FT Yanga 1-0 Simba Ngao ya Jamii Jumanne Septemba 16,2025 | Benjamin Mkapa Stadium | Saa 11:00 Jioni

FT Yanga 1-0 Simba Ngao ya Jamii Jumanne Septemba 16,2025 | Benjamin Mkapa Stadium | Saa 11:00 Jioni

I see, hi
Hakika hii haina afya kwa Simba. Kwa nini wasichukuliwe hatua hawa vijana?
Simba ilikuwa haishindi huu mchezo kwa njia yoyote ile.

Hiyo video ilikuwa kutengeneza mazingira tu ili hali ikiwa mbaya wawaangushie hao jumba bovu.

Juzi nilisema Simba itapigwa shoti, kuna watu wakajifanya hawanielewi.
 
Yanga mnacheza Mpira wa hovyo sana msipo fanya reshuffle ya kikosi chenu this season mtaumbuka

Second mmefanya makosa sana kumuachia AUCHO

Poor performance sijapenda
Kama kweli unafahamu soka hii kauli yako sio sahihi. Ni kweli Yanga leo hawakua bora lakini ni utovu wa nidhamu mkubwa sana kusema wafanye reshuffle. Yanga ndo timu iliyokamilika zaidi katika timu zote za ligi kuu msimu huu. Na hii ni kwasababu bado wachezaji wake ambao wamekaa pamoja muda mrefu wana ubora ule ule na walioondoka ni wachache sana. Yani unasema timu ifanye reshuffle kwasababu tu ya kuondoka Aucho? Matokeo ya mpira yanaamuliwa na moments tu. Ile mechi Simba anashinda 2-0 Yanga ilikua bora sana lakini moments tu ziliamua ile mechi kwasababu Simba walipress sana kuanzia dakika ya kwanza wakapata kona Inonga akafunga, muda mfupi baadae walifanya tena counter pressing Kibu akafunga. Ile ni Yanga ya Mayele, Bangala na Aucho ujue. Lakini guess what?! Yanga alichukua ndoo zote msimu ule na aifika fainali CAF Confederation Cup. Msimu uliopita mechi mbili za mwanzo za Simba na Yanga, yani ngao ya jamii na ile ya ligi Simba alikua bora sana mechi zote mbili ila ziliamuliwa na moments na Yanga kushinda. Yanga alibadili makocha mara 3 lakini bado alichukua ubingwa na alimfunga Simba tena (total dominance). Huyu kocha wa Yanga ni mgeni lakini bado Fadlu kashindwa kumfunga. Then wewe unakuja kusema Yanga ifanye reshuffle kwasababu tu Aucho hayupo? Point nyingine ya msingi Simba amefungwa sana na Yanga siku zote hua wanakua aggressive sana wanapokutana na Yanga. Nikisema leo walikamia sana mechi kwasababu waliahidiwa pesa nyingi na viongozi endapo wataifunga Yanga nitakua nimekosea? Finally, mechi ya Simba na Yanga ni derby sio mechi rahisi kiasi hicho so timu iliyokua inataka sana matokeo ni Simba na pamoja na kua bora leo na kutengeneza nafasi nyingi sana kama ile derby waliyofunga 2-0 leo walikua na umaliziaji mbovu na Yanga kashinda mechi kwa kikubwa kwa kutumia kosa moja na kwaadhibu. By the way Ecua haukua smart tu mwishoni amepata nafasi mbili zote kazingua vinginevyo sasa hivi stori ingekua ni 3-0. Last season ilikua hivi hivi, Simba anakamia derby kuwaaminisha kua timu iko vizuri baadae inakuja kuzingua mwishoni tunaanza upya, wenzenu ndoo ya kwanza kabatini tayari we endelea tu kusema timu imecheza vizuri huku inakandwa mara 6 mfululizo. Kwa msimu huu tena naona kabsa Yanga bingwa wa vikombe vyote vya ndani, tunzeni hii comment yangu.
 
Kukunjwa hivi si mchezo🤣🤣🤣🤣
IMG-20250916-WA0000.jpg

 
kiuhalisia hii mechi ilipangwa yanga washinde bila usbishi goli la offside ya wazi refa anapeta
 
Back
Top Bottom