Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Hizi ndiyo siasa za kistaraabu, siyo viongozi wanangania kutotambui matokeo ya uchaguzi wa 2020 na matunda yake.
-Nenda kwenye meza ya mazungumzo kuyajenga,
-Tume ya uchaguzi ikitangaza matokeo hizi nchi zetu za Africa kubadilisha inakuwa ngumu sana.
-Matokeo yakitangazwa saa 8 usiku tegemea Raisi ataapishwa kesho yake.
-Hawatoi muda wa asiyeridhika na matokeo kukata rufaa mahajama.
-Ni vema tukawa na Mahakama ya Katiba.
-Africa kusini na Kenya wenzetu Wana Mahakama za Katiba na matokeo ya uchaguzi yanaruhusiwa kupingwa mahakamani ,na Mahakama ikaruhusu kurudia uchaguzi.
-Katika hao wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA naibu Katibu Mkuu Kigaila yumo,kwa maana huwa anatoa statement ambazo hazina mashiko mara nyingi.
-Mchezo wa siasa hautaki hasira.

Ushauri
-Chadema Wana kila sababu ya kuumpa ushirikiano Mama SSH kwa kupeleka wabunge wa viti Maalum 19 vilivyopatikana kutokana na asilimia za kura za uraisi na wabunge kwenye uchaguzi wa 2020.
-Wabunge hawa watapeleka agenda mbadala kwa niaba ya wananchi/Chadema Bungeni.japakuwa ni wachache,
-CCM/CHADEMA /ACT wazalendo wawashauri Wabunge wao wawe wanawasilisha matatizo au maoni ya wapiga kura wa kwenye majimbo yao au wananchi kwa kufanya mikutano na wananchi kusikiliza matatizo yao kabla ya kwenda bungeni.
-Wabunge wa CCM/CHADEMA/ACT wazalendo wawe wanatoa hoja na ushauri wa kujenga nchi,kwa Uhuru na bila uoga.
-Yaliyopita si ndwele tugange yanayokuja
-Hongera Sana viongozi wakuu wa CCM na CHADEMA kwa kukutana na kuyajenga . -Wananchi tunataka amani itamalaki ,ili kazi ziendelea.
 
Watu wanadharau sana. Sijui kwanini, utadhani wao tuu ndio wamepewa akili na mungu na wengine wakanyimwa
Unadhani akili za Lisu ni kama za kabudi? Watu wanatofautiana sana tena sana kufikiri. Kama umesoma some history of science, Albert Einstein alipopendekeza theory of relativity, wharping of spacetime and the like dunia nzima ya Scientists haikumuelewa. But later walimshangaa kwa kiwango alichokuwa nacho baada ya kumuelewa. Na mpaka leo hakuna mwanadamu kama yeye kwa akili alizokuwa nazo.
Likewise Tanzaia, kuna wachache kama 0.000000000000000000000000001 wana uwezo wa kufikiri sawasawa
 
Picha hii ya Ikulu Chamwino inanikumbusha zile za Korea ya Kaskazini

1653105804584.png

1653106002397.png

1653106066496.png
 
To open up a new chapter as a nation haijawahi kuwa dhambi...

Hili kama ni kweli bac ni jambo jema kwa kila mwenye pumzi..

Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara lenye umoja na nguvu kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.

Nchi haiwezi kujengwa na mawazo ya upande mmoja.
Mimi sielewei mbona Zitto alibezwa alipoanza hii political reconciliation???
 
kichwa cha mada chajitosheleza..watamtukana,watamkebehi,watamdharau,watasema anajifanya anamuiga JK.. ila hawataona nia njema yake..

Je hawa watu huwa wanataka nini kilichojificha mioyoni mwao..hasa kuhusu siasa za Tanzania
 
Siasa za bongo Hazina watu serious.

Zimejaa wajanja wachache wanaotafuta Ugali na kundi kubwa sana la misukule wanaoishi na ndoto za alinacha, huku wakiendaga kutajirika Genge dogo Lile Lile miaka kwa miaka.
 
kichwa cha mada chajitosheleza..watamtukana,watamkebehi,watamdharau,watasema anajifanya anamuiga JK.. ila hawataona nia njema yake..

