FT| NBC | Namungo 1-1 Simba Sc | Majaliwa Stadium | Mei 3, 2023

FT| NBC | Namungo 1-1 Simba Sc | Majaliwa Stadium | Mei 3, 2023

Mechi ni saa 1 usiku

Kuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha leo na kile cha mwisho kilichocheza kule Morroco

Pamoja na hoja ya kuwapumzisha wachezaji lakini mtu kama Moses Phiri kukosekana hata benchi kunaongeza maswali.

Kibu D naye mechi hii kaikosa.


LIGI KUU: SIMBA YASHIKWA, YAZUIWA KUIKIMBIZA YANGA KWENYE UBINGWA
Simba imeshindwa kuikimbiza Yanga katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara Msimu wa 2022/23 baada ya kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Namungo FC kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Kwa matokeo hayo Simba imebaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 64 katika mechi 27, nyuma ya #Yanga yenye pointi 68 katika mechi 26 wakati NamungoFC ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 36 kwenye mechi 27.

Goli la Simba limefungwa na Jean Baleke dakika ya 27 kisha Hassan Kabunda akasawazisha katika dakika ya 39.

View attachment 2608839
Ujinga uliopo simba huwezi ona yanga ndio maana watakuwa mabingwa daima kocha amepewa uhuru sana haiwezekani wachezaji wengine hawataki tu na kuleta timu hovyo kbs bora wampe timu kibadeni tu
 
Tulia binti chura...sisi na Ihefu ndo wababe wenu 😆😆😆
Upo lakini unitag kwenye story kule tusuuze mioyo...
Natuliaje na watu mnakufa kiume. Sijui nanyinyi warembo mnakufa kiume? 🤣🤣🤣🤣🤣

Luv hata nafatilia hadithi yoyote basi kwasasa? Hakuna, Steve naye sijui kaendelea ama lah. Ila nikikutana na story yoyote nitakutag mtani wangu mzuri.
 
Natuliaje na watu mnakufa kiume. Sijui nanyinyi warembo mnakufa kiume? 🤣🤣🤣🤣🤣

Luv hata nafatilia hadithi yoyote basi kwasasa? Hakuna, Steve naye sijui kaendelea ama lah. Ila nikikutana na story yoyote nitakutag mtani wangu mzuri.
Wewe mtagi hata story ya MAJEDWALI asee 🤔😅🏃🏃
 
Ndio maanake hata akina Club Africaine, Real Bamako, Monistir na Rivers United nao waliwapa bahasha na hata Marumo Gallants nao tayari wameshapokea bahasha.

Dah.. Kwa kweli hivi vitimu vidogovidogo visivyokuwa na majina ukiacha Rivers Utd wengi tumevijua mwaka huu. Vina hadhi ya kucheza Ile Ligi tunayowakilishwa na Utopolo, Namungo, Geita, Azam
 
Baada ya Simba KUFA KIUME huko MOROCCO na mwili wake kusafirishwa Hadi nchini Tanzania, na kamati ya mazishi kukubaliana akazikwe mkoani Lindi kwa ndugu zake. Hatimaye hapo Jana, mazishi yalifanyika na KUZIKWA KIUME.

Kwake yeye kila goti litapigwa

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom