Furaha Dominic: Askofu Gwajima ndiye kiongozi wa kundi linalomkwamisha Rais Samia

Furaha Dominic: Askofu Gwajima ndiye kiongozi wa kundi linalomkwamisha Rais Samia

Gwajima kumshinda inahitaji akili kubwa sana na hoja za msingi....

Asubiri tu kulipuliwa
 
Hv kupe ni wakina nani? Maana kawasema sana kuwa walikuwa wanamuingiza kingi mjomba wake kwa taarifa za uongo na mjomba wake akawa anawaumiza watu bila hatiya yoyote!
Huyu Dogo anatoa chumvi. Haiwezekani info nyeti kama hizo zitolewe mbele yake. Unless ni ndogo ndogo alizozipata kupitia familia. Sidhani kuwa kwa kazi yake alikuwa anaishi Magogoni pia... Something is not right.....!!
 
Dogo inaonekana anahasira sana na hao kupe! Je hao kupe ni wakinanani? Waliokuwa wanamlisha matongo pori jiwe na jiwe kuumiza watu kama yeye alivyo kuwa anasema.
 
Furaha Dominic, ambaye alishinda kura za maoni kuwania ubunge katika jimbo la Kawe lakini akaporwa ushindi, amesema Askofu Gwajima ni kiumbe wa ajabu sana…..ni muongo, tapeli wa kisiasa na hafai katika jamii.

1642005697089.png

Askofu Gwajima akiwa kanisani kwake, Uzima na Ufufuo, Dar es Salaam

Akiendelea mbele zaidi kwenye mahojiano, mwanasiasa huyo machachari alimtaja Gwajima kuwa ndiye kinara (kiongozi) wa kundi la Sukuma Gang linalopambana kila kukicha kurudisha nyuma juhudi za Rais Samia kuwaletea maendeleo watanzania. Hivyo, amemtahadharisha Rais Samia kuwa makini na kauli mbalimbali ambazo Gwajima amekuwa akizitoa hadharani kupinga juhudi zake za maendeleo ya watanzania, hasa suala la chanjo ya UVIKO-19. Dominic amesema hayo jijini Mwanza wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Star TV. Unaweza kumsikiliza mwenyewe akifunguka hapo chini kama ifuatavyo:

MAONI YANGU
Baada ya Rais Samia kufanikiwa kuwaondoa ‘wahuni’ kwenye nafasi za uwaziri, wakati sasa umefika ateremshe panga lake chini afyekelee mbali wahuni akina Gwajima na genge lake ili kuhakikisha anawaondoa chawa wote kwenye mfumo wa serikali na chama. Hii itamsaidia sana kufikia malengo ya kuwatumikia watanzania na hata kupata kura za kishindo kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.

Nawasilisha.​
 
Huyo ni mtoto wa dada wa Magufuli, sio mtoto wa Magufuli, naona story zake zimekuwa nyingi sana sijui anatumiwa au anajitumia ili akumbukwe kwenye ulaji wa awamu ya sita.

Kwa haya majibu yake asijekuwa analazimisha kuaminiwa, nitamshangaa sana, vyema aache kila jambo lipite siasa sio kila kitu maishani.
 
Huyo ni mtoto wa dada wa Magufuli, sio mtoto wa Magufuli, naona story zake zimekuwa nyingi sana sijui anatumiwa au anajitumia ili akumbukwe kwenye ulaji wa awamu ya sita.
Mtoto wa dada naye ni mtoto wako mkuu, hakuna tatizo
 
Back
Top Bottom