Gari Brevis tamu sana kwa safari ndefu!

Una prado gani? Prado zipo zinazokimbia na brevis ya 2Jz pekee ndio yenye cc3000 ntingin ni 2.5
 
Iko vizuri pia
 
Hana akili huyu,anadhani mbio ndio kujua kuendesha gari!
Wanaume tuna tabia ya kutaka kusifiwa usafiri tunaotumia.

Mwenye ist atataka asifiwe gari haili mafuta, mwenye brevis/Cresta atataka asifiwe mbio n.k Ni kawaida kwetu wanaume kutaka kusifiwa gari zetu.

Ni tatizo la saikolojia tulilo nalo wanaume kama ambavyo wanawake wanavyotaka kusifiwa mawigi sijui nywele.

Tatizo huwa kubwa zaidi pale mtu anapolazimika kumiliki gari inayopatikana badala ya gari anayoitaka.

Hapa sasa ndo utakuta mtu mpo carwash anasifia gari lake kuukuu kuwa lina mbio wakati hata kuwaka limegoma baada ya kuingia maji.
 
Ok boss. Nimekuelewa. Huenda ni namna ulivyowasilisha hoja ndo wadau wakaelewa vinginevyo.
 
Sijui ndiyo ujana maji ya moto, ila ni hatari sana🙄
Watu wamepoteza viungo, wengine wamekufa na kuacha watoto wanateseka,Kisa mbio barabarani.Kuna kampuni Moja hapa nchini, nikiwa salesman hapo speed kubwa mwisho 80,na walifunga car track system na kila anayeendesha gari, alikuwa na funguo yake ya gari kumsoma Yeye anayeendesha.Gari zenyewe ni brand new kutoka kiwandani!Zingine zinasoma hadi kms240,ole wako mara 3ikusome umeover speed!Maelezo yake uwe nayo ya kutosha.Kwa mfumo huo ajali hazikuwepo kabisa kwenye kampuni hiyo hadi nimeondoka 2013,Narudia mbio kama Ngiri sio udereva Bali ni kukuita Kifo Cha mapema na Uzembe.Mwenye masikio na Asikie maneno haya.Tahadhali Muhimu.
 
Kupoteza viungo sio mbio kama umepangiwa utagongwa hata kama unatembea
 
Mbio mkuu barabarani sio sifa NJEMA,yakikukuta ya ajali mbaya ndio tutajua!Bora ufe peke Yako kuliko upone utangulize wenzako,kichwa hakitokaa sawa Maishani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…