Habari Njema; Nimeidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kutoa Elimu ya Fedha

Rafiki yangu mpendwa,

Nimekuwa napenda utajiri tangu nikiwa mtoto mdogo.

Nakumbuka niliwahi kumwambia mama yangu kwamba kwenye maisha yangu lazima nitakuwa tajiri. Alicheka na kuniambia ni utoto tu unanisumbua.

Nikiwa shuleni nilifuata vizuri ile kanuni maarufu ya NENDA SHULE, SOMA KWA BIDII, FAULU, UTAPATA KAZI NA KUWA NA MAISHA MAZURI.

Lakini katika kufuata hiyo kanuni, tangu naanza darasa la kwanza mpaka nafika chuo kikuu, sikuwahi kufundishwa chochote kuhusu usimamizi wa fedha binafsi.

Baada ya kutoka kwenye mfumo wa elimu na kuingia mtaani, ndiyo niliona ombwe kubwa lililopo kwenye eneo la USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI (PERSONAL FINANCE MANAGEMENT).

photo_2024-06-08_11-57-47-2-1-1024x768.jpg

Hilo lilinisukuma mimi binafsi kuanza kujifunza peke yangu kuhusu eneo hilo la fedha binafsi. Nilisome vitabu vingi vya fedha, utajiri na uhuru wa kifedha. Vitabu hivyo vilinifungua sana ufahamu wangu kwenye eneo la fedha.

Vitabu vitatu vilivyonifungua sana ni THINK AND GROW RICH, THE RICHEST MAN IN BABYLON na RICH DAD POOR DAD. Mwaka 2012 niliamua rasmi kwamba nitaweka kwenye matendo yale yote ninayojifunza kwenye vitabu hivyo.

Tangu mwaka 2013 nimekuwa najifunza na kufanya uwekezaji kwa vitendo, kitu ambacho kimekuwa kinanipa manufaa makubwa.

Kwa sababu nimekuwa naandika na kufundisha, nimekuwa pia nikiandikia na kufundisha eneo la fedha binafsi. Pamoja na fursa nyingi za uwekezaji na kujenga utajiri zinazopatikana Tanzania, bado watu wengi hawanufaiki nazo.

Hilo ndiyo limekuwa linanisukuma kushirikisha maarifa haya ya fedha na utajiri kwa watu wengi zaidi. Pamoja na kufanya hilo kwa nia kubwa, bado watu wengi wamekuwa siyo waelewa, wakiwa hawaamini kama yale ninayofundisha yanaweza kufanya kazi kwao.

Benki Kuu Ya Tanzania (BOT) wakiwa kama watu wenye dhamana ya usimamizi wa fedha hapa Tanzania, wameona ombwe kubwa lililopo kwenye uelewa wa fedha kwa wananchi.

Kumekuwa na harakati za serikali kuingiza somo la usimamizi wa fedha binafsi kwenye mtaala wa elimu. Maboresho ya mtaala wa sasa yanaleta elimu ya fedha kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.

Pamoja na hatua hizo, ilionekana wazi kuna kundi kubwa la watu ambao hawapo kwenye mfumo wa elimu. Kundi hilo linahitaji kupata elimu sahihi ya fedha ili kuwa na maisha bora.

Na hapo ndipo BOT ilipokuja na programu ya mafunzo kwa watoaji wa elimu ya fedha na kuwaidhinisha ili wakatoe elimu ya fedha kwa umma. BOT wameweza kuandaa na kuendesha mafunzo hayo ya watoa elimu ya fedha na kuwatunuku vyeti vya CERTIFIED FINANCIAL EDUCATORS.

photo_2024-06-08_12-02-41.jpg

Ninayo furaha kukujulisha kwamba mimi Kocha wako, Amani Emanuel Makirita ni mmoja wa kundi la kwanza kabisa kupate elimu hii. Hivyo sasa nimethibitishwa kuwa mtoaji wa elimu ya fedha.

Rafiki, nimekuwa nafundisha na kufanya hayo kwa vitendo kwa miaka zaidi ya 10 sasa. Kupata uthibitisho huu inanipa mimi fursa ya kuendelea kufanya kwa upana zaidi na kuaminika na wengi.

Hivyo nikukaribishe tuendelee kushirikishana elimu hii na kufanyia kazi ili kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha.

Kwa sasa elimu ya fedha ninayotoa inasimamia maeneo matano muhimu;

1. Kuwa na njia halali ya kuingiza kipato cha uhakika.

2. Kudhibiti matumizi yasizidi kipato.

3. Kuondoka kwenye madeni binafsi.

4. Kuwa na akiba kwa ajili ya dharura na mipango ya maendeleo.

5. Kufanya uwekezaji kwa ajili ya uhuru wa baadaye.

photo_2024-06-08_12-03-39-576x1024.jpg

Pia nafundisha na kusimamia njia kuu mbili za kujenga utajiri.

