FT: Ngao ya Jamii: Simba SC 0-0 Singida FG Penati (4-2)| Mkwakwani Stadium Tanga | Agosti 10, 2023

FT: Ngao ya Jamii: Simba SC 0-0 Singida FG Penati (4-2)| Mkwakwani Stadium Tanga | Agosti 10, 2023

===

Greatest of all time
Leo ni Sikukuu ya Soka.

Mnyama Mkubwa Mwituni. Simba SC itakuwa ikishuka dimbani kuwakabili Singida FG FC katika dimba la Mkwakwani pale jijini Tanga.

Simba ambayo imesheheni wachezaji mafundi kama vile Onana, Baleke, Kramo, Mwalimu Fabrice Ngoma na wengineo wanatarajiwa kutoa burudani kubwa sana kwa wapenda kandanda nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla mara baada ya butua butua na piga nikupige ya jana.

Singida ambayo imefuzu kucheza kimataifa nayo imesajili wachezaji kadhaa akiwemo Kiyombo, Babu Onyango, Yahaya Mbegu na wengineo wanatarajiwa kuleta ushindani.

Ewe mwana Simba uliyepo Kasulu, Jinja, Makambako, Kisumu, Uyui, Ndola, na mahala popote tegemea mpira mkubwa leo na mechi yenye mvuto.

Mechi itapigwa Saa 1:00 Usiku na itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD
20230808_200639.jpg
 
Kuna timu ina wakati mgumu sana. Maana ikifanikiwa kufuzu hatua ya fainali, inakutana na kisiki cha mpingo!
Ikishindwa na kupambania mshindi wa tatu, napo itakutana na kisiki kingine cha mpingo!

Naona malengo ya waandaji yameenda tofauti kabisa na matarajio.
 
Kisiki cha mpingo kitakutana na KONDE BOY na kitachongwa na kugeuzwa kinyago cha mpapure.
😝😝😝😝
 
Back
Top Bottom