PostGE2025 Gen Z hawapoi: Desemba 9, 2025 kuja na maandamano mapya

PostGE2025 Gen Z hawapoi: Desemba 9, 2025 kuja na maandamano mapya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mnachotaka kukifanya kitapelekea maisha ya wananchi wa kawaida hasa wanawake na watoto kudhurika. Mnakuwa hamna tofauti yoyote na hao oppressors wadaiwa. At that point, nani atamuhukumu nani?

Tafuteni njia mbadala.
 
vipo jeshi pia litakua upande wenu na siku hiyo? kama mulivyodai mwanzo
 
Sema wanafunzi wamewapita hadi walimu wao waliowafundisha kuandamana
 
Wewe ni mnafki unang’ata na kupuliza. Uzungumze na nani?? Au kwakua familia yako haijaguswa??? Yeyote atakaekubali mazungumzo na wauaji atengwe, watu tumeponea chupu chupu risasi unazisikia hadi barazani kwako, tangia tar 29 bila kunywa dawa ya usingizi au kamnywesho siwez kulala naota risasi na mabomu tu. Halafu unazungumzia mazungumzo 🖕
Sio wewe tu, mimi bila safari mbili usingizi hauji. Hapo awali sikuwa natumia kileo kabisa.
 
Nyinyi wahamasishaji wa maandamano mna mizigo yenu katika hili. NYINYI, tukiwaambia mtulie hamtaki, mmesababisha fitna ambayo iliwaenea waliohusika na wasiohusika. Mmesababisha ugumu kwetu sote. Na mimi sijaua mtu yoyote, sio kila ambaye anapinga uharibifu wenu basi lazima atakuwa Polisi au CCM. Wengine tunapinga haya maandamano na uasi dhidi ya watawala kwa sababu Dini yetu (Uislam) imetukataza hilo ili kuchunga damu za watu na kuchunga heshima za watu na mali zao. Tunachunga maslahi mapana zaidi. Nyinyi mnaohamasisha na mnaofanya haya maandamano na uasi dhidi ya watawala hamtengenezi, bali mnaharibu zaidi.
Mtawala kashasema yupo tayari kupimana mabavu, Haya Vijana nao wako tayari. Hampo asiye na busara ni nani? Mtu mzima kaishi miaka 60 kabikiza 10 afe, afu kijana ana miaka 20 kabakiza 50 nani anataka kuharibu nchi yake? Wazee mnawaharibia vijana acheni wadai nchi yao mlioshindwa kuwalisisha. Kama wewe ni mtu wa Dini, Zipo Nyakati Mungu aliruhusu watu wauane kwa Vita ili suluhu ipatikane. Kama Vita italiponya taifa hili basi na Ije, Kuliko Amani bandia
 
Maandamano sio njia ya kudai haki. Amani kwanza. Msiminyane na watawala, mnajikomoa na kututia kwenye shida sote. Amani ikitoweka hata hiyo haki unayoidai huipati.
Kuna Amani gani hapa? Kuna Amani watu wakipingana na wewe unawateka, unawalawiti au wewe hiyo ndo Amani?
Amani ni kuwapa watu kesi za uongo kisa hawafanani mawazo na wewe, Amani ni kuuza Rasilimali muhimu za Vizazi vijavyo kwa bei ya Hasara? Hiyo ndo Amani? Nijibu kama hiyo ndo tafsiri yako ya Amani
 
Noooo, not again,
Guys, kukaa ndani huku ukiwa na hofu kuna bore, hakuna namna tunaweza kuliweka hili suala mezani!?
Mezani linakaaje, hivi mtu kamuua Mama yako, mtoto wako au Baba yako mnakaa mezani kufanyaje?
Malipo yake alistahili naye kufa kama alivyoua wengine, akipata msamaha sana ni awapishe watu wengine ambao mikono yao ni misafi hainuki Damu
 
1430773798.jpg
 
NYIE endeleeni tu kucheza na huyu mama atawamaliza maana hamuelewi mnaingia kwenye vita mikono mitupu wakati wenzenu wako serious mko serious kweli.hao jamaa hapo hawasaki ndezi wanasaka roho za watu .ndo maana nawaambia safari hii kama mnania basi mjipange na mumjuenadui yenu ni nani.
Hivi hujaona tu juzi hapo Busara alizozitumia Rutto? Watu wameshafika hatua ambayo uhai kwao sio kitu kuliko kuendelea kutawalia na mafashisti na wahuni. Mtaua 10,000 watabaki 100 ndo mbegu hiyo, Ili zao litoke udongo lazima utifuliwe, ardhi inalia, Jembe linalia, mlimaji analia ila mwisho wa siku wote watacheka Mwishoni ndo tulipo
 
Unapindua Serikali yenye majeshi yote halafu hauna hata kisu?
Majeshi ya serikali yana Siraha, Ili uwashinde uwe siraha zaidi Yao.
Mnaongea Kama Kuku waliokatwa vichwa ila tunajua mpo kazini kupandikiza Uoga, South Africa Waliuliwa watu wengi sana na makaburu, Gaddaffi alikuwa na jeshi kubwa hili la Tanzania ni takataka, ila ilichukua Wiki tu akatembea. Waachieni Vijana wadai Nchi yao, Kwa njia yoyote watakayoona inafaa, wako tayari kulipa hiyo bei. Kama ni uhai wenzao wametangulia Majuzi.
 
Back
Top Bottom