Godbless Lema: Kuna mtu mkubwa anataka kujenga hoteli Ngorongoro

Godbless Lema: Kuna mtu mkubwa anataka kujenga hoteli Ngorongoro

Kaongeza kuwa wanasubiri wapate makaratasi/ karatasi kuna siku watamtaja.
Kutokumtaja ni dalili fulani hivi za kutengeneza mazingira ya kuomba rushwa. Kama yupo "clean" huyo mtoa tuhuma aje 'front' kuwataja anaowatuhumu.
 
Safi kabisa!

Mpaka akili ziwakae sawa,

Maana yule mwingine tulimwita dikteta, dhalimu, muuaji!

Sasa tunapumua!
Huyo kweli alikuwa na sifa Zote, mfano ni wafuasi wake.sabaya &makonda.
 
Nchi hii ni kubwa sana na kila raia ana uhuru wa kuishi popote. Kama tuliwahi tuliwahamisha wafugaji wa usukumani (bila kujali kabila gani) miaka ya 90 kuwapeleka Morogoro, Lindi na Mbeya kunusuru mazingira, kuna ubaya gani kuwahamisha wafugaji wa ngorongoro kunusuru hifadhi na wanyama? Leo hii tuna Wamasai nchi nzima na hawabaguliwi na bado ni kivutio cha watalii kwa shughuli zao za kimila wafanyazo. Napongeza Azimio la Bunge, kama kuna sheria ilibariki hayo, setikali iifanyie mabadiliko yatakayoendana na uhalisia wa sasa.
 
Mama hataki shida
Jana kasema chaguo ni letu tukitaka Ngorongoro iangamie sawa tu na tukitaka ilindwe sawa

Kama vile JK watu walipoanzisha sekeseke la kutaka Mchakato wa Katiba mpya akaridhia na walipokuja na sekeseke la kutaka mchakato wa katiba mpya usitishwe nako pia akaridhia…matokeo yake wote tunayajua
Hii issue inaenda kuwa kubwa sana huko mbeleni unless wanaachana na huo mpango wao.
 
Jambo moja Katika hii nchi kila mtu anasema lake hata hao Wapinzani husema mengi ya uongo...Wakati mmoja walisema Mlinzi wa Magufuli kafa kumbe sio kweli....
Cha msingi kila mtu ananyandua anachoweza basi
 
Hii ni kauli ya Godbless Lema kupitia mariaspace muda mfupi uliopita.

Kaongeza kuwa wanasubiri wapate makaratasi/ karatasi kuna siku watamtaja.

Swali: Mtu huyu ni nani?
Kibibi cha kiarabu mwaka tu tayari kinagawa urithi wetu Ngorongoro kwa ndugu zake warabu wa kwao Oman.. LAANAKUM Hangaya.
 
Jambo moja Katika hii nchi kila mtu anasema lake hata hao Wapinzani husema mengi ya uongo...Wakati mmoja walisema Mlinzi wa Magufuli kafa kumbe sio kweli....
Cha msingi kila mtu ananyandua anachoweza basi
Akili zako hazina akili.
 
Lema azingatiwe....tusimpuuze moja kwa moja huyu mtu

Baada ya miaka kadhaa huenda tukaja kumuona alisema kitu cha msingi sana...

Mambo kama haya ni kuyapa muda tu,, hakuna ulazima wa kubisha saaana wala kukubali,,, Wakati ukifika uzushi hujitenga na Ukweli
 
Je sheria imezuia kujenga hotel Ngorongoro? Kwani hakuna hotel? Vipi angetaka kujenga mtu mdogo ingekuwa nongwa?

Acheni upumbavu usio na faida nyie machadomo.
kwani umekatazwa kujenga.. tunapinga wananchi kufurushwa kwenye ardhi yao na kuleta hao mabazazi wenu
 
Ile branding ya Tanzania Royal Tour; head guide akiwa SSH ime summarize kila kitu!
Ila mimi naomba niseme kitu: Tunapopinga au kukubali Wamasai kuondolewa kutoka mle NCA tusiishie hapo tu. Tuanze sasa kupinge vile vile ujenzi holela wa hoteli za kitalii na ofisi za NCAA.
Kila kitu kijengwe maeneo nje ya hifadhi kuruhusu uhifadhi endelevu!

NB: Sera ya ujenzi nje ya hifadhi ihusu hadi hifadhi zilizo chini ya TANAPA!
Tusiposimama imara ipo siku hifadhi zetu zitakosa maana kutokana na ujenzi holela wa hoteli.
Kitu ambacho wengi hawajui; makampuni makubwa ya utalii yenye sifa mbaya maeneo mengi duniani ndo yale yale tunayakumbatia kwa kuwapa maeneo nyeti ndani ya hifadhi zetu!
 
Back
Top Bottom