Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Mnaona yanayoonekana kwa nje; yanayofanyika kwa ndani hayaonekani, lakini yapo na yatajulikana kwa wakati wake
Kwa maneno haya ndani ya bahasha basi sitosema niliyotaka kusema, maana nilijiandaa kukutapikia nyongo. Acha nisubirie bahasha itakapo funguliwa.
 
Akili za kuvukia barabara hizi, ulisoma shule gani ambayo mwalimu alikuwa hafundishi kwa mifano? Hebu ficha uninga wako walau hata kidogo tu.
Kwa hio kwenye bandiko la TL bata ni nani?
CCM?
Tueleweshe basi
 
Bado sijaona wala kusikia hoja yoyote iliyonishawishi kuwa taifa linahitaji maridhiano, kama alivyoomba Bwana Mbowe hapo jana.

Hatuna sababu ya kufanya maridhiano.

Ila, kinadharia tu, hebu ngoja niulize.

Tukishafanya hayo maridhiano, ina maana siasa za ushindani ndo mwisho wake, siyo?

Mwakani uchaguzi utakuwa hauna maana tena, siyo?

Baada ya hayo maridhiano, hakuna tena kufanya kampeni za kisiasa na kukosoana kwa maneno makali, siyo?

2020 Magufuli anaendelea kuwa rais na anawapa nafasi za uwaziri wapinzani.

Maisha yanaendelea kwa sababu tumefanya maridhiano....hakuna tena kukosoana, kushitakiana, kushindana, na kadhalika, kwa ajili ya manufaa ya taifa.....

SMDH
 
Je chadema wanakiri bila kinyongo kuwa JPM ni rais wao na pia wamwombe msamaha JK kwa kususa sherehe zote za uhuru wakati wa awamu yake !
 
Ukishakubali kuolewa inabidi ulale vile anavyotaka mumeo. Period.
 
Kwani maridhiano ni nini? Hebu tuanzie hapa, nilishawahi kumsikiliza mbatia akasema kwa tulipo fikia sasa, siasa za kibabe zitaleta zaidi mgawanyiko ktk jamii hivyo suruhu pekee ni maridhiano ya kisiasa. Tulipofika ni pabaya kila mtu akitunisha msuli anayeumia ni mmoja tu.
 
Chadema wana akili sana! The Gambler knows Secret to survive is knowing what to through away and what to keep.
 
Baada ya Mbowe kuomba maridhiano na serikali ya CCM inadaiwa Chama cha Mapinduzi kimeamua kumuunga Mkono Mbowe kuwa mwenyekiti wa kudumu kama fadhila.

Baadhi ya makada wa CCM wamedai Mbowe ni kiongozi anaefaa kusimamia maridhiano yanayoendelea kati ya CCM na Chadema kwa mstakabali mwema wa nchi yetu..

Wameongeza kuwa zile kelele za kutaka Mbowe aachie madaraka ziliisha rasmi juzi baada ya Mbowe kupewa nafasi ya kuongea kwenye sherehe za uhuru.
 
Huwa najitahidi kukuelewa lakini nafikiri nahitaki tuition zaidi ipo siku nitakuelewa.
 
[emoji777]Mlikataa matokeo ya Urais

[emoji777]Mlimkataa Rais na kusema hamumtambui;

[emoji777]Mlikataa kushiriki kuapishwa kwake;

[emoji777]Mlikataa kumsikiliza Bungeni na mkatoka nje (mwenzenu Zitto aka Kigogo alishafanya maridhiano maana siku hii alibaki Bungeni);

[emoji777]Mlimuita Rais anayewaletea wananchi maendeleo kuwa ni Dikteta;

[emoji777]Mkapanga Maandamano (UKUTA) kuvuruga amani ya nchi;

[emoji777]Mkazunguka Dunia nzima kumshtaki na kujaribu kuidanganya dunia, mkashangaa wazungu hao hao wanaleta misaada na wanakuja kuwekeza;

[emoji777]Mnamzushia tuhuma mbalimbali za kijinga;

