PostGE2025 Gen Z hawapoi: Desemba 9, 2025 kuja na maandamano mapya

PostGE2025 Gen Z hawapoi: Desemba 9, 2025 kuja na maandamano mapya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Bado hamjajifunza namna maandamano yalivyosababisha fitna na mabalaa kwetu. Nimejifunza kitu, kwa yaliyotokea na kwa jinsi nilivyoona kwenye baadhi ya vyombo vya habari vya nje hasa vya Kenya, nimeamini kuna hujuma Tanzania inafanyiwa, na Allah ni Mjuzi zaidi. Ninamuomba Allah Ailinde nchi yetu na Aidumishe Amani yetu.

Damu za ndugu zetu hazijawatosha. Na uharibifu wote uliotokea hayajawatosha, mnataka muichome nchi yetu zaidi na watu wafe halafu msambaze picha za maiti zao kuudhalilisha utu wao zaidi, mnataka kutimiza malengo yenu kwa damu zetu na heshima zetu. Nyinyi sio watu wazuri kabisa.
Acha kupiga kelele kama mtu anaetatuliwa linda kwa nini Rais hataki kukaa chini kuzungumza na hao watu Rais mwenye kajichagua haiachaguliwa na, watu alafu analeta dharau
 
Mnaongea Kama Kuku waliokatwa vichwa ila tunajua mpo kazini kupandikiza Uoga, South Africa Waliuliwa watu wengi sana na makaburu, Gaddaffi alikuwa na jeshi kubwa hili la Tanzania ni takataka, ila ilichukua Wiki tu akatembea. Waachieni Vijana wadai Nchi yao, Kwa njia yoyote watakayoona inafaa, wako tayari kulipa hiyo bei. Kama ni uhai wenzao wametangulia Majuzi.

Nikajua na wewe unaenda kuandamana. Kumbe unahamasisha wenzio huku ukiwa uvunguni mwa kitanda.
Huoni wewe ndiyo unaongea kama umekatwa kichwa.
 
Unaoengea nini wewe au unaongelea mali za watu?!

Kabla ya maandamano raia walitekwa kubakwa kupotezwa na kuuwawa kinyama na uongozi huu huu wa CCM Na POLISCCM

Ulitaka tukae kimya mpaka lini?
TUTAKIWASHA 9Dec!
Mali zenyewe za Mafisadi
 
Bado sijajua kiongozi wa hay maandamano ni nani Hadi sasa!

Lakini namwambia hiyo sio njia sahihi Kwa watz kudai haki zao!!

Tuzungumze na samiah aliahidi katiba mpya kwenye kampeni,tumdai aitishe bungee la katiba!
Kama mpaka sasa Unafikiri Samia anaweza kutoa katiba na mambo yote aliyofanya Utakua unaota atoe katiba itayomfunga yeye na swahiba wake JK Haiwezekani nafasi alikua nayo pale Magufuli amefariki ya kutoa katiba mpya maana alikua bado ni msafi ule mwaka wa kwanza alitakiwa kutoa katiba huwezi kupata katiba kwa sasa acha ndoto za Mchana
 
Seran uko wapi mzima popote ulipo jitokeze kipenzi maana mwanza palikua pa moto sana sema kitu na roho yangu itapona
Jamani mi nimejaa tele ni kukoswa koswa na mabomu tu ila niko salama Mungu mwema! Huku wezi walijipatia nafasi tu wakafanya yao ila mambo yalikuwa ya moto! 🔥
 
Gen Z wangepita majumbani mwa watu na kutoa onyo kali kwamba hakuna mtu yoyote kubaki nyumbani labda mama mjamzito na watoto chini ya miaka kumi ila wote tuingie barabarani
Hii ilifanyika Arusha nasikia
 
Acha kupiga kelele kama mtu anaetatuliwa linda kwa nini Rais hataki kukaa chini kuzungumza na hao watu Rais mwenye kajichagua haiachaguliwa na, watu alafu analeta dharau
Wanaotatuliwa kumbe wanapigaga kelele 😂😂😂😂
 
December ni mbali sana. Momentum ya wakati huu ndiyo ingetumika kuendeleza pale walipoishia.

Tanzania isingeweza kustahimili kiuchumi kufunga mitandao na kuweka watu ndani hata kwa wiki moja zaidi. Pia dunia nzima ilianza kuangalia kinachoendelea. Yale mauaji yasingeweza kufanyika kwa siku tatu au nne mfululizo.
 
29/10/2025 Jumatano nilikuwepo hadi saa 3 usiku, ila Polisi walipiga vyuma aiseee ukitizama ni cheche tu
Duuh na inaanzaga hivi hivi.
Kwa sasa watanzania ni kama wamejisusa just imagine POLISI & TCRA kila mara kutuma msg za vitisho mara hatua kali zitachukuliwa. Ila hicho wanachokataza ndio kinafanyika zaidi. Tesha alishauri kitu kwamba vitisho vya kisaikolojia havina tija kwa sasa
Wanataka watu waishi kama Israel na Gaza, ndo watu washaamua ishi hivyo na mwenda wa kuviziana tu hakuna kingine.
Ukipata upenyo wewe fanya lako mapema.
Usisahau gloves na bleach kufuta DNA yako
 
Back
Top Bottom