Je hawa watu huwa wanataka nini kilichojificha mioyoni mwao..hasa kuhusu siasa za Tanzania
Kwa mfano nani aliyechukia!? Waambieni Boss hanuniwi watulie kazi iendelee
 
kichwa cha mada chajitosheleza..watamtukana,watamkebehi,watamdharau,watasema anajifanya anamuiga JK.. ila hawataona nia njema yake..

Je hawa watu huwa wanataka nini kilichojificha mioyoni mwao..hasa kuhusu siasa za Tanzania
Wivu, husuda, kijicho [emoji23]
 
NAAM..!
Pamoja na changamoto zilizopo, Ukweli ni kuwa Rais SSH anafanya vizuri sana kurejesha umoja wa nchi yetu. Japo bado kuna giza ...Lakini kwa mwendo huu asubuhi tutaiona. Katiba mpya itapatikana, Uhuni utapungua kwa kiasi kikubwa. Cha muhimu ni uvumilivu.
 
kichwa cha mada chajitosheleza..watamtukana,watamkebehi,watamdharau,watasema anajifanya anamuiga JK.. ila hawataona nia njema yake..

Je hawa watu huwa wanataka nini kilichojificha mioyoni mwao..hasa kuhusu siasa za Tanzania
Ukiona hivyo ni wamichongo🚶
 
Hii nchi bwana ni vituko tu. Lema anauliza Vita ys Ukraine itaisha lini?
FTPo4k6X0AAS_Sy.jpeg

Ati nao Ikulu nao wanahoji huko Canada watu huwa wajula nini?
20220521_071533.jpg

Sasa hapo sijui tumjibu nani?😂😂😂
 
Hizi ndiyo siasa za kistaraabu, siyo viongozi wanangania kutotambui matokeo ya uchaguzi wa 2020 na matunda yake.
-Nenda kwenye meza ya mazungumzo kuyajenga,
-Tume ya uchaguzi ikitangaza matokeo hizi nchi zetu za Africa kubadilisha inakuwa ngumu sana.
-Matokeo yakitangazwa saa 8 usiku tegemea Raisi ataapishwa kesho yake.
-Hawatoi muda wa asiyeridhika na matokeo kukata rufaa mahajama.
-Ni vema tukawa na Mahakama ya Katiba.
-Africa kusini na Kenya wenzetu Wana Mahakama za Katiba na matokeo ya uchaguzi yanaruhusiwa kupingwa mahakamani ,na Mahakama ikaruhusu kurudia uchaguzi.
-Katika hao wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA naibu Katibu Mkuu Kigaila yumo,kwa maana huwa anatoa statement ambazo hazina mashiko mara nyingi.
-Mchezo wa siasa hautaki hasira.

Ushauri
-Chadema Wana kila sababu ya kuumpa ushirikiano Mama SSH kwa kupeleka wabunge wa viti Maalum 19 vilivyopatikana kutokana na asilimia za kura za uraisi na wabunge kwenye uchaguzi wa 2020.
-Wabunge hawa watapeleka agenda mbadala kwa niaba ya wananchi/Chadema Bungeni.japakuwa ni wachache,
-CCM/CHADEMA /ACT wazalendo wawashauri Wabunge wao wawe wanawasilisha matatizo au maoni ya wapiga kura wa kwenye majimbo yao au wananchi kwa kufanya mikutano na wananchi kusikiliza matatizo yao kabla ya kwenda bungeni.
-Wabunge wa CCM/CHADEMA/ACT wazalendo wawe wanatoa hoja na ushauri wa kujenga nchi,kwa Uhuru na bila uoga.
-Yaliyopita si ndwele tugange yanayokuja
-Hongera Sana viongozi wakuu wa CCM na CHADEMA kwa kukutana na kuyajenga . -Wananchi tunataka amani itamalaki ,ili kazi ziendelea.

