Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Acha wayapindue tu kwa sababu hayana akili. Kwenye sanduku la kura yanatuibia na kutupakaza mawino ya bure kwenye vidole. Dawa yao ni hiyo tu.
 
It goes down well. We are tired of having leaders who propagates the gospel of democracy, while thriving in corruption. Africa is changing. One of the days, they will pay for their crimes.
Na wanapoguswa wanaleta taharuki za udini, ukabila, ukanda na mengine mengi!
Mwenye Mungu atawalipa kadri ya mwendo wenu. Hamtawarisisha watoto wenu mali ambazo sio za kwenu.
 
nchi kama Zimbabwe, pamoja na madudu yaliyofichuliwa na Documentary ya gold mafia majuzi tu, still mtu kama Mnangagwa bado anashinda uraisi, how comes🚮🚮🚮🚮
 
Naunga mkono hili. Mwaka 2020 Tz yalitokea mambo mabaya sana wakati wa uchaguzi
 
Taratibu tutafikiwa tu
 
Afu Cha kushangaza,
Wanaoongoza mapinduzi Ni wanajeshi wa vyeo vya chini[emoji4]
Hii sayansi hii, nadhani ufaransa ndio wanaijua zaidi; makoloni ya muingereza na ujerumani yote yako chali 😀
 
Tume ya uchaguzi ilikuwa tayari imeshamtangaza Ally Bongo kuwa mshindi. Watu wamechoka na demokrasia za mchongo
Watawala wa Afrika wana akili kama za mnyama ngiri anayeweza kusahau mambo muda huo huo yatokeapo!

Kwa misemo ya kiswahili twaweza sema: " wana masikio ya kufa yasiyosikia dawa"!

Ukichunguza akili za ngiri ni kama alishushwa mahususi ili awe chakula cha simba kutokana na upeo wa akili zake.

Kwa sababu ngiri akikikwepa kifo kwa juhudi zake za kumzidi simba kwa mbio, kabla hata hajajihakikishia usalama wake ama kukaa kutafakari tukio lililotaka kugharimu maisha yake, muda huo huo husahau yaliyopita na kuanza kusakura minyoo kwenye udongo(kula)!

Watawala wa Afrika 99% akili zao wote zinafanana na sisi Tz tukiwemo, kuiba kura, kuchezea mifumo ya kuhesabia kura, kuunda tume za uchaguzi za bandia, kuweka wasimamizi wa kura mamluki nk nk!

Na wakishaghushi ushindi, hubweteka na kuanza kula mema ya Taifa na kuwasahau wananchi na umasikini wao!

Angalia kwa mfano hivi sasa, nchi hii ipo kwenye taharuki ya kisiasa, mfumuko wa wazi na wa kutisha wa bei na kupanda kwa gharama za maisha kulikosababishwa na mifumo ya kifisadi, leo Rais yupo kwao akitumbua pesa za walipa kodi na kusherehesha wateule wake kwa gharama za walipa kodi!

Pamoja na kelele zote kupigwa juu ya Baraza bovu la mawaziri kwa tuhuma zao mbali mbali ovu, leo Rais kaexchange portifolio zao bila ya kuwaondoa magarasa!

Ndiyo nikasema kwamba, mapinduzi ya kijeshi ya Gabon pamoja na mataifa mengine ya west Afrika yalikotokea mapinduzi mfululizo ya kijeshi, hayawezi kuwa ni"shamba darasa" kwa viongozi wetu kuweza kushituka na kuanza kufuata mifumo ya utawala bora, maana ni sikio la kufa".

Ndiyo kwanza wanavuta shuka na kushindilia pamba masikioni kana kwamba vurugu zote hizo za kidemokrasia zinazofanyika barani Afrika hivi sasa, kwao ni msamiati mpya na haziwahusu!
 
Magazeti ya dunia yanaripoti kuwa Ufaransa, mshiriki mkubwa wa utawala wa Bongo na babaake, imepinga na kulaani Gabon kupinduliwa.

Hapa ndio mjue Mzungu sio ndugu yenu, sio mwokozi wetu, sio malaika wetu, msibabaishwe na misaada.

Mtu ametawala na baba yake miaka 56, wenye nchi wanasema kawaibia, kawaua, hafai, Mzungu anasema analaani familia hiyo kuondoka madarakani!

Ufaransa, watu ambao wako tayari kufa kutetea haki zao za kiraia, kukashifu dini wanasema ni uhuru wa maoni na wako tayari kufa kumchora katuni Mtume, leo inamtetea dikteta mkandamizaji! Kwa vile ni Mwafrika, anawapasua kende Waafrika wenzie, Ufaransa wanapata chao basi wanaona shauri yao heathen Africans watajiju!
 
Tuombe yasifike Afrika Mashariki
Kwa mujibu wa Katiba ya Afrika Mashariki-Somalia, moja kazi ya wajeda ni kumlinda Katiba, yaani maana yake ni kwamba kulazimisha Katiba ifuatwe Sasa sijajua kama wajeda wasiposikilizwa kanuni zao zinasemaje!
 
🤔🤔🤔🤔
Makes sense
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…