FT: Simba 0-3 Raja Casablanca | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.02.2023
Niliwaambia mashabiki wenzangu wa Simba sioni sababu ya kuletwa huyu kocha mpya katikati ya msimu wakati Mgunda anafanya vizuri na alishapata combination nzuri ya Boko Chama na Ntibanzonkiza. Walinishukia kama mwewe. Leo hii toka huyu kocha aje Simba imekuwa ikishinda kwa tabu huku ikicheza mpira mbovu na Boko hafungi tena.
Mgunda asingetufikisha popote pale.

Simba haina wachezaji
 
Sasa kama nyumbani tu unakubali kufungwa 3 bila! Ukienda kwao si unaenda kupigwa 🤚

Ndiyo hii timu ilikuwa inawakejeli Vipers, ambao wametoa sare na mbabe mwingine Horoya!!

Kwa hali hii sitashangaa wakishika mkia kwenye kundi lao.
Washike mkia mara ya pili? Kwa uchezaji huu simba atafungwa na timu zote kwenye group.

Yaani mwaka huu Mo atautema urais wa heshima simba.
 
Halafu wana mechi ya nyumbani dhidi ya Azam!! Aisee huu mwaka ni wa tabu. Cha kushangaza lawama zote atatupiwa Mbrazil wa watu! Sijui ni kwa nini alikubali kuja kufundisha timu kama simba!
Kwani majuaji mawili ya humu leo yako wapi popoma genta na yule babu okwi
Kucha kutwa kumnaga babra sasa hayupo mtamnanga nani?
 
Halafu wana mechi ya nyumbani dhidi ya Azam!! Aisee huu mwaka ni wa tabu. Cha kushangaza lawama zote atatupiwa Mbrazil wa watu! Sijui ni kwa nini alikubali kuja kufundisha timu kama simba!
Eti nae mjinga limeacha timu lake la vipers amekuja kukimbizana na wahuni


Atapigwa nje ndani

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ilikuwa ni suala la muda tu.

Simba imejitahidi kadiri ya uwezo wa wachezaji wake.

Ukilinganisha Raja ni wepesi na wakishambulia hawatoi pasi chonganishi kama Simba.

Hata hivyo, kwa kufanya maboresho ya madhaifu bado Simba ina nafasi ya kupata nafasi ya pili iwapo itashinda mechi 3 na sare 1.
 
News Alert kutoka Breaking News
Screenshot_20230218-212752_1.jpg
 
Back
Top Bottom