Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato

Mkuu wa wilaya ya Geita Fadhili Juma amaesema amepeleka mapendekezo Serikalini ya kukataa mpango huo wa kuchukua maeneo ya wilaya hiyo kwenda Chato kwakuwa yatasababisha athari kwa wananchi.

Safi sana madiwani kuongea kama watu-huru . Pia sijaona mmevaa yale majoho ya ki-diwani na kofia zake ambazo kwa kweli ziliongeza mzigo wa gharama kwa wananchi wa Geita.

Kwa mapendekezo haya 'mkoa' wa Chato umekosa sifa na vigezo, hivyo usiundwe.
Tujikumbushe tarehe 26 Machi 2021 Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisisitiza vigezo
Majibu ya Rais Samia kwa mzee wa Chato aliyelilia mkoa wa Chato uundwe
 
hakuna logic mkoa mdogo kama geita kumegwa na kuunda mkoa mpya wa Chato ni bora wangeigawanya Tabora au Morogoro kwanza maana angalau ina ukubwa fulani unadunisha huduma kwa jamii.
 
Kuna mambo ata Magufuli angekuwa hai iwapo asingekamilisha ndani ya muda wake; raisi ajae angeyafuta.

Bado hospitali ya kanda, kuwekeza kitega uchumi kama hiko Chato ni kwenda kuwapelekea stress wataalamu utakaowalazimisha kwenda kuishi huko.
 
Kuunda mkoa mpya wa Chato ilikuwa hatua ya kumfurahisha mwendazake na siyo kusogeza huduma kwa wananchi. Haina uhalali kisiasa wala kiuchumi.
 
JPM mwenyewe alisema kwa hatakubali kuanzishwa kwa mikoa mipya kwenye kipindi chake, ameenda zake sasa wanatafuta namna ya kumuenzi ambayo hakuitaka.

Vv
 
Ningeehangaa sana endapo wangekubali kwa sasa ambapo Jiwe ni kiongozi wa Malaika huko upande wa pili.

Mama Samia aliposema wataangalia kama vigezo vitakidhi, hilo lilikuwa ni jibu la kukataa kiaina.
Wewe unaongea kinyume, mama alisema wale wanaosimamia hilo zoezi la kuifanya chato mkoa waharakishe kumpelekea vigezo na kama havijakamilika basi waseme ili vitafutwe vigezo na kuifanya kuwa mkoa! Kwa maana nyingine mama ashabariki Chato lazima iwe mkoa!
 
Kama aliowatuma ndio wametoa majibu haya, hapo basi hawezi kushurutisha lifanyike
 
Hawa hawa wengi wao walisaidiwa kupita udiwani wao bila kupingwa ndiyo hao hao wanamkaanga....kama leo mwendazake angeibuka wangesema wamenukuliwa vibaya!! Walimaanisha isiwe mkoa bali liwe jiji.
Ha ha ha!
 
He was "kilaza" .
 
Ndio maana tunahitaji inclusive leadership - uongozi shirikisha sio utawala. Sasa mtawala kaondoka, hata hao wa Geita hawataki kujiunga na huo mkoa wa Mwendazake.
 
Kwa nini makao makuu yasiwe biharamulo na mkoa usiitwe biharamulo wachukue sehemu ya muleba, biharamulo,ngara,kakonko,bukombe na chato yenyew?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…