FT: Ngao ya Jamii: Simba SC 0-0 Singida FG Penati (4-2)| Mkwakwani Stadium Tanga | Agosti 10, 2023

FT: Ngao ya Jamii: Simba SC 0-0 Singida FG Penati (4-2)| Mkwakwani Stadium Tanga | Agosti 10, 2023

Ngoja tuone dua la kuku
1691581251282.jpg

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
===

Greatest of all time
Leo ni Sikukuu ya Soka.

Mnyama Mkubwa Mwituni. Simba SC itakuwa ikishuka dimbani kuwakabili Singida FG FC katika dimba la Mkwakwani pale jijini Tanga.

Simba ambayo imesheheni wachezaji mafundi kama vile Onana, Baleke, Kramo, Mwalimu Fabrice Ngoma na wengineo wanatarajiwa kutoa burudani kubwa sana kwa wapenda kandanda nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla mara baada ya butua butua na piga nikupige ya jana.

Singida ambayo imefuzu kucheza kimataifa nayo imesajili wachezaji kadhaa akiwemo Kiyombo, Babu Onyango, Yahaya Mbegu na wengineo wanatarajiwa kuleta ushindani.

Ewe mwana Simba uliyepo Kasulu, Jinja, Makambako, Kisumu, Uyui, Ndola, na mahala popote tegemea mpira mkubwa leo na mechi yenye mvuto.

Mechi itapigwa Saa 1:00 Usiku na itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD
Baada ya vioja vya jana hatimaye leo tunapata nafasi ya kuangalia soccer. Kila lakheri Mnyama wa mwituni.
 
Nitafurahi Simba akishinda ili kidooogo alete ushindan kwenye Fainal ila nitafurah zaidi Singida akishinda alafu Makolo wakapigwe na azam ili Waanze kutukanana na kukosa furaha Mapema in shot napenda tu kuona Mtani anateseka [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Si vibaya kuota, endelea kuota kijana ila ujue usiyempenda kaja.
 
Back
Top Bottom