Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Boss Mpinzire Je, Katiba na Sheria zetu za Nchi zinasemaje kuhusu Siasa??? Maana umeauliza kuhusu Siasa.
Labda tuanzie hapo ... Den ukishajibu ndio tutaendelea kuchangia ....
Nchi inaongozwa na Katiba na Sheria ....
 
1576152128773.png
 
Hahahaha
Wakurupukaji hawa jamaa walipigialo kelele leo kesho watalipinga
Hawajui Wmetoka wapi
Wapo wapi na wanaelekea wapi
Hovyo hovyo full mkurupuko!!
 
Either with us or against us, hakuna maridhiano na wasaliti.
Ccm ndio actually wenye kuhitaji maridhiano zaidi kuliko hata hao Chadema na usishangae ndio engineers wa huu mkakati.

Ccm kama bado wana ambition ya kutawala hii nchi kwa miaka ijayo wajue wazi kuwa "They can't traverse the formidable jungle themselves".

Wasaliti ni wale walioshuhudia rasilimali za nchi zikiporwa kwa miaka mingi bila kupinga na leo wanarudi kujifanya eti ndio wazalendo, hata maana ya neno uzalendo hawalijui.

Kwa lugha sahihi hawa ni wanafiki wanaotafuta sifa feki ili kuhadaa wajinga wawaone kuwa ni wazalendo hawa ni wazalendo wa majukwaani. Hawana maana kabisa.
 
Ni kweli yapo maumivu, japo Watanzania walio wengi tunayaona yana nia njema. Ukiwa Baba wa familia wakati mwingine utalazimisha watoto wale mahalagwe mfululizo ili mjenge muondokane na kupanga. Ukijifanya mwenye huruma ukasikiliza vilio vya watoto mtaendelea kupanga siku zote na baadaye watoto hao hao watakubeza kukuona ulikuwa Baba dhaifu. Tuliyasema mengi tena ya kashifa kwa JK Mlisho. JPM akaze Uzi ule ule, ili tupate meza nzuri ubao lazima ulandwe.

Hoja ya mboye ni ya Msingi "maridhiano" lakini anaridhiana na nani? Mbowe na wore wanaochagiza chama tawala wamepoteana. Suala muhimu ni kuhakikisha kwa haraka iwezekanavyo fanyeni muungano wa dhati na hulka ya umimi muiweke pembeni mjenge umoja wenye nguvu kudai mnachokidai, sasa hivi sauti yenu imekuwa dhaifu sana kiasi cha kutokuaminika.

Nadhani ni busara kwamba kwa uchaguzi 2020 hamuwezi kushinda chama tawala niwaombe kiti cha urais ( haya ni maoni yangu) achaneni kugombea kiti cha urais mwacheni apite, jengeni hoja pesa ambazo zingetumika kwa kampeni za urais ziingie katika kuimalisha vyama vya upinzani ili pia kuepuka vyama vya upinzani kuishi kwa kutembeza bakuli ughaibuni jambo ambalo liwalazimu kukumbana na masharti ambayo mengi yanakinzana na utamaduni wetu na unweza kuiathiri amani yetu.

Ni vizuri kumpa nguvu mpinzani wako ili hata pale atakapokukosoa akukosoe kwa upendo nadhani hayo ndo maridhiano. Huu ni ushauri kwa chama tawala na upinzani.pia
Tujenge umoja wetu sote ni Watanzania, watu wa nje wasitugawe kwa sababu hiyo ni mbinu yao kubwa na tuitakie mema Tanzania ya kesho.

Kwa CCM kumshinda mpinzani wapo mpaka kumchakaza kabisa siyo sifa pia hata bondia akimpiga Nguni ya uso upinzani hadi hadi kumlambisha sakafu hugeuka na kumwinua na mchezo ukiisha hukumbatiana. Nadhani siasa siyo mchezo mbaya kuzidi wa ngumi. In politics the is no permanent enemy and no permanent friend. Tusiwape nafasi wasiotutakia mema.
 
Mh Rais John Pombe magufuli amerudia Tena kwamba hataongeza hata siku moja katika utawala wake Hilo ni Jambo la kupongezwa.

Bado umebakiza Mambo kadhaa ili historia ikusamehe na ikuandike vizuri fungua mlango wa maridhiano na upinzani kitu ambacho ni kizuri kwa ustawi wa taifa.

Shida ninayoiona bado Kuna kila dalili ya kushupaza shingo. Tanzania ni yetu sote.
 
Maridhiano Kwani wapo kwenye mgogoro gani?

Au mnataka mkale tende ikulu
 
Maridhiano yatakuwepo wewe Mbowe ukiacha udikiteta kwa kuwaachia na wengine uenyekiti.
 
Kila mmoja kwa wakati wake,hawa wenyeviti wetu wa upinzani mnaomba poo!

Je ni lini mlitangaza kugombana na JPM?

mnaomba maridhiano kwa ajili ya kufuta ile kauli yenu ya NCHI HAITATAWALIKA a.k.a "●ukuta"?

Ebu kuweni wakweli ni maridhiano gani mnayoyaongelea nyinyi wakuu MBOWE + mbatia# kama taifa tunahitaji maridhiano[emoji1241]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano.

Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:

Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!

Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.

Nawapongeza sana Watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.

Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.

Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh Freeman Mbowe katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
Kumbe ilianza kitambo
 
Unaenda kumpigia magoti mtu aliyemtandika risasi 38 nduguyo utadhani anaua CHATU na kama haitoshi akaendelea kumshughulikia vivyo hivyo huku akiwa hoi kitandani.

CHADEMA hakuna kitu
KUkaa ndani miaka miaka miwili haikuwa poa
20250115_233501.jpg
 
Back
Top Bottom