[emoji777]Mkafurahia hujuma za ndege kukamatwa;

[emoji777]Mkasusia baadhi ya chaguzi ndogo;

[emoji777]Mkasusia uchaguzi wa Serikali za Mitaa;

[emoji777]Mkatangaza kutowatambua viongozi wa Serikali za Mitaa;

*Katika yote bado Mzee Baba kama hawaoni vile:*

[emoji457]Ameimarisha uchumi wa nchi kwa kuongeza mapato ya Serikali na nidhamu ya matumizi;

[emoji457]Anajenga barabara na madaraja yakiwemo maflyover;

[emoji457]Anatoa elimu bure kwa bilioni 23 kila mwezi;

[emoji457]Anajenga vituo vya afya 480 na hospitali za wilaya 90 na za Kanda 8;

[emoji457]Amenunua ndege 11 mpya "cash."

[emoji457]Anajenga reli ya kisasa SGR kwa trilioni 7 cash;

[emoji457]Anajenga mradi wa umeme Rufiji Trilioni 6.5 cash;

[emoji457]Ametoa Bilioni 153 kuunda meli mpya na kukarabati zingine 3 na cherezo kimoja;

[emoji457]Anajenga daraja la Kigongo Busisi kwa bilioni 700 cash;

[emoji457]Ametoa fedha kwa wakati za mikopo ya elimu ya juu zaidi ya bilioni 450 na hakuna tena maandamano vyuoni;

[emoji457]Anasambaza umeme vijijini kwa kasi zaidi, afikisha vijiji 9,000 na kufikia 2021 vijiji vyote 12k nchini vitakuwa na umeme.

[emoji457]Anajenga mabweni ya wanafunzi, majengo ya vyuo, madarasa n.k

[emoji457]Anajenga Daraja la Wami, kakamilisha daraja la kihistoria la Sibiti na sasa ameanza kupanua Barabara Dar kwenda Kibaha kwa njia nane;

[emoji457]Mkoa wa Kigoma uliochoka sasa unaunganishwa na Tabora na Katavi na Kagera kwa barabara za lami;

[emoji457]Anainda meli mpya Ziwa Tanganyikabna kuikarabati MV Liemba;

[emoji457]Amewalipa wakulima wa korosho bei nzuri baada ya kutaka kunyonywa na makabaila weusi na weuoe, ametumia Bilioni 700;

[emoji457]Heshima imerudi mjini na hata Krismas hii tunaheshimiana hapa mjini;

[emoji457]Nimetua Moshi juzi tu, katugusa sisi wa Machame, karejesha treni safi baada ya kukarabati reli;

[emoji457]Kahamasisha viwanda na tunaviona vinajengwa na watu wanapata ajira;

[emoji457]Madini mnajua, wale wa kujimwambafy Acacia wako chali, wamebaki wanaumeeee Barrick na sisi mezani tunagawana chetu kwa haki;

[emoji457]Mirerani shamba la Bibi la Tanzanite kaigeuza kuwa hub ambapo mapato yanepanda kutoka Milioni 70 hadi Bilioni 2.5;

[emoji457]Mapato sekta ya madini kwa ujumla yameongezeka kutoka Bilioni 191 hadi Bilioni 320 na mwaka huu wataalamu wanasema yatavuka Bilioni 400;

[emoji457]Anatoa mshahara kwa watumishi wa umma haizidi tarehe 23 ya mwezi bila kukosa.

[emoji457]Kaongeza mshahara kwa watumishi kwa njia ya annual increament kwa watumishi zaidi ya laki 3 na kapandisha madaraja watumishi zaidi ya laki 5 ikiwa ni baada ya kusimamia tangu mwaka 2013;

[emoji457]Kashusha kodi kwenye mishahara kutoka asilimia 14 mpaka 9;

[emoji457]Kaweka rekodi ya makusanyo ya mwezi kufikia trilioni 1.7, haijawahi kutokea tangu nchi hii iwepo na kabla haijakuwepo;

