Furaha Dominic: Askofu Gwajima ndiye kiongozi wa kundi linalomkwamisha Rais Samia

Hivi rais anakwamishwaje? Watu waache ujinga!

Kumkwamisha rais ni kutenda jinsi, haya mengine ni maneno ya kujikomba na kukwepa uwajibikaji tu.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kama sukuma gang ni kundi tiifu kwa mwendazake na linaendelea kumpambania hata sasa iweje mpwa wa mwendazake kujitokeza na kumwita Gwajiboy ndie kiongozi wa kundi tajwa?
Je, huyu mpwa ameshaunga juhudi tayari au ndio anasaka uteuzi?
 
Furaha Dominic, ambaye alishinda kura za maoni kuwania ubunge katika jimbo la Kawe lakini akaporwa ushindi, amesema Askofu Gwajima ni kiumbe wa ajabu sana…..ni muongo, tapeli wa kisiasa na hafai katika jamii.

View attachment 2078536
Askofu Gwajima akiwa kanisani kwake, Uzima na Ufufuo, Dar es Salaam

Akiendelea mbele zaidi kwenye mahojiano, mwanasiasa huyo machachari alimtaja Gwajima kuwa ndiye kinara (kiongozi) wa kundi la Sukuma Gang linalopambana kila kukicha kurudisha nyuma juhudi za Rais Samia kuwaletea maendeleo watanzania. Hivyo, amemtahadharisha Rais Samia kuwa makini na kauli mbalimbali ambazo Gwajima amekuwa akizitoa hadharani kupinga juhudi zake za maendeleo ya watanzania, hasa suala la chanjo ya UVIKO-19. Dominic amesema hayo jijini Mwanza wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Star TV. Unaweza kumsikiliza mwenyewe akifunguka hapo chini kama ifuatavyo:

MAONI YANGU
Baada ya Rais Samia kufanikiwa kuwaondoa ‘wahuni’ kwenye nafasi za uwaziri, wakati sasa umefika ateremshe panga lake chini afyekelee mbali wahuni akina Gwajima na genge lake ili kuhakikisha anawaondoa chawa wote kwenye mfumo wa serikali na chama. Hii itamsaidia sana kufikia malengo ya kuwatumikia watanzania na hata kupata kura za kishindo kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.

Nawasilisha.​
Gwajima hawezi kuondolewa na rais sio mteule wa rais
 
Gwaji boy atamuwashia moto. Naona anatafuta kuchambwa madhabahuni
 
Huyo ni mtoto wa dada wa Magufuli, sio mtoto wa Magufuli, naona story zake zimekuwa nyingi sana sijui anatumiwa au anajitumia ili akumbukwe kwenye ulaji wa awamu ya sita.

Kwa haya majibu yake asijekuwa analazimisha kuaminiwa, nitamshangaa sana, vyema aache kila jambo lipite siasa sio kila kitu maishani.
Uje kwetu nikupikie pilau la kondoo kaka. You've nailed it
 
Gwajima hawezi kuondolewa na rais sio mteule wa rais
Atamuwekea kigingi kwenye kura za maoni ndani ya chama ili jina lake lisirudi na endapo ataendelea kumuandama mama, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa chama, anaweza kumvua uanachama, hivyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kama sukuma gang ni kundi tiifu kwa mwendazake na linaendelea kumpambania hata sasa iweje mpwa wa mwendazake kujitokeza na kumwita Gwajiboy ndie kiongozi wa kundi tajwa?
Je, huyu mpwa ameshaunga juhudi tayari au ndio anasaka uteuzi?
Inaonekana yeye hayumo au yumo kundini kiintelejensia zaidi akisaka habari na kumpenyezea mama.....huenda kwa ahadi ya uteuzi. You never know.
 
Kwenye interview ya Furaha, amemchanachana Askofu Gwajima kwa kusema kuwa ni MNAFIKI na MUONGO. Kazungumzia vipi alivyowatapeli wananchi wa Kawe kwa kudai kuwa ndani ya siku 100 atawajengea wana Kawe Barabara na kuwapeleka Birmingham.

Kwa kweli Gwajima amekuwa Muongo kwa siku nyingi sana, amedanganya kufufua watu. Amedanganya kuleta train za umeme n.k. n.k.

Ila kwa jinsi tunavyomjua Gwajima, huyu dogo ajiandae kwa majibu yake Jumapili.

NB. Kuna mambo ambayo Dogo amezungumzia kuhusu Kupe ambayo siyo rahisi kuyazungumza mbele ya wanafamilia. Pia sidhani kama Dogo alikuwa anaishi Magogoni.
Fungu la kukosa huyo
 
Ha ha ha ha swahiba Furaha Dominick AFUNGUKAAAA......🤣🤣

#Siempre JMT🙏
#Gwajima Ni Mnafiki
 
Hivi kwa nini gwajima habebi biblia na badala yake anatumia Ipad
 
Kwenye interview ya Furaha, amemchanachana Askofu Gwajima kwa kusema kuwa ni MNAFIKI na MUONGO. Kazungumzia vipi alivyowatapeli wananchi wa Kawe kwa kudai kuwa ndani ya siku 100 atawajengea wana Kawe Barabara na kuwapeleka Birmingham.

Kwa kweli Gwajima amekuwa Muongo kwa siku nyingi sana, amedanganya kufufua watu. Amedanganya kuleta train za umeme n.k. n.k.

Ila kwa jinsi tunavyomjua Gwajima, huyu dogo ajiandae kwa majibu yake Jumapili.

NB. Kuna mambo ambayo Dogo amezungumzia kuhusu Kupe ambayo siyo rahisi kuyazungumza mbele ya wanafamilia. Pia sidhani kama Dogo alikuwa anaishi Magogoni.
Hivi kweli mtu na akulizako umuamini Gwajima?

Alisema na kutuaminisha kuwa yeye anafufua watu lkn siku amekufa ndugu yake hatukumuona anamfufua.
 
Back
Top Bottom