ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,922
- 3,916
Je mleta maada, wakati unajiuliza uwezo wa Mungu na Uhuru wa kuchagua. Je umejiuliza maswali haya mawili?. 1. Je ni kweli tuliumbwa na Mungu?. 2. Kama ni kweri kwa Nini alituumba?. Kama hatujaumbwa na Mungu maada hiii Haina maana. Sasa kwa umuhimu wa maada hii ni kwanza lazima tukiri tuliumbwa na Mungu. Sasa kwa Nini alituumba?. Kwa wakatoliki jiubu huwa tumpende, tumujue na tumutumikie ( kwa kifupi Yeye anatafuta recognization only).Mungu anajua hatma kwasababu yupo nje ya time dimension. Hivyo yeye anakuona mwaka 2000, anakuona mwaka 2022 na anakuona mwaka 2040 (mfano tuu).
Hajakupangia wala haku control ila anakuona unavyofanya maamuzi yako na unavyovuna matokeo yake.
Hata hivyo ameweka njia ambayo ukichagua kuifuata unapata matokeo mazuri wakati wote.
Kujua kwa jambo kuna kuzuia nini weww kufanya unachotaka ? Shida yenu wote wanao pinga hii "free will" hawaonyeshi uhusiano wa kujua na kufanya matendo.
Katika Uislamu kuna baadhi ya makundi yalikuwa yanaitwa Jahmiyah na Jabriyah, hawa walikuwa wanajinasibu ya kuwa wao ni Waislamu, katika istilahi ya Kiislamu tunaziita "Firaq" hawa katika itikadi zao walikuwa wanasema au kuamini ya kuwa "Mwanadamu hana uhuru wa kuchagua, yaani ni kama vile ua au jani linalo au lililo pulizwa na upepo" lakini wote walio kuwa na imani hiyo hawaonyeshi popote uhusiano wa kujua na ufanyaji matendo. Hili ni tatizo la kulazimisha mambo na kutofikiria mambo kwa undani.
Nakubaliana na wewe hakika hapa ndo pana utata. Mi nadhani hutajitambua kabisa kwa sababu hutakumbuka kabisa ya duniani. Mind inaikomind brain kufanya vitu. Na kumbukumbu zipo kwa brain zimetunzwa. Wanasayansi walishadhibitisha ubongo ndio unaotunza kumbukumbu. Ni baada ya jamaa mmoja kupoteza sehemu ya ubungo wake katika ajali, ikawa kuna vitu anakumbuka ila vingine hakumbuki kabisa.
Ila tumetoka mbali sana ni karne ya juzi tu hapa watu wa kisomo walikuwa wakidhania moyo ndo unatunza kumbukumbu.
fre will is illusion
Ambao mnadhania kuna free will mnijibu haya.
- wapi ulichagua kuzaliwa, unafikiri ungepewa nafasi ya kuchagua ungechagua kuzaliwa maxingira uliyopo. Why ulikuwa walia ulivyozaliwa tu
- wapi ulichagua kuwa muumini wa dini unayoabudu. Jee wazazi wako wangekuwa dini tofauti na yako uliyonayo sasa hivi, ungekuwa na dini hii unafikiri?
- kwa wale walio na magonjwa ya kurithi, hivi kuna sehemu walichagua kuwa nayo au the whole sequence of events was predetermined from moment their parents fall in love to moment they conceive.
Freewill ipo kwenye uhuru tuliopewa wa kufanya maamuzi ya ama kuwa wema ama wabaya.
Kwamba, Mungu hatakaa aingilie uhuru wa uamuzi wote unaoufanya mpaka utakapokufa.
Amekupa mamlaka ya kujichagulia hatma yako - uwe mwema ama mbaya.
As I said there is no freewill at all, it is just an illusion
Free will haipaswi kuwa na mipaka, na kwa perception ya kimungu, hiyo comment sijaandika kwa utashi wangu na nilikuwa sina uwezo wa kuepuka kutoiandika. ikiwemo na hii nayoandika sasa
Ephesians 1:11
11 All things are done according to God's plan and decision; and God chose us to be his own people in union with Christ because of his own purpose, based on what he had decided from the very beginning.