[emoji457]Katimiza ahadi ya miaka 40 ya nchi kuhamia Dodoma na kila aliyehamia kalipwa haki zake hakuna madeni;

[emoji457]Kajenga mji mpya wa Serikali Dodoma na anaendelea kujenga;

[emoji457]Kawabana mafisadi sawa sawa na kaanzisha mahakama maalum;

[emoji457]Kakamilisha ujenzi wa megawati 240 umeme wa gesi Kinyerezi II na anakamilisha Kinyerezi I extension megawati nyingine 185;

*Niendelee????......... inatoshaaaaa!!!*

Kama haya na mengineyo yamefanyika bila MARIDHIANO mi naona nyie endeleeni kususa tu, sisi tuendelee kutekeleza.
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa umemalizika na chama tawala kimepita bila kupingwa baada ya wagombea wa upinzani kuelezwa na wasimamizi wa uchaguzi kuwa hawakukidhi vigezo na hivyo kuenguliwa. Hali hii imewaacha watazania wakiwa hawajui wafanye nini ili kupata viongozi wanaoendana na matwaka pamoja na matarajio yao ya miaka mitano ijayo.

Katika taharuki hiyo wapo wanaosema yamepita na tuendelee na Maisha kama kawaida. Pia wapo wanaodhani kuna sababu ya kutatua kasoro zilizopo na kuwepo na maridhiano ili umoja na ushiriki wa kila Mtanzania kwenye shughuli za maendeleo uwe wa uhakika na hiari zaidi.

Makundi yote Haya yanasababu zake na hoja zao zinamashiko Licha ya ukweli kuwa umoja ndiyo msingi wa maendeleo Kwa mtu binafsi na taifa Kwa ujumla.

Katika maadhimisho ya siku ya uhuru yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimabli wa serikali na vyama vya siasa. Na kikubwa kilichojiri ni baada ya mwenyeki wa chadema kueleza kuwa amehudhuria sherehe Hizo kama njia ya kutaka kuwepo Kwa maridhiano ili kuwaleta pamoja watanzania na kushiriki kikamikifu katika ujenzi wa taifa lao.

Pamoja na nia hiyo njema ya kiongozi wa chadema lakini wadau na wanasiasa mbalimabli walitoa maoni juu ya kauli hiyo. Wapo wanaodiriki kusema chadema wamekosea na wapo wanaoona kuwa wapo sahihi na kuna haja ya kuwepo Kwa maridhiano.

Binafsi naona walichofanya vyama vya upinzani ni sahihi Licha ya kuwa inaonekana kama wamesalimu amri na kubariki yaliyotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Lakini katika ujenzi wa taifa lolote tunahitaji viongozi wavumlivu na wenye uwezo wa kuamua mambo yenye manufaa Kwa taifa na ustawi wa watu wake na si kujikweza na kujikusanyia sifa binafsi.

Siku zote Matatizo hayatatuliwi Kwa jaziba Bali hutatuliwa Kwa hekima na kukaa meza moja kuyazungumza na kuyamaliza. Kilichofanywa na chadema na viongozi wengine kina tija na maslahi Kwa taifa katika kuimarisha umoja wa kitaifa.

Mataifa ambayo viongozi wake wameshindwa kujishusha na kutafuta meza ya mazungumzo yamesabaritika na yana haha kurejea katika meza ya mazungumzo ili kutatua kasoro zilizopo. Maridhiano yakiwepo ni ushindi wa watanzania wote na siasa yetu tutaifanya tukiwa wamoja na hivyo kupata viongozi watakaotufikisha katika Tanzania tunayoitaka.

SHIME WATANZANIA TURIDHIANE SASA.
 
