Wewe kufanya uovu ni matokeo ya wewe kuacha kufanya mema, maana yake ungetaka kufanya wema ungefanya ila ukachagua kufanya uovu. Kwahiyo hiyo ni juu yako.Uwezo wa kufanya uovu na ubaya amenipa Mungu, sio? Mimi kufanya uovu ni matokeo ya kushindwa kufanya mema kutokana na vichocheo vya ubaya kuzidi ndani yangu, sasa nani aliniumba hivi? Kwanin aruhusu vichocheo vya ubaya kuzid wema ndani yangu? Utasema mim ndo nimechagua, Kwanin nimechagua ni kwasababu ya udhaifu uliopo ndani yangu ambao Mungu ameniumbia nao, kwanin aniwekee mtego huu?
Sababu amekupa uhuru, yaani amekupa vyote ukitaka kufanya wema unafanya na ukitaka kufanya uovu unafanya. Kwahiyo kufanya kwako wewe uovu ni matokeo ya kuzembea kadhalika.