Ikiwa kila kitu ni mipango ya Mungu utasemaje tuna freewil?
Kama tuna free will kivipi kila jambo liwe ni sehemu ya mipango yake?
Jibu swali nililo kuuliza, kujua kwa Mola, kupanga mambo kuna uhusiano gani na wewe kushindwa kufanya unachokitaka ?Unashindwa kuelewa jambo
Ni kwamba katika concept ya freewill na dhana ya Mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na mwenye upendo wote.
Tunasema freewill ni illusion kwasababu kila kitu kilipangwa though the choice may seem very free for you but in reality you're choice cannot be otherwise
Hakuna sehemu niliyo jichanganya, ni wewe kutokuelewa jambo husika.Hapa ndipo unapojichanganya
Si kitu kipya sababu Allah anajua kila kitu "in general" na anajua kila kitu "in details".Kuomba kwako dua kutakuwa ni kitu kipya kitachoweza kubadilisha maono ya Mungu?
Ni utashi wako ndiyo maana unajua hapa umekosea na hapa unatakiwa ufanye kadha wa kadha.Kuomba kwako msamaha nako sio kwa utashi wako, na hata ukibadilishiwa hiyo itaonekana hivyo katika perception yako lakini uhalisia ni kuwa yeye ndiye alitaka iwe hivyo
Sijaelewa swali lako. Nipe ufafanuzi.Unakuaga na logic za kidini sana ila sisi tulikua tunaamin ivo ivo sasa kama anajua itazuia nn mm kufanya nafny sabab alijua nitafnya
Weka umakini sio kila jibu linaanza na neno "kwasababu"Jibu swali nililo kuuliza, kujua kwa Mola, kupanga mambo kuna uhusiano gani na wewe kushindwa kufanya unachokitaka ?
Mungu akijua utaenda kushoto, hapo una uchaguzi wa kufanya unachotaka ukaenda kulia?Hakuna sehemu niliyo jichanganya, ni wewe kutokuelewa jambo husika.
Si kitu kipya sababu Allah anajua kila kitu "in general" na anajua kila kitu "in details".
Anajua mja wangu atatoka hapa ataenda pale ? Atafanya kadha ? Atakosea ataomba msamaha, nitambadilishia nilichompangia sababu atafanya jambo fulani. Jambo rahisi sana hili.
Mimi nasubiri mnionyeshe uhusiano wa kujua kwake Allah ana kuzuia nini weww kufanya unachotaka ?
Kwanini una akili na kwanini una matashi na kwanini una uwezo wa kufanya jambo fulani na kuacha jambo fulani ?
Ni utashi wako ndiyo maana unajua hapa umekosea na hapa unatakiwa ufanye kadha wa kadha.
Umeona e, maoni yako tafadhaliMada ngumu sana hii
Maelezo mengi mpaka nimeshindwa kujua umejibu wapi swali languNitajibu;
Ndiyoni freewill ni kuchagua mema na yasiyo mema kwetu, kuchagua kwenda left ama right wewe tu na utaendelea kuyapata matokeo kadri ya unavyochagua.
Ndiyo, ubaya ni matokeo ya makosa katika chaguzi zetu, na mda mwingine unatufunza kuwa njia ile ya mwanzo sio sahihi, tubadilike/tubadilishe.
Na ipo popote utakapokuwa utakuwa na freewill [hadi levo fulani za mbinguni] kulingana na mazingira utakayokuwapo [mfano huwezi kuamua tu kupaa ukiwa duniani], free will ni sifa zetu wanaadamu na baadhi ya viumbe wengine wa Mungu. Ndiyo maana kuna mahala Yesu alisisitiza sana kuwa tutumie utashi wetu kuyafanya mapenzi ya baba wa Mbinguni. Kumbe hata yeye angeweza kutotii kukinywa kikombe kama angeamua hivyo ila akaamua kutumia utashi wake kukubali kuyatenda mapenzi ya Baba yake. Maana huo ni mfano mzuri wa kujitoa kwa upendo kusema ukweli hata kama maisha ya matatani.