Nimeona watu wakisifu wapinzani kuhudhuria sherehe ya Uhuru leo pale CCM Kirumba. Ni vyema tukumbushe Kirumba ilivyojengwa ili kumbukumbu iishi. Uwanja wa Kirumba ulijengwa kwa michango ya wafanyakazi na wafanyabiashara chini ya usimamizi wa CCM. Tulikatwa mishahara mwaka mzima. Hatukuona ubaya kwa kuwa tuliona utafanya tupate kiwanja cha sherehe na michezo. Enzi zile ilikuwepo nyamagana peke yake na ilikuwa ndogo mno kiasi cha kuhatarisha maisha. Siku ya Yanga Vs Simba mechi aliyozomia mchezaji wa SSC Saad ilikuwa nusura mambo yaharibike.
Kwa hiyo leo Mbowe na ujumbe wake wamenufaika na michango yetu. Kina Mapalala na Mtikila wangekuwa na mawazo ya kupinga kama wao leo Mbowe angehudhuria sherehe porini?

Nimeshangaa sana kina Mbowe wanapongezwa! Hakika leo ilipaswa wahojiwe ni kwa nini takriban miaka 10 hawajajumuika na familia katika sherehe hii muhimu? Pia ingefaa waulizwe ile kauli ya kutotoa ushirikiano wameipuuza? Maana itakuwa kituko leo wameenda Kirumba kesho wasusie ujenzi wa shule!

Lakini niitizame hotuba ya Mbowe. Ilikuwa fursa muhimu kama kweli yeye na wenzake walikuwa na nia ya kweli ya maridhiano. Inashangaza ujumbe wake ulivaa magwanda japo yeye alivaa suti. Hivi ndugu akija harusini kavaa kininja atakuwa anahitaji maridhiano? Walijiandaa Kwa kitu gani kilichohitaji magwanda? Najua kuna CCM waliovaa kijani hata wao walipotoka. Hii ni sikukuu ya Uhuru wa mtanzania!

Lakini achilia mbali taswira ya vazi nadhani Mbowe hakutumia fursa vizuri. Nilitegemea kama kweli anahitaji maridhiano katika hotuba yake angeonyesha hilo. Angewaasa wanachama na viongozi wa chama chake wapuuze kauli zake za kutotoa ushirikiano! Huwezi kuagiza wanachama nchi nzima wasitoe ushirikiano na wakae standby kusubiri maelekezo halafu ujidai unaagiza maridhiano yaboreshwe! Badala yake anamwambia mkuu wa nchi ndiye aboreshe mahusiano! Charity begins at home! Mbowe himiza viongozi wako waboreshe mahusiano kabla hujamwambia mkuu wa nchi. Ndani ya msafara wako alikuwepo Lema! Majuzi tu katangaza kazi yake namba moja ni kuingamiza CCM kanda ya Kaskazini! Huyu nani ataboresha mahusiano naye? Anza kwanza kuwanasihi hawa! Toa boriti jicho lako!

Nilidhani leo Mbowe angetumia fursa kutia nia kwamba hawatapinga miradi ya maendeleo! Na awahimize wanachama wake kuunga mkono juhudi za serikali. Nilitegemea leo Mbowe awaase wanachama wake waliofyeka mashamba na kuchoma nyumba waache ili kuboresha mahusiano! Haya Mbowe hakuona ni mambo mabaya yanayodumaza maridhiano?

Hakika leo Mbowe alikuwa mgeni mwovu! Hakuja kwenye sherehe ya familia na roho nyeupe! Walikuwa na lao jambo ila likabuma!

Sitaki kuwa nabii lakini nahisi Mbowe na ujumbe wake walidhani bado Wana wanachama wengi kanda ya ziwa na watajitokeza kwa wingi na sare za chama! Wamekuta kanda ya ziwa iko na JPM wa CCM.
Hii ni salamu tosha kuwa oktoba 2020 kuna kilio!

Mpira uko kwa Mbowe! The ball is in Mbowe's court! Je kuanzia sasa tutakuona ukidumaza au ukiboresha maridhiano?
Umejipa mtihani mwenyewe!
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani
Hapo mtamke Mbowe tuu! Wengine hakuna haja, maana akiwaambia twende lazima wafuate. Anyway katika hilo Mbowe alijiongoza vizuri na angamlau amekijengea taswira nzuri chama chake juu ya mambo ya kitaifa kuliko kususa.
 
Back
Top Bottom