiana ni ya kushindana
 
Yupo kimkakati hapo, mama akishalamba mitano tena ndio atapumzika.

Bado kuna waasi ccm sasa huyu Kanali ndio mtu sahihi kuwanyoosha na kumuweka mama salama bila kumjaribu, huyu ni Comrade.
Kwa hiyo 2025 Chadema mmekubaliana hakuna wa kumzuia Samia?? Ok tusubirie 2030 lisu ataachiwa urais 😂😂
 
Chadema imegawanyika kwenye hili, Wamarangu na Machame wako na con man Mbowe na wanaona ni sawa ili kumlinda corrupt Mbowe na chadema second class wa Mikoa mingine wana doubt hii move, ngoja tuone itakavyokuwa!
 
Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.

- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.

- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.

- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Duh, umegusa 'buttons' zote zenye maumivu kwa CHADEMA katika andiko fupi kabisa!
Acha tusikie yatakayoletwa kwetu juu ya mkutano huo.
 
Back
Top Bottom