God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Free will ni uhuru wa kuchagua mema na mabaya, wote tunakubaliana na tafsiri hiyo.

Na kwamba ubaya unatokea kwasababu kuna freewill na bila freewill kusingekuwa na raha kwasababu watu wangeishi kama robots

Anyway. Peponi kuna freewill au haipo?
 
Ikiwa Mungu anafanya mambo yote kwa shauri na mapenzi yake, utasemaje una freewill ya kuchagua unachotaka?
 
Unakakubali kuwa kila jambo hutokea kwasababu au kuna bahati mbaya?
Tulikuwa na concept ya freewill, tukaingiza predestination; unataka tuongeze concept ya tatu - determinism? Mbona tutakesha sasa. 😁
 
Kujua kwa Mungu mambo yote hata kabla sijazaliwa kunanizuia kufanya mimi nayo taka unless niwe na option ya kufanya kile ambacho yeye hajakiona au kwenda kinyume na alivyoona
Wewe kwa mfano kama unajua Juma asiposoma atafeli na akisoma atafaulu kunamzuiaje Juma kusoma na akafaulu au kutokusoma na akafeli?
 
Kabla ya kuzaliwa kwako Mungu akijua utaua, una option ya kutoua?

Kama huna option ya kutoua utasemaje sijazuliwa kufanya nachotaka?
Kama Mungu anaingilia mambo ya wengine na kama hakuna freewill basi kusingekuwa na uovu.

Uovu upo kwa kuwa mnatumia freewill zenu kuamua kuwa waovu.

Hakuna anayekupangia.
 
You must be kidding! Yesu alifundisha maporini?

Luka 23:2
Wakaanza kumshitaki, wakisema, "Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo Mfalme."

Kama hawakumjua ni nani, na alishinda porini akisali; walimwonaje akipotosha watu wasilipe kodi?
 
Ikiwa Mungu anafanya mambo yote kwa shauri na mapenzi yake, utasemaje una freewill ya kuchagua unachotaka?
Wewe unapofanya mambo yako kwa uhuru inamaanisha sisi wengine hatupo huru?

Mungu anatumia uhuru wake kufanya mema, sisi nasi tunatumia uhuru wetu kadiri tupendavyo.

Kila mmoja anashinda mechi zake.
 
Tulikuwa na concept ya freewill, tukaingiza predestination; unataka tuongeze concept ya tatu - determinism? Mbona tutakesha sasa. 😁
Hili sio jambo la kuongezwa, ni jambo ambalo lipo na linafungama na sifa za Mungu wako otherwise umpunguze sifa Mungu ili tui exclude hiyo hoja hapa

Kwa sifa za Mungu ni kwamba kila kitu kilishakuwa calculated na hapa tunapita njia aliyotuwekea sisi japo katika fikra zetu tunaweza hisi tunafanya mambo kwa utashi wetu Refer katika ile verse ya ephisians.

Sasa kama kila kitu kinachotokea hakitokei kwa bahati mbaya, ipi nafasi ya mtu kuwa responsible kwa matendo ayafanyayo wakati tayari alikwisha umbwa aje afanye hayo aliyofanya?
 
Wewe kwa mfano kama unajua Juma asiposoma atafeli na akisoma atafaulu kunamzuiaje Juma kusoma na akafaulu au kutokusoma na akafeli?
Mfano wako hauko relevant

Kwasababu ujuzi wangu sio wa uhakika, pili swala la juma kutosoma sio uamuzi wake maana alikwisha pangiwa asije kusoma tangu hata hajazaliwa na hakuweza kuepuka hilo

Niambie kwa namna gani Juma angeweza kutumia freewill ya kusoma na kufaulu ikiwa Mungu alikwisha mpangia tangu hajazaliwa?

Ubaya na wema ni matokeo ya freewill

Sasa mama mjamzito anayetoa mimba kwa kukiua kichanga tumboni halafu Mungu alikwisha kujua hilo na alikuwa na uwezo wa kulizuia lakini akaruhusu litokee kwasababu ya freewill

Kama Mungu anajali freewill, ni ipi nafasi ya hicho kichanga kutumia freewill kati ya kuchagua kuuliwa au kutouliwa?
 
Kama Mungu anaingilia mambo ya wengine na kama hakuna freewill basi kusingekuwa na uovu.

Uovu upo kwa kuwa mnatumia freewill zenu kuamua kuwa waovu.

Hakuna anayekupangia.
Unatumia ubaya kufanya mazuri yaonekane mazuri

Kwani haiwezekani kuwa na freewill yenye kuchagua mazuri pekee?
 
Wewe unapofanya mambo yako kwa uhuru inamaanisha sisi wengine hatupo huru?