Ya kwanza ni njia ya MWENDO POLE, hii inahusisha kuwekeza asilimia 10 ya kipato kwa muda mrefu. Njia hii inachukua miaka 20 mpaka 30 kujenga utajiri.

Njia ya pili ni ya MWENDO KASI, hii inahusisha kuwekeza asilimia 50 ya kipato kwa muda mfupi. Njia hii inachukua miaka 10 mpaka 15 kujenga utajiri.

Katika kuhakikisha unapata elimu hii na kunufaika, nina programu kuu mbili;

Moja ni NGUVU YA BUKU, hii ni programu ya bure kabisa ambapo unapata mafunzo na usimamizi wa kujenga utajiri.

Mbili ni UHURU WA KIFEDHA, hii ni programu ya kulipia ambapo unasimamiwa kufikia uhuru wa kifedha kama ulivyopanga.

Kupata mafunzo na huduma hizi, tuwasiliane kwa namba 0678 977 007.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua hayo kwa kina na hatua za kuchukua ili uweze kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha. Karibu ujifunze na kuchukua hatua.

View: https://youtu.be/iEbOi5pDQ44

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.

Ni muhimu kutoka elimu hiyo,ingawa ni ngumu kwa tulio wengine kutakeleza hayo.Nitajitahidi.
 
Tupe somo namna ya kujenga kipato kwa kutumia Bond za Benk kuu, naamini zile ni hela rahisi kwa mwekezaji anayeanza
 
Sio hela rahis kama unavyozan...kule ukiwekeza pakubwa zaid faida utaiona tu nzuri..lakin mzigo wa kutosha...mbona zipo taasisi nyingi tu unaweza invest mdogo mdogo na ukatoboa..mfano crdb mwaka huu dividends imekuwa Tsh 50..kias fulan imeongezeka na hisa zake sio gharama...Nmb kule hisa moja haizid 5,000 na gawio linapanda waza longrun target hutajuta
 
bond za BOT zinalipa mpaka 15% for 25 years, nafikiri ni easy money kwa kiasi fulani
 
Haya kwa mfano pale minimum ni 1,000,000 na addition ya 100,000 as par face au value na pale bonds zinakuwa matuared kwa vipindi 6..,kwa miaka 2, 5,7, 10, 15 na 20...fanya calculation kwa investment ya one milion kwa miaka 15 mpaka 20 na percent ya 15..
 
Mkuu,
Sitakupa namba zangu, lakini nataka nikupe ushahidi wa karibu.
Mwaka 2014, karibu miaka 10 imepita, niliweka hapa bandiko la kujenga utajiri kwa kuanza na shilingi elfu 1.
Nikuambie tu kwamba nimeliishi andiko lile na nimeweza kufanya kaisi kikubwa cha uwekezaji. Japo sitakupa namba hapa hata ufanye nini.
Ila elewa nimeishi hilo kwa miaka 10 na ninajiamini kuweza kumwelekeza mwingine afanye kama nilivyofanya.

Andiko liko hapa; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja
Hakuna namna hiyo idea yako inaweza fanya kazi katika ulimwengu halisiwa nje ya makaratasi
 
Jambo zuri sana. Elimu ya masuala ya uchumi binafsi inapaswa kutolewa sana. Hasa mashuleni. Sisi(App ya Maktaba Sauti) huwa tunafasiri vitabu. Watu wanatuuliziaga sana vitabu vya Dr. Amani.

Moja ya kitabu chetu kinachopendwa sana ni Tajiri wa Babeli(The Richest Man in Babylon). Hiki kinafaa sana juu ya elimu ya uchumi binafsi.

Tajiri wa Babeli-Tiba saba dhidi ya pochi tupu.
 
Rafiki yangu mpendwa,

Nimekuwa napenda utajiri tangu nikiwa mtoto mdogo.

Nakumbuka niliwahi kumwambia mama yangu kwamba kwenye maisha yangu lazima nitakuwa tajiri. Alicheka na kuniambia ni utoto tu unanisumbua.

Nikiwa shuleni nilifuata vizuri ile kanuni maarufu ya NENDA SHULE, SOMA KWA BIDII, FAULU, UTAPATA KAZI NA KUWA NA MAISHA MAZURI.

Lakini katika kufuata hiyo kanuni, tangu naanza darasa la kwanza mpaka nafika chuo kikuu, sikuwahi kufundishwa chochote kuhusu usimamizi wa fedha binafsi.

Baada ya kutoka kwenye mfumo wa elimu na kuingia mtaani, ndiyo niliona ombwe kubwa lililopo kwenye eneo la USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI (PERSONAL FINANCE MANAGEMENT).

photo_2024-06-08_11-57-47-2-1-1024x768.jpg

Hilo lilinisukuma mimi binafsi kuanza kujifunza peke yangu kuhusu eneo hilo la fedha binafsi. Nilisome vitabu vingi vya fedha, utajiri na uhuru wa kifedha. Vitabu hivyo vilinifungua sana ufahamu wangu kwenye eneo la fedha.

