FT: Ngao ya Jamii: Simba SC 0-0 Singida FG Penati (4-2)| Mkwakwani Stadium Tanga | Agosti 10, 2023

FT: Ngao ya Jamii: Simba SC 0-0 Singida FG Penati (4-2)| Mkwakwani Stadium Tanga | Agosti 10, 2023

Simba inacheza utafikiria ninile ya mwaka 1936 wakati inaanzishwa, tofauti ni ndogo hivi. Kumbe zile kelele za Mwamed zinatokanaga na depression za Simba hii
We unadhani mchezo nini? Utoe kitita kusajili wachezaji halafu uone huu utumbo uwanjani utaacha kuwa na stress? Maana yake ni kwamba msimu ujao pia atoboke pesa nyingi kusajili kundi jingine kubwa la wachezaji ambao matokeo yake ni unforseen.


Ununue simu ya 3.6M kisha umefika nyumbani kuiweka charge kabla ya kuitumia halafu iungue, utaacha kuwa na stress hata kama hela ipo?

Mwamedi lazima achanganyikiwe tu[emoji23].
 

===

Greatest of all time
Leo ni Sikukuu ya Soka.

Mnyama Mkubwa Mwituni. Simba SC itakuwa ikishuka dimbani kuwakabili Singida FG FC katika dimba la Mkwakwani pale jijini Tanga.

Simba ambayo imesheheni wachezaji mafundi kama vile Onana, Baleke, Kramo, Mwalimu Fabrice Ngoma na wengineo wanatarajiwa kutoa burudani kubwa sana kwa wapenda kandanda nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla mara baada ya butua butua na piga nikupige ya jana.

Singida ambayo imefuzu kucheza kimataifa nayo imesajili wachezaji kadhaa akiwemo Kiyombo, Babu Onyango, Yahaya Mbegu na wengineo wanatarajiwa kuleta ushindani.

Ewe mwana Simba uliyepo Kasulu, Jinja, Makambako, Kisumu, Uyui, Ndola, na mahala popote tegemea mpira mkubwa leo na mechi yenye mvuto.

Mechi itapigwa Saa 1:00 Usiku na itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD.

---
Kikosi cha Simba kinachoanza

Kikosi cha Singida FG kilichoanza


---

Mpira umeanza
04' Bado milango ni migumu bado hawajafungana

05' Singida wanapata goli lakini linakataliwa

40' Bado milango migumu kwa timu zote mbli huku zikishambuliana kwa zamu

45' Mapumziko timu bado hazijafungana

46' Anaingia Ngoma na Bocco wanatoka Kanoute na Baleke

55' Milango bado migumu kwa timu zote mbili
Mpira wa jana ulikuwa si butua butua ulikuaa ni mchezo wa kuwaonesha kuwa watu wamejipanga kimkakati zaid
 
Leo Simba tukitoboa wakatambike. Timu haieleweki
 
Back
Top Bottom