GPA ya 5 - Anazurura mtaani; we are not serious!

Sio kila mtu anasoma/amesoma SUA.

Vyuo vingi inaagaliwa grade, A ya 81 na ya 99 zote ni point sawa, kama wanatafuta top student, ndio wataangalia hizo marks.
Ni kweli nilisema tu ili watu wasidhani ni vyuo vyote grade ndo inatumik
 
Mtoa mada buana!mtaani na maofisin hatuishi kwa GPA,Mimi Nina GPA ya 2.1 lakini pengo langu hakuna wa kuliziba ofisini kwetu ingawa wapo wenye hizo GPA za 4s.
Mwalimu unajisifia pengo lako hakuna wa kuliziba? Huna akili
 
Hizo GPA ya 5 mnapataje Nyie vitoto vya sasa? Unajua maana ya GPA 5 Points.

Maskini Tanzania! Ni ya chuo gani hiyo GPA?
Na mimi nashangaa GPA ya 5, labda computation ipo kinamna.
 
Hizo GPA ya 5 mnapataje Nyie vitoto vya sasa? Unajua maana ya GPA 5 Points.

Maskini Tanzania! Ni ya chuo gani hiyo GPA?
Mzee hii nchi kuna vichwa aisee labda kama hujakutana navyo tu, mimi sikuamini mpaka nilivyokutana na mwanafunzi ana A zote mwaka wa kwanza na wa pili!, (sasa hivi yupo mwaka wa tatu kozi ngumu tena sayansi!) asipoyumba mwaka huu wa mwisho lazima awe overall
 
Safi sana,
 
Kwa mtazamo wangu tumechelewa kujua umuhimu wa pass za juu katika kupaisha Taifa kiuchumi nk
Hivi inakuwaje mwanafunzi amemaliza Chuo amepata GPA ya 4.8 au kwa wenzetu wa Arts wanapata hadi GPA 5 naye yupo mtaani hana ajira?
Kosa kubwa sana la kiufundi,Hawa vijana wanaopasi kwa alama za juu,kuanzia secondary mpaka vyuoni,ilibidi wapewe nafasi kubwa walelewe kwenye vitengo kazi wanazozitaka,au kuwafaa,wapikwe mpaka waive ndani na nje ya nchi,then wapewe nafasi wafanye maajabu baada ya kuiva,sasa li inchi letu mtu katoka chuo bado amejaa nadharia tu na anaufaulu mkubwa wanataka ajiajiri,ushenzi mtupu
 
Huo zamani tuliuita USONGO! Ni ujinga fulani uliokuwa umetuingia vichwani.
Msongo hujikita kusoma tu bila kutengeneza connection, markert demand nk.
Unasoma soma tu ili ufaulu halafu ulichokisoma hakiitajiki sokoni, huo ufaulu unakuwa na maana gani?
Ufaulu mkubwa wa sasa uendane na mahitaji ya soko. Mfano wewe una GPA 5. ya BA in history na mwenzio ana ufaulu wa Finance au Data science unafikiri ufaulu upi utafaa mtaani hapo? Je yupi atabaki anazurura kama mbuzi wa uswahili ?
 
A modern HR professional doesn't rely on GPA when recruiting!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…