Full Time: Tanzania 0- 2 DR Congo | Qualification AFCON 2025 | Benjamin Mkapa Stadium | 15 Oktoba, 2024

Full Time: Tanzania 0- 2 DR Congo | Qualification AFCON 2025 | Benjamin Mkapa Stadium | 15 Oktoba, 2024

kincho niuma sio kufungwa 2 ila matumiz mabaya ya pesa na ndege ya WaTz iliyobeba hizi ng'ombe hadi congo na kurudi tz kisha zikakubali kukamuliwa nje ndani...
tuache usengerema tuache siasa tz hatuna team hatuna coach, tujenge team miujiza na hamasa haiwezekan kwenye team ambayo ni kichwa cha mwendazimu...
 
Leo Jumanne, Taifa Stars itakuwa dimba la Benjamin Mkapa kwa kazi moja tu kusaka ushindi dhidi ya DR Congo katika mechi ya kuwania kufuzu AFCON 2025 nchini Morocco.

Mechi hii itachezwa saa 10:00 jioni


Mpira umeanza kipindi cha kwanza na DR Congo ndiyo wameanzisha gozi.

Dakika, 2 Stars wanapata kona.

Dakika, 4 Stars wanafanya shambulizi zuri sana na kupata kona.

Dakika 6 Taifa Stars wamefanya shambulizi zuri kutoka kwa Mzize.

Dakika,12 Sammata anakosa goli hapa.

Dakika, 18 DRC wamefanya shambulizi zuri.

Dakika, 38 Mpira umekuwa kasi sana

Dakika, 39 Kibu anakosa nafasi ya wazi

Dakika, 42 Ali Salmu anafanya save nzuri na kuwaweka salama Taifa Stars.

Zimeongezwa Dakika 3 kukamilisha dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika Tanzania 0 - 0 DR Congo.

Kipindi cha pili kimeanza

Dakika,52 Taifa Stars wamefanya majaribo mawili lakini wameshindwa kutumia nafasi vyema.

Dakika, 73 DR Congo na Taifa Stars wamefanya Mabadiliko ya wachezaji

Ametoka Mudathri anaingia Mao. Kwa upande wa DRC anaingia Mayele.

Dakika 84 Mzize anatoka nafasi yake inachukuliwa na Mwalimu Hassan.

Dakika, 86 DRC wanapata goli

Dakika,93 DRC Meshakc Anawapatia goli la pili
Samata Hana msaada
 
Wote tunalalamika ila wewe huna hoja kabisa, nisamehe kukuita mbumbumbu wa football
Utopolo utamjua tu!! Huwezi kufanikiwa kuondoa mawazo ya wachezaji wa hizo timu mbili kwenye mchuano kati yao zikiwa zimebaki siku chache hivyo! Hawawezi ku-concetrate kumsikiliza kocha hata kidogo! Walitakiwa kuusogeza mbele kidogo mchezo huo!!
 
Nasikitika tumefungwa japo magoli waliyotufunga ni mazuri sana!! Yule mfungaji wao wa magoli yote itabidi Yanga au Simba wamsajili!!
 
Hemed Morroco amewekwa hapo baada ya zile kero 23 za muungano kutatuliwa na Samia sio kwambao Yuko Taifa stars kwasababu ya uwezo hapana Bali Yuko pale kukamiliaha sheria na taratibu za muungano.
Ujinga mtupu
 
Sijatazama mechi ila kila kona mama hivi mama vile.

Hivi huyo mama anacheza nafasi gani kwenye hii timu?

Au ndio 4R tunazoambiwa?
IMG_20241015_202839.jpg
h
 
Kocha Hana uwezo wa mbinu , pale alipomtoa muda na mzize aliua presha ya stars kupeleka Mpira mbele
 
Back
Top Bottom