DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Aiseee.

[emoji1666][emoji1666][emoji1666]
 
Dah nchi ngumu sana hii, kuja kuendelea si leo wala kesho, pole sana mkuu
 
Hatua zote muhimu nimezipitia ndiyo sababu niliweza kuonana na dakitari na kupata huduma za awali. Naomba unieleze umuhimu wa hiyo CD kuingizwa kwenye mfumo wa Muhimbili badala ya kuwa ni kati ya mimi na dakitari wangu, mimi si mtu maarufu kiasi hicho cha kuingizwa kwenye kumbukumbu za hosipitali.
 
Komaa.:
1. Hospitali haina jukumu la kufatilia majibu ulopewa ulete. Ni wajibu wako.
2. Huruhusiwi kutoa taarifa kwa wasiohusika. Na inaonekana alifanya hilo. Bora angekiri kwamba kiutunduutundu alitaka kuona kilichomo.
Niliposema kasahau ni wapi? Na kama kasahau,kasahau kwake haijabaki sospitali.
Wauguzi hawana uelewa. Hospitali nzima walikosa mtu wa kuwaelekeza?
Jeuri zenu ndo zinazopelekea matatizo kama hayo. Kikubwa narudia,humu kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kumsaidia akapata tiba,ila kama kibri bado kipo pale pale,nenda kamsaidie
 
Ishu ni kwamba kwanini DAKTARI asiweze ku_upload yeye mpk Mgonjwa aende kwa mtu wa ICT?

Kingine.. unavyosema ufinyu wa Mtandao unamaanisha nini exactly..?
 
X-ray na CT scan vyote vinaonesha kinachoendelea ndani ya mwili wako na vinawekwa kwenye mfumo wa picha ili dakitari aone, sasa kwanini nilipie kiasi hicho cha fedha huku lengo la kulipia kufanya ct-scan ni kumuwezesha dakitari aone kinachoendelea ndani ya mwili wangu, hiyo sh 86,000/= ninalipia nini tena?
 
Ishu ni kwamba kwanini DAKTARI asiweze ku_upload yeye mpk Mgonjwa aende kwa mtu wa ICT?

Kingine.. unavyosema ufinyu wa Mtandao unamaanisha nini exactly..?
Mkuu,ni kweli hapa tunaongelea sensitive case na issue,lakini. CD haiwezi kuwa tatizo. Ripoti inayoambatana na CD na yenyewe inatosha. Nadhani wenye uelewa wajitokeze au kama kuna mtu wa Mhimbili kitengo husika,aje hapa atueleze utaratibu huo unatoka wapi
 
Ndo nimeuliza maswali mkuu..
Ulijisajili ulipofika Hospitali nyingine?
Ulilipia pesa ya Consultation?
Kila kitu nimelipia pasi na shaka, ila hilo la kulipia ili iwekwe kwenye mfumo wao kwangu mimi ni nje ya kuhudumiwa.
 
Toka ameondoka mwamba mtetezi wa wanyonge Hali hii ipo karibu Kila sekta serikalini.
 
Kumbee! Hongera! Au unadhani una kinga ya matatizo wewe! Leo kwake kesho kwako.
tatizo letu wabongo hatupendi kuambiwa ukweli.! afuate utaratibu uliowekwa na mamlaka husika apate matibabu.

Leo unakuta mtu analalamika system mbovu wakati uchaguzi ukifika unamkuta polling station na kikofia chake na litisheti likubwa la kile chama cha matapeli, useless 🛃
 
Ndugu zangu hili tunaloongelea hapa linawapata wengi, wapo wanaishia kimya kimya na wengine tumo humu ili tujaribu kujitetea na kuwatetea wasio na sauti kama yule mama mzazi aliyefariki Handeni.
 
