Furaha Dominic, ambaye alishinda kura za maoni kuwania ubunge katika jimbo la Kawe lakini akaporwa ushindi, amesema Askofu Gwajima ni kiumbe wa ajabu sana…..ni muongo, tapeli wa kisiasa na hafai katika jamii.
View attachment 2078536
Askofu Gwajima akiwa kanisani kwake, Uzima na Ufufuo, Dar es Salaam
Akiendelea mbele zaidi kwenye mahojiano, mwanasiasa huyo machachari alimtaja Gwajima kuwa ndiye kinara (kiongozi) wa kundi la Sukuma Gang linalopambana kila kukicha kurudisha nyuma juhudi za Rais Samia kuwaletea maendeleo watanzania. Hivyo, amemtahadharisha Rais Samia kuwa makini na kauli mbalimbali ambazo Gwajima amekuwa akizitoa hadharani kupinga juhudi zake za maendeleo ya watanzania, hasa suala la chanjo ya UVIKO-19. Dominic amesema hayo jijini Mwanza wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Star TV. Unaweza kumsikiliza mwenyewe akifunguka hapo chini kama ifuatavyo:
MAONI YANGU
Baada ya Rais Samia kufanikiwa kuwaondoa ‘wahuni’ kwenye nafasi za uwaziri, wakati sasa umefika ateremshe panga lake chini afyekelee mbali wahuni akina Gwajima na genge lake ili kuhakikisha anawaondoa chawa wote kwenye mfumo wa serikali na chama. Hii itamsaidia sana kufikia malengo ya kuwatumikia watanzania na hata kupata kura za kishindo kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.
Nawasilisha.