Habari Njema; Nimeidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kutoa Elimu ya Fedha

Habari Njema; Nimeidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kutoa Elimu ya Fedha

Why easy money,Ukae na hela yangu for 25 years unipe 15%. ?

Inflation ni 4.6 to 6 kwa mwaka. Mnaakili nyie?
15% ni Kila mwaka na unaweza kuuza bond yako anytime ukitaka, biashara chache sana Kwa bongo za kukupa 15% net profit, hata Kwa hiyo inflation rate & taxes bado utakuwa net on green, wala usiwe na wasiwasi tumezungukwa na nchi nyingi kuanzia Zambia,Kenya, Uganda etc kama wewe ni hustler wa bond market hizo nchi zote zina top 20% Kwa 10 years, lakini angalia sana taxes na inflation rates, wahindi na wachina ndio biashara yao kubwa sana sasa Africa, hizi serikali zetu ni ovyo lakini likija swala la kulipa hizi security wako vizuri sana
 
labda uwe na mtaji kaka but siwezi chimbia milion 10 kwa mwaka kupata 1.5 net achilia inflation kodi
 
Rafiki yangu mpendwa,

Nimekuwa napenda utajiri tangu nikiwa mtoto mdogo.

Nakumbuka niliwahi kumwambia mama yangu kwamba kwenye maisha yangu lazima nitakuwa tajiri. Alicheka na kuniambia ni utoto tu unanisumbua.

Nikiwa shuleni nilifuata vizuri ile kanuni maarufu ya NENDA SHULE, SOMA KWA BIDII, FAULU, UTAPATA KAZI NA KUWA NA MAISHA MAZURI.

Lakini katika kufuata hiyo kanuni, tangu naanza darasa la kwanza mpaka nafika chuo kikuu, sikuwahi kufundishwa chochote kuhusu usimamizi wa fedha binafsi.

Baada ya kutoka kwenye mfumo wa elimu na kuingia mtaani, ndiyo niliona ombwe kubwa lililopo kwenye eneo la USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI (PERSONAL FINANCE MANAGEMENT).

photo_2024-06-08_11-57-47-2-1-1024x768.jpg

Hilo lilinisukuma mimi binafsi kuanza kujifunza peke yangu kuhusu eneo hilo la fedha binafsi. Nilisome vitabu vingi vya fedha, utajiri na uhuru wa kifedha. Vitabu hivyo vilinifungua sana ufahamu wangu kwenye eneo la fedha.

Vitabu vitatu vilivyonifungua sana ni THINK AND GROW RICH, THE RICHEST MAN IN BABYLON na RICH DAD POOR DAD. Mwaka 2012 niliamua rasmi kwamba nitaweka kwenye matendo yale yote ninayojifunza kwenye vitabu hivyo.

Tangu mwaka 2013 nimekuwa najifunza na kufanya uwekezaji kwa vitendo, kitu ambacho kimekuwa kinanipa manufaa makubwa.

Kwa sababu nimekuwa naandika na kufundisha, nimekuwa pia nikiandikia na kufundisha eneo la fedha binafsi. Pamoja na fursa nyingi za uwekezaji na kujenga utajiri zinazopatikana Tanzania, bado watu wengi hawanufaiki nazo.

Hilo ndiyo limekuwa linanisukuma kushirikisha maarifa haya ya fedha na utajiri kwa watu wengi zaidi. Pamoja na kufanya hilo kwa nia kubwa, bado watu wengi wamekuwa siyo waelewa, wakiwa hawaamini kama yale ninayofundisha yanaweza kufanya kazi kwao.

Benki Kuu Ya Tanzania (BOT) wakiwa kama watu wenye dhamana ya usimamizi wa fedha hapa Tanzania, wameona ombwe kubwa lililopo kwenye uelewa wa fedha kwa wananchi.

Kumekuwa na harakati za serikali kuingiza somo la usimamizi wa fedha binafsi kwenye mtaala wa elimu. Maboresho ya mtaala wa sasa yanaleta elimu ya fedha kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.

Pamoja na hatua hizo, ilionekana wazi kuna kundi kubwa la watu ambao hawapo kwenye mfumo wa elimu. Kundi hilo linahitaji kupata elimu sahihi ya fedha ili kuwa na maisha bora.

Na hapo ndipo BOT ilipokuja na programu ya mafunzo kwa watoaji wa elimu ya fedha na kuwaidhinisha ili wakatoe elimu ya fedha kwa umma. BOT wameweza kuandaa na kuendesha mafunzo hayo ya watoa elimu ya fedha na kuwatunuku vyeti vya CERTIFIED FINANCIAL EDUCATORS.

photo_2024-06-08_12-02-41.jpg

Ninayo furaha kukujulisha kwamba mimi Kocha wako, Amani Emanuel Makirita ni mmoja wa kundi la kwanza kabisa kupate elimu hii. Hivyo sasa nimethibitishwa kuwa mtoaji wa elimu ya fedha.

Rafiki, nimekuwa nafundisha na kufanya hayo kwa vitendo kwa miaka zaidi ya 10 sasa. Kupata uthibitisho huu inanipa mimi fursa ya kuendelea kufanya kwa upana zaidi na kuaminika na wengi.

Hivyo nikukaribishe tuendelee kushirikishana elimu hii na kufanyia kazi ili kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha.

Kwa sasa elimu ya fedha ninayotoa inasimamia maeneo matano muhimu;

1. Kuwa na njia halali ya kuingiza kipato cha uhakika.

2. Kudhibiti matumizi yasizidi kipato.

3. Kuondoka kwenye madeni binafsi.

4. Kuwa na akiba kwa ajili ya dharura na mipango ya maendeleo.

5. Kufanya uwekezaji kwa ajili ya uhuru wa baadaye.

photo_2024-06-08_12-03-39-576x1024.jpg

Pia nafundisha na kusimamia njia kuu mbili za kujenga utajiri.​


Ya kwanza ni njia ya MWENDO POLE, hii inahusisha kuwekeza asilimia 10 ya kipato kwa muda mrefu. Njia hii inachukua miaka 20 mpaka 30 kujenga utajiri.


Njia ya pili ni ya MWENDO KASI, hii inahusisha kuwekeza asilimia 50 ya kipato kwa muda mfupi. Njia hii inachukua miaka 10 mpaka 15 kujenga utajiri.

Katika kuhakikisha unapata elimu hii na kunufaika, nina programu kuu mbili;

Moja ni NGUVU YA BUKU, hii ni programu ya bure kabisa ambapo unapata mafunzo na usimamizi wa kujenga utajiri.

Mbili ni UHURU WA KIFEDHA, hii ni programu ya kulipia ambapo unasimamiwa kufikia uhuru wa kifedha kama ulivyopanga.

Kupata mafunzo na huduma hizi, tuwasiliane kwa