GPA ya 5 - Anazurura mtaani; we are not serious!

GPA ya 5 - Anazurura mtaani; we are not serious!

Sio kila mtu anasoma/amesoma SUA.

Vyuo vingi inaagaliwa grade, A ya 81 na ya 99 zote ni point sawa, kama wanatafuta top student, ndio wataangalia hizo marks.
Ni kweli nilisema tu ili watu wasidhani ni vyuo vyote grade ndo inatumik
 
Mtoa mada buana!mtaani na maofisin hatuishi kwa GPA,Mimi Nina GPA ya 2.1 lakini pengo langu hakuna wa kuliziba ofisini kwetu ingawa wapo wenye hizo GPA za 4s.
Mwalimu unajisifia pengo lako hakuna wa kuliziba? Huna akili
 
Hizo GPA ya 5 mnapataje Nyie vitoto vya sasa? Unajua maana ya GPA 5 Points.

Maskini Tanzania! Ni ya chuo gani hiyo GPA?
Na mimi nashangaa GPA ya 5, labda computation ipo kinamna.
 
Hizo GPA ya 5 mnapataje Nyie vitoto vya sasa? Unajua maana ya GPA 5 Points.

Maskini Tanzania! Ni ya chuo gani hiyo GPA?
Mzee hii nchi kuna vichwa aisee labda kama hujakutana navyo tu, mimi sikuamini mpaka nilivyokutana na mwanafunzi ana A zote mwaka wa kwanza na wa pili!, (sasa hivi yupo mwaka wa tatu kozi ngumu tena sayansi!) asipoyumba mwaka huu wa mwisho lazima awe overall
 
[emoji23][emoji23][emoji23]umenikumbusha mbali kipindi na mimi nimemaliza chuo nahustle hakuna aliekua na time na mimi,wote wenye uwezo wananicheki tu waone nitaishia wapi,wengine wananisikitikia eti kasoma lakini hana kazi,anadhurura mtaani,elimu haijamsaidia

Nimekuja kulamba shavu kwa juhudi zangu,mambo safi sasa naanza ona simu simu,mara naitwa kijana wetu,mara kaka.

Walikua na vijigari vyao,wamejenga vijumba wanajidai dai,nimewalipa mara mbili.

Binadamu ni wanafiki,nimechinjia wote baharini,wanabaki wanasema tu.ooh eti ninadharau [emoji23]

Ulikua huna time na mimi,na mimi sina time na wewe

Sitakagi ujinga
Safi sana,
 
Kwa mtazamo wangu tumechelewa kujua umuhimu wa pass za juu katika kupaisha Taifa kiuchumi nk
Hivi inakuwaje mwanafunzi amemaliza Chuo amepata GPA ya 4.8 au kwa wenzetu wa Arts wanapata hadi GPA 5 naye yupo mtaani hana ajira?
Kosa kubwa sana la kiufundi,Hawa vijana wanaopasi kwa alama za juu,kuanzia secondary mpaka vyuoni,ilibidi wapewe nafasi kubwa walelewe kwenye vitengo kazi wanazozitaka,au kuwafaa,wapikwe mpaka waive ndani na nje ya nchi,then wapewe nafasi wafanye maajabu baada ya kuiva,sasa li inchi letu mtu katoka chuo bado amejaa nadharia tu na anaufaulu mkubwa wanataka ajiajiri,ushenzi mtupu
 
Kifupi mleta mada mumbeya tu hajaitaja hiyo GPA ni ya course gani na chuo gani

Nafikiriataluwa wale mafailure vyuoni wenye GPA ya chini akijifariji

Kwenye maisha penda ku perform vizuri popote unapokuwa iwe shuleni chuoni,kazini ,nyumbani nk kama uwezo unao

Kupata GPA ya chini sio sifa .Unatakiwa kila unapopita uache mark ya highest performance
Huo zamani tuliuita USONGO! Ni ujinga fulani uliokuwa umetuingia vichwani.
Msongo hujikita kusoma tu bila kutengeneza connection, markert demand nk.
Unasoma soma tu ili ufaulu halafu ulichokisoma hakiitajiki sokoni, huo ufaulu unakuwa na maana gani?
Ufaulu mkubwa wa sasa uendane na mahitaji ya soko. Mfano wewe una GPA 5. ya BA in history na mwenzio ana ufaulu wa Finance au Data science unafikiri ufaulu upi utafaa mtaani hapo? Je yupi atabaki anazurura kama mbuzi wa uswahili ?
 
Kuna baadhi ya kampuni na hata zingine zinazotoa graduate trainee programs chini ya 4.0 GPA sahau kupata maana hata mimi siamini mtu mwenye GPA ya juu ya 4.5 akawa ni mtu asiye na commitment au discipline kwa lolote atakaloligusa. Ila kwa kazi ambazo ni skills based ambazo ndio nyingi mtaani hawawezi kuangalia GPA maana haziwasaidii na kingine hizo kazi zinahitaji creativity na ule uwezo wa mtu natural zaidi kuliko knowledge ambayo mtu anayo kupitia shule

Mfano unahitaji graphic designer, marketing or IT person, GPA itaisaidia nini kampuni kama haioni kitu umedeliver ila kama ni reputable company na mmekutana wawili mnaoshabihiana vigezo na mwenzio ana GPA kubwa, hata kama wewe ni HR lazma utampa mwenye GPA
A modern HR professional doesn't rely on GPA when recruiting!
 
Back
Top Bottom