Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Pole mko wengi msiyoelewa maana ya maridhiano. Na tatizo kubwa liko upande ule wa kijani. Kudhani nchi hii ni ya kwao pekee. Wengine hawakujaaliwa ufahamu wa kutosha. Lakini kuna wengi sana hasa wasomi tuliyowahi kuwaamini wanaongozwa na matumbo yao. Maridhiano yatawapunguzia mkono kwenda kinywani.
Mbowe anatapa tapa tu
Bada ya watu kugoma kuwabembeleza wanataka maridhiano,watu tupo bize nyakati hizi yeye aendelee na kususa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
State Agent ndiye terrorist mlimpiga Lissu risasi hakuna aliyeshitakiwa, sasa terrorist ni nani??
Wacha watu wenye akili watafute amani maana wewe huna shida unaishi Lumumba pale Mnazi Mmoja!!
 
Pole mko wengi msiyoelewa maana ya maridhiano. Na tatizo kubwa liko upande ule wa kijani. Kudhani nchi hii ni ya kwao pekee. Wengine hawakujaaliwa ufahamu wa kutosha. Lakini kuna wengi sana hasa wasomi tuliyowahi kuwaamini wanaongozwa na matumbo yao. Maridhiano yatawapunguzia mkono kwenda kinywani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwan kuna ugomvi gani mpaka turidhiane?
 
domokaya,
Hayo hayakufanyika sababu hakuna demokrasia,Kama raia wangekuwa na uhuru wa kukutanika na kufanya mikutano ungeamini kuwa mawazo yako Ni choo kabisa.

Kama unabisha acheni Uhuru muone mziki wake kwa mikutanona huenda bana kuba akakosa kura milioni mbili mwakani na huu ukweli pia anaujua
 
CCM na Jiwe wanajua maridhiano ina maana wahatarishe ushindi wao kwenye sanduku la kura.CCM bila figisu(kusaidiwa na polisi na vyombo vingine Vya dola),ushindi kwao inakuwa 50/50,wanaweza kushinda au wasishinde.Ni sawa na kumuambia mtu aliyezoea kuishi kwa wizi aishi kwa njia halali!
 
Hayo hayakufanyika sababu hakuna demokrasia,Kama raia wangekuwa na uhuru wa kukutanika na kufanya mikutano ungeamini kuwa mawazo yako Ni choo kabisa.

Kama unabisha acheni Uhuru muone mziki wake kwa mikutanona huenda bana kuba akakosa kura milioni mbili mwakani na huu ukweli pia anaujua

Hicho unachokizungumza ni demokrasia gani? Demokrasia ina misingi yake na mikutano ya hadhara si mmoja wa misingi ya demokrasia. Hata hivyo kipi ambacho kingezungumzwa katika mikutano ya hadhara upinzani unashindwa kukizungumza? Wewe na wenzako MNA Uhuru mpaka wa kutukana, unatukana humu na mnatukana kila mahali. Hebu Sema wewe binafsi Uhuru wako UPI umeminywa? Watanzania sio wajinga, wanafahamu chama kipi cha maboy friend, ma girl friend na usagaji na wanajua chama kipi cha kukipa ridhaa. Haiwezekani chama miaka yote kisubiri makombo kutoka CCM kiwafanye kuwa wagombea wananchi wakiamini. Leo watu wajinga wanasema eti mikutano ya hadhara hakuna, mngeenda kusema nini? Kina Patrobas, Kafulila, Shonza, Slaa wangewamaliza kwa dakika mbili tu, tens mshukuru sana. Msifikiri CCM ya Leo ni ile ya juzi, CCM ya Leo imejaa watu wanaowafahamu uzuri,na kama kuisoma namba mtumeisoma uzuri, mpaka akina Prof Safari wamechoka kuna mini tens hapo? Kilichobaki ni kutiana mimba na kusagana tu, siasa tens kwishney!
 
Game changer yupo kazini Hongera JPM Watanzania watakukumbuka katika Maisha yao yote. Jina lako litakuwa ndio limeikomboa Afrika kwa ujumla. Wazungu ambao walikuwa wanakula bila kunawa mikono sasa wanaandaa plan 'B' wakati Watanzania wameondoka kwenye ule usingizi ambao uliwakumba wakati wa uongozi wa BWM na JMK.
 
Amani iwe nanyi wanajamvi....!
Binafsi nimetafakari kwa kina juu ya ombi la Mh Freeman Mbowe (MB) kwa Mh Rais Magufuli kwa kumsihi Mh Rais kuwa Taifa linahitaji maridhiano, Je? kweli Taifa linahitaji maridhiano ama wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani ndiyo wanahitaji maridhiano ili waachiwe mwanya wa kufanya siasa bila mipaka?

Binafsi naamini Mh Rais akisema niko tayari kujadiliana na vyama vya upinzani hoja yao itakuwa waachiwe wafanye siasa popote bila sharti kama la sasa linalowatesa, Je, hii itakuwa hitaji la Taifa ama hitaji la wanasiasa?

Wanajamvi nawasilisha kwenu tujadili
 
Mbowe anataka tufanyia uhuni kama alioufanya 2015 kumpokea Lowasa, ukiukwaji wa haki za binadamu mwingi umefanyika mataifa ya nje yameona jinsi mambo yanavyoenda hakuna uhuru wa kujieleza nk, chaguzi iliyopita ya serikali za mitaa ilikuwa ni ushahidi tosha kwa yaliyotendeka sasa tumekaribia kwenye peak watanzania wamechoka mbowe kaitwa uko wanapojuana kadiwa donge nono anakuja na hoja zake eti maridhiano maridhiano yepi hayo ya uchaguzi urudiwe wa serikali za mitaa au vipi

Kiukweli wana siasa wetu tatizo sana
 
Viongozi wa kisiasa ndo wananchi wenyewe,na wao ndo wanaweza wakaliponya taifa ama kuliangamiza.
 
Mh.Mbowe anahitaji kuendelea na cheo chake cha Kiongozi wa Upinzan Bungen
 
Mbowe anataka tufanyia uhuni kama alioufanya 2015 kumpokea Lowasa, ukiukwaji wa haki za binadamu mwingi umefanyika mataifa ya nje yameona jinsi mambo yanavyoenda hakuna uhuru wa kujieleza nk, chaguzi iliyopita ya serikali za mitaa ilikuwa ni ushahidi tosha kwa yaliyotendeka sasa tumekaribia kwenye peak watanzania wamechoka mbowe kaitwa uko wanapojuana kadiwa donge nono anakuja na hoja zake eti maridhiano maridhiano yepi hayo ya uchaguzi urudiwe wa serikali za mitaa au vipi

Kiukweli wana siasa wetu tatizo sana
Kama unaona maridhiano hayafai, tufanye nini?
 
Wananchi hatuna shida na Nchi vibaraka wa mabepari ndio wanaojifanya Nchi haina maridhiano ,wakati wao ndio wanaojifanya kutaka Nchi iparaganyike
 
Back
Top Bottom