Kwamba unahalalisha chaguzi za kihuni kuwa hata ufanyike uhuni wa wazi vipi, inabidi ukubaliane nao kwa huku ni Afrika ama? Kwa hiyo wewe kwako amani itapatikana tu hata mtu akifanyiwa uhuni vipi! Sasa kama unahalalisha chaguzi kunajisiwa tunaenda kupiga kura ili iwe nini?
 
Mtu bado anakukanyaga makusudi halafu anakwambia usilalamike, bado tupo kwenye meza ya mazungumzo, kuwa mvumilivu!
Unachosema ni sahihi lakini bahati mbaya sana mkuu hutoi alternative wanafanye nini badala yake.
Chadema wanaangalia na aina ya jamii tuliyonayo. Mbali na maridhiano njia pekee ni maandamano na kufanya nchi isitawalike. Yuko wapi mwananchi wa kufanya hayo? Wazee wa nchi wapo kimya,wamejaa unafiki,wananchi wanalalamika kichini chini. Sisi wachache mimi na wewe tumejificha kwenye keyboard. Mbowe afanye nini zaidi ya kutumia fursa ya kukaa meza moja.
Kukaa meza moja pia haimaanishi kusaliti misisimamo bali kueleza misimamo badala ya kutunishiana misuli kwenye majukwaa. Utatuna msuli jukwaani lakini ili unayemtunishia akupate vizuri inabidi akusikilize ukiwa kwenye utulivu na umweleze kwa ufasaha.

Ni kipi ambacho Chadema hawajafanya katika kutunisha misuli. Waliingia barabarani ikapalekea mauaji kesi ikawageuka na wananchi hawakuchukua hatua yeyote. Mbowe kakaa jela,Lissu kapigwa risasi mchana. Uchaguzi kura zimeibwa nk Wananchi walichukua hatua gani kali?

Naunga mkoni maridhiano kwa sababu hayupo raia wa kuingia barabarani kutumia nguvu ya umma
 
Mmekosa ajenda mafirauni nyie. Mliwatukama ACT leo hamna la kusema. Rais akiamua hata kutokukutana na Chama chochote atatawala tu. Poor idiots .
Mkuu
Wanaccm Lazima tuwe na uwezo wa kufikiri sawasawa!
JIWE alinajisi uchaguzi nini kilimpata!!?Hadi akaingiza covid-19 Bungeni na haikutosha Hadi ikaigharimu serikali take!!!?
Unafikiri Sasa HIVI Kati ya mama na Mbowe nani anamuita mwenziwe IKULU!!?kama SERIKALI haioni umuhimu wa UPINZANI!!? HIVI unajua kesi ya MBOWE ilikuwa inaenda kuigharimu serikali ndio maana watu walitumwa wammbembeleze Mbowe atoke na alipototoka akaitwa ikulu Moja kwa Moja!!?
NAJUA MADARAKA YAMEPOFUSHA WANACCM WENGI NA HAWAONI MAMBO SAWASAWA!!

NIKUJUZE TU KIFUPI NI KWAMBA KUONDOLEWA KWA WABUNGE WA COVID-19 NI MAAGIZO YA THE STATE KWA MAMA SASA MAMA ANAOGOPA WAKIONDOKA NA SERIKALI YAKE ITAKUFA!!
SASA ANATAKA CHADEMA IRIDHIE WABAKI KIBISHI KINYUME NA TARATIBU HAPO NDIO KAZI!
KAMA UNAFIKIRI RAIS ANAWEZA TAWALA BILA UPINZANI BUNGENI NENDA KAMUULIZE JPM CHATO KWANINI ALITAFUTA WABUNGE WA UPINZANI KWA MLANGO WA NYUMA!!!!
I REST MY CASE
Naongezea kuwa uwepo wa covid-19 Bungeni ni kufeli kea Tiss kwenye uchaguzi wa 2020 kwasababu Tiss walicheza tune ya CCM wakati wa uchaguzi wakasahau utaifa SASA Tiss imeikosea NCHI na the state haitokubali ujinga kama huo tena na LAZIMA katiba MPYA ipatikane Ili kuepuka ujinga kama ule mlioubariki uchaguzi 2020!!!TISS ITUBU KWA KUINGIZA TANZANIA MATATIZONI NDIO MAANA WAKABARIKI UHUNI WA COVID 19 ILI KUINUSURU SERIKALI YAKE KISHERIA ZA KIMATAIFA NA UHALALI WAKE!!!
UMENIELEWA!!
 