Vitabu vitatu vilivyonifungua sana ni THINK AND GROW RICH, THE RICHEST MAN IN BABYLON na RICH DAD POOR DAD. Mwaka 2012 niliamua rasmi kwamba nitaweka kwenye matendo yale yote ninayojifunza kwenye vitabu hivyo.

Tangu mwaka 2013 nimekuwa najifunza na kufanya uwekezaji kwa vitendo, kitu ambacho kimekuwa kinanipa manufaa makubwa.

Kwa sababu nimekuwa naandika na kufundisha, nimekuwa pia nikiandikia na kufundisha eneo la fedha binafsi. Pamoja na fursa nyingi za uwekezaji na kujenga utajiri zinazopatikana Tanzania, bado watu wengi hawanufaiki nazo.

Hilo ndiyo limekuwa linanisukuma kushirikisha maarifa haya ya fedha na utajiri kwa watu wengi zaidi. Pamoja na kufanya hilo kwa nia kubwa, bado watu wengi wamekuwa siyo waelewa, wakiwa hawaamini kama yale ninayofundisha yanaweza kufanya kazi kwao.

Benki Kuu Ya Tanzania (BOT) wakiwa kama watu wenye dhamana ya usimamizi wa fedha hapa Tanzania, wameona ombwe kubwa lililopo kwenye uelewa wa fedha kwa wananchi.

Kumekuwa na harakati za serikali kuingiza somo la usimamizi wa fedha binafsi kwenye mtaala wa elimu. Maboresho ya mtaala wa sasa yanaleta elimu ya fedha kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.

Pamoja na hatua hizo, ilionekana wazi kuna kundi kubwa la watu ambao hawapo kwenye mfumo wa elimu. Kundi hilo linahitaji kupata elimu sahihi ya fedha ili kuwa na maisha bora.

Na hapo ndipo BOT ilipokuja na programu ya mafunzo kwa watoaji wa elimu ya fedha na kuwaidhinisha ili wakatoe elimu ya fedha kwa umma. BOT wameweza kuandaa na kuendesha mafunzo hayo ya watoa elimu ya fedha na kuwatunuku vyeti vya CERTIFIED FINANCIAL EDUCATORS.

photo_2024-06-08_12-02-41.jpg

Ninayo furaha kukujulisha kwamba mimi Kocha wako, Amani Emanuel Makirita ni mmoja wa kundi la kwanza kabisa kupate elimu hii. Hivyo sasa nimethibitishwa kuwa mtoaji wa elimu ya fedha.

Rafiki, nimekuwa nafundisha na kufanya hayo kwa vitendo kwa miaka zaidi ya 10 sasa. Kupata uthibitisho huu inanipa mimi fursa ya kuendelea kufanya kwa upana zaidi na kuaminika na wengi.

Hivyo nikukaribishe tuendelee kushirikishana elimu hii na kufanyia kazi ili kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha.

Kwa sasa elimu ya fedha ninayotoa inasimamia maeneo matano muhimu;

1. Kuwa na njia halali ya kuingiza kipato cha uhakika.

2. Kudhibiti matumizi yasizidi kipato.

3. Kuondoka kwenye madeni binafsi.

4. Kuwa na akiba kwa ajili ya dharura na mipango ya maendeleo.

5. Kufanya uwekezaji kwa ajili ya uhuru wa baadaye.

photo_2024-06-08_12-03-39-576x1024.jpg

Pia nafundisha na kusimamia njia kuu mbili za kujenga utajiri.​

Ya kwanza ni njia ya MWENDO POLE, hii inahusisha kuwekeza asilimia 10 ya kipato kwa muda mrefu. Njia hii inachukua miaka 20 mpaka 30 kujenga utajiri.

Njia ya pili ni ya MWENDO KASI, hii inahusisha kuwekeza asilimia 50 ya kipato kwa muda mfupi. Njia hii inachukua miaka 10 mpaka 15 kujenga utajiri.

Katika kuhakikisha unapata elimu hii na kunufaika, nina programu kuu mbili;

Moja ni NGUVU YA BUKU, hii ni programu ya bure kabisa ambapo unapata mafunzo na usimamizi wa kujenga utajiri.

Mbili ni UHURU WA KIFEDHA, hii ni programu ya kulipia ambapo unasimamiwa kufikia uhuru wa kifedha kama ulivyopanga.

Kupata mafunzo na huduma hizi, tuwasiliane kwa namba 0678 977 007.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua hayo kwa kina na hatua za kuchukua ili uweze kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha. Karibu ujifunze na kuchukua hatua.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.
We akaunti yako ina kiasi gani hadi sasa?
 
Back
Top Bottom