Mkuu,mtafute Komredi BASHITE ndio asaidie hilo suala lako,huoni KENGE zinavyomsifia humu kwamba anatatua matatizo ya Wananchi papo kwa papo?au kuna zile KENGE LUCAS MWASHAMBWA, JIDULABAMBASI nk ziambie zikusaidie shida yako?zaidi ya hapo hiyo CD wamelekee Bongo Movie tu
 
Mkuu kuna kitu kimoja unakisahau sana (Samahani kusema hivyo)
Kumbuka Taarifa zako zote za ugonjwa pamoja Na CT-Scan ulopiga zipo Huko Hospitali ya mkoa ulikotoka..

Muhimbili ni hospitali Ya Rufaa Haiwezi kurelly Kwenye Report uliyokuja nayo kutoka Hopitali nyingine hii hairuhusiwi katika Refferal system guildlines..

Kusoma report uliyokuja nayo atasoma Ili kujua Anaanzia wapi kuangalia na nini hasa afanye zaidi ili.kugundua tatizo lako..
Hawezi kuchukua Moja kwa moja Report iliyoandikwa na hospitali Nyingine na yeye akaifanyia kazi bila kufanya na yeye uchunguzi wa vipimo vilivyofanywa ikiwa atarely only kwwnye report ya uchunguzi uliyokuja nayo bila kuangalia CD uliyoleta...

Unfikiri kama Yule Daktari wa Ulikotoka alikosea Kuku-Diagnose na yeye akachkua report yko kama ilivyo Ingekuwepo maana ya Wewe kupewa Rufaa

Umuhimu wa kuingizwa Taarifa zako Kwenye Mfumo wa kimatibabu (HMIS)
Kuingiza Taarifa zako katika mfumo wa kimatibabu ni muhimu sio lazima uwe maarufu kwa sababu kwanza...

  • Inafanya Taarifa zako ziwe more accesible na jopo jingine la madaktari kama Taarifa zako zitabidi zitatuliwe na Wataalamu wa juu zaid kama mabingwa zaidi...hakutakuwa na haja tena ya kwenda kitengo kingine wakuulize maswali ambayo tayari wanayoma kwenye mfumo au kufanya vipimo ambavyo tayari vimeshafnywa
  • kutafanya iwe vyepesi kurejea Taarifa zako za kimatibabu pale ambapo Utapata tatizo jingine na ili wajue jinsi ya kukusaidia ensapo tatizo jipya linaweza kuwa ni chanzo kutoka tatizo la zamani
  • mambo ya legas cases pia
  • ziko nyingi sana ila ni muhimu taarufa kutunzwa kwa ajili ya marejeo ya baadae
NB: kumbukumbu za Hospitali hawaingizwi maarufu tu ni kwa sababu ya Taarifa za kimatibabu kwa ajili na kwa ajili ya ofisi...

Nakupa scenario chukulia Umetibiwa Muhimbiri miaka Mitatu ilopita lets say Kisukari na ukawa unatumia Dawa aina fulani ambazo ulipewa umetumia dawa kwa muda mrefu na una Mzio (Allgy ) na dawa fulani ukitumia unazidiwa..
BAada ya miak miwili umepelekwa ukiwa umepata ajali n hujitambui unafikiri zile Taarifa zilizowekwa hazitakufaa kuchagua aina ya matibabu Utakayopewa?
 
Pole sana mkuu, hii ndio ccm, iyena iyena nyigiiiiiii wizi kila kona
 
Ulichokiandika hapa umesoma vizuri maelezo yangu yote? Kama umesoma sema nilipokosea ni wapi.
Kwa kifupi CD na tipoti ya maandishi kuhusu kinachoonekana kwenye picha nimewasilisha na malipo muhimu nimelipa.
 
Mbona CD dakitari ameweza kuifungua, kwahiyo unanishauri nipige picha hapo nyingine ya x-ray na ct-scan!
 
Daktari aliyeitisha vipimo huko ulikotoka ndo alitakiwa aandike ripoti ya kilichoonekana ili uende nayo huko muhimbili, daktari wa muhimbili anaweza kuamua kutoa matibabu kwa kuzingatia ripoti uliyokuja nayo au akaamua kufanya vipimo upya.......hilo la kusoma CD au vipimo ambavyo hajaagiza yeye vifanyike sidhani kama huwa wanakuwa radhi kwa hilo.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…