Unachosema ni sahihi lakini bahati mbaya sana mkuu hutoi alternative wanafanye nini badala yake.
Chadema wanaangalia na aina ya jamii tuliyonayo. Mbali na maridhiano njia pekee ni maandamano na kufanya nchi isitawalike. Yuko wapi mwananchi wa kufanya hayo? Wazee wa nchi wapo kimya,wamejaa unafiki,wananchi wanalalamika kichini chini. Sisi wachache mimi na wewe tumejificha kwenye keyboard. Mbowe afanye nini zaidi ya kutumia fursa ya kukaa meza moja.
Kukaa meza moja pia haimaanishi kusaliti misisimamo bali kueleza misimamo badala ya kutunishiana misuli kwenye majukwaa. Utatuna msuli jukwaani lakini ili unayemtunishia akupate vizuri inabidi akusikilize ukiwa kwenye utulivu na umweleze kwa ufasaha.

Ni kipi ambacho Chadema hawajafanya katika kutunisha misuli. Waliingia barabarani ikapalekea mauaji kesi ikawageuka na wananchi hawakuchukua hatua yeyote. Mbowe kakaa jela,Lissu kapigwa risasi mchana. Uchaguzi kura zimeibwa nk Wananchi walichukua hatua gani kali?

Naunga mkoni maridhiano kwa sababu hayupo raia wa kuingia barabarani kutumia nguvu ya umma

Mkuu je hayo maridhiano yatawalipa CDM, au ndio wamehalalisha uhuni uwe unafanyika kisha wanaitwa kukaa kwenye meza ya mazungumzo? Huu uhuni tunauona sana Zanzibar, huko wapinzani huwa wanaoporwa uchaguzi, wafuasi wake wanauwawa, kisha baada ya uchaguzi viongozi wanaitwa wanaelewana wawili watatu wanapewa ulaji, ikija uchaguzi mwingine uhuni na mauaji unafanyika tena, kisha mazungumzo tena! Katika mazingira hayo mtu anategemea mimi niunge mkono hayo mazungumzo, au nijitokeze tena kupiga kura? Never.
 
Kwa hali ilivyokuwa katika utawala wa awamu ya5 hata CCM wenyewe watakuwa wamepata fundisho kuwa kuna haja ya kufanya mabadiliko katika mambo fulanifulani hasa katika jambo la kuleta katiba mpya.

Baada ya nchi kupitia kwenye mkono wa utawala wa kishetanni ambao haukuwa na huruma hakuna mwana CCM yeyote mwenye akili timamu ambaye anaweza akapinga mabadiliko ya katiba.
 
Mkuu je hayo maridhiano yatawalipa CDM, au ndio wamehalalisha uhuni uwe unafanyika kisha wanaitwa kukaa kwenye meza ya mazungumzo? Huu uhuni tunauona sana Zanzibar, huko wapinzani huwa wanaoporwa uchaguzi, wafuasi wake wanauwawa, kisha baada ya uchaguzi viongozi wanaitwa wanaelewana wawili watatu wanapewa ulaji, ikija uchaguzi mwingine uhuni na mauaji unafanyika tena, kisha mazungumzo tena! Katika mazingira hayo mtu anategemea mimi niunge mkono hayo mazungumzo, au nijitokeze tena kupiga kura? Never.
Mkuu badala yake wafanye nini? Waandamane? Wako wapi waandamanaji
Waingie msituni? Liko wapi jeshi la kuingia msituni?
 
Back
Top Bottom