Mungu anatumia uhuru wake kufanya mema, sisi nasi tunatumia uhuru wetu kadiri tupendavyo.

Kila mmoja anashinda mechi zake.
Verse haizungumzii uhuru wa Mungu kwenye mambo yake, imnazungumzia nafasi ya Mungu katika kuwapangia watu mambo yote kwa mapenzi yake

Mungu anayewachagulia watu kwa kusudi lake, hao watu waliochaguliwa kwenye mambo fulani utasemaje wametumia freewill kuchagua hayo waliyo chaguliwa?
 
Davinci naona unayachakata mawazo mithili ya Tafakuri na tungo za dan brown ndani ya code ya maria magdalena kukimbilia ulaya/ufaransa na ujauzito wa bwana Yeshua/Yesu Mnazeleti na uzaoo wake upo hadi hivi sasa-holy grail' (Mark 16-8 ):

Project yangu ipo mbioni kumalizika "ALISINA UTACHOMWA MOTO NAKUAPIA"

Huku miaka mitano Ijayo Project ya "FREEDOM FROM RELIGION FOUNDATION -TANZANIA"
 
Unathibitisha ya kuwa mfano wako si halisi. Swali langu la msingi unalotakiwa kujibu ni kuwa kujua kwake kuna kuzuia nini wewe kufanya unalo taka ?

Mola wetu kwa kutuumba sisi na kutujua vizuri nje ndani anajua cha kabla na baadae, mfano mwepesi sana, wewe lro hii kwa kumjua kwako vizuri mtu fulani basi huwa unajua nini atafanya baada ya jambo fulani.

Sasa hapo ndipo ulipo uhuru kamili wa mwanadamu, Allah anajua kila kitu ana uwezo wa kila kitu, lakini anakuacha ufanye unachotaka sababu amekupa uhuru ila angetaka kuzuia angezuia.
 
Kabla ya kuzaliwa kwako Mungu akijua utaua, una option ya kutoua?

Kama huna option ya kutoua utasemaje sijazuliwa kufanya nachotaka?
Options zipo kibao, kuna kuomba dua Mola akuepusha na madhila. Ndiyo maana huwa tunaomba msamaha kwa makosa tunayofanya na kusamehewa, na dua hubadilisha aliyokupangia Mola.
 
Unashindwa kuelewa jambo

Ni kwamba katika concept ya freewill na dhana ya Mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na mwenye upendo wote.

Tunasema freewill ni illusion kwasababu kila kitu kilipangwa though the choice may seem very free for you but in reality you're choice cannot be otherwise
 
Options zipo kibao, kuna kuomba dua Mola akuepusha na madhila. Ndiyo maana huwa tunaomba msamaha kwa makosa tunayofanya na kusamehewa, na dua hubadilisha aliyokupangia Mola.
Hapa ndipo unapojichanganya

Kuomba kwako dua kutakuwa ni kitu kipya kitachoweza kubadilisha maono ya Mungu?

Kuomba kwako msamaha nako sio kwa utashi wako, na hata ukibadilishiwa hiyo itaonekana hivyo katika perception yako lakini uhalisia ni kuwa yeye ndiye alitaka iwe hivyo
 
Free will ni uhuru wa kuchagua mema na mabaya, wote tunakubaliana na tafsiri hiyo.

Na kwamba ubaya unatokea kwasababu kuna freewill na bila freewill kusingekuwa na raha kwasababu watu wangeishi kama robots

Anyway. Peponi kuna freewill au haipo?
Nitajibu;

Ndiyoni freewill ni kuchagua mema na yasiyo mema kwetu, kuchagua kwenda left ama right wewe tu na utaendelea kuyapata matokeo kadri ya unavyochagua.

Ndiyo, ubaya ni matokeo ya makosa katika chaguzi zetu, na mda mwingine unatufunza kuwa njia ile ya mwanzo sio sahihi, tubadilike/tubadilishe.

Na ipo popote utakapokuwa utakuwa na freewill [hadi levo fulani za mbinguni] kulingana na mazingira utakayokuwapo [mfano huwezi kuamua tu kupaa ukiwa duniani], free will ni sifa zetu wanaadamu na baadhi ya viumbe wengine wa Mungu. Ndiyo maana kuna mahala Yesu alisisitiza sana kuwa tutumie utashi wetu kuyafanya mapenzi ya baba wa Mbinguni. Kumbe hata yeye angeweza kutotii kukinywa kikombe kama angeamua hivyo ila akaamua kutumia utashi wake kukubali kuyatenda mapenzi ya Baba yake. Maana huo ni mfano mzuri wa kujitoa kwa upendo kusema ukweli hata kama maisha ya matatani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…