Unachanganya kati ya foreknowledge, kujua kitu kabla hakijatukia na kufanya kitukie.Mungu anajua kila kitu kutuhusu sisi wanadamu, anajua kesho nitakua wapi,nitakula nini na nitakufa lini...pia ametupa uwezo wa kuchagua kuishi ville tupendavyo bila yeye kutuingilia(free will) sasa hapa ndio kuna msingi mkuu wa mada yangu ambapo imekua ikinitatiza sana jambo hili. Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema? Je anajua kwamba mimi nikifa nitakua wa mbinguni au wa motoni? Na kama anajua nikifa nitafikia motoni je mimi naweza kubadirisha nisiende motoni?
Mungu anajua maamuzi yako yote na utakavyoishia. Ni kama uone mkanda wa video mpaka mwisho halafu muwe mnaangalia na wengine. Hakuna kinachobadilika. Sema mfano huu sio mkamilifu kwa sababu Mungu hana mfanowe. lakini utakupa picha!Kumbuka kwamba kama nitaweza kubadirisha nikaenda mbinguni badala ya motoni basi Mungu anakua hajui kila kitu kuhusu mimi…
Kila mwanadamu ametenda dhambi na amehukumiwa kwenda Jehanamu. Yesu ametoa nafasi kwa wanaotaka kulipiwa deni lao kumwamini. Mungu anajua kama utatumia utashi wako kuchagua kumwamini Yesu ama la! Na kwa sababu hiyo anajua kama uchaguzi wako ni wa Jehanamu ama mbinguni. Kumbuka kwenye hili Mungu sio bystander bali ndiye Jaji haswa na sheria anaijua vizuri.Pia kama anajua moja kwa moja nitaenda motoni basi wanadamu hatuna uhuru wa kuchagua kufanya yale tupendayo.
Hapa sijui kama umetumia akili sawasawa kuwaza. Kama nikijua leo utaamua kuwa mwizi kesho maana yake hauko huru kwa sababu nimejua? Kwamba nimekupangia kwa kuwa nimejua utakachofanya?Mungu kama anajua tutachagua kufanya kitu Fulani kwa uhuru basi huo sio uhuru tena bali tunapangiwa yale ya kuchagua
Shida yako unachanganya mambo. Mungu kujua au kutojua utakachofanya kwa uchaguzi wako hakuna madhara kwenye utashi. Mimi nikijua ama nisjue kesho utaiba sukari haibadilishi uhalisia kuwa ulichagua kuba sukari!hivyo free will hatuna its illusion na kama Mungu hajui kama nitachagua jambo Fulani kwa uhuru basi anapoteza sifa ya kujua kila kitu toka kwangu.?
IpoMaelezo mengi mpaka nimeshindwa kujua umejibu wapi swali langu
Peponi kuna freewill au haipo?
Kwa hiyo nako peponi ipo possibility ya uovu kufanyika?I
Ipo
Ukifikia hatua upo peponi, upo Edeni, upo uweponi mwa Bwana unakuwa unaweza kuwa mwovu in theory. Lakini hapo upo tried and tested kiasi kwamba uovu kwako ni almost impossible.Kwa hiyo nako peponi ipo possibility ya uovu kufanyika?
Nakukumbusha kuwa Freewill ni uchaguzi wa mema na mabayaUkifikia hatua upo peponi, upo Edeni, upo uweponi mwa Bwana unakuwa unaweza kuwa mwovu in theory. Lakini hapo upo tried and tested kiasi kwamba uovu kwako ni almost impossible.
Au tuseme kuna hatua fulani unaweza kufanya uovu ila kuna hatua unafikia kuwa mtakatifu kama Mungu mwenyewe alivyo mtakatifu mambo ya uovu yanakuwa kwako hayapo.
Sema kabla hujafikia utakatifu unaweza kukosea lakini kadri unavyoupunguza umbali wako wa kiroho kutoka pointi A[unyama] kupitia pointi BCD [Ubinadamu] hadi pointi X[Umungu]. Ndio umazidi kupunguza uwezekano wa kutenda dhambi hadi almost zero.
Nasema almost zero kwa kuwa kwa sisi hadi kumfikia Mungu kuna infinity hatuas. And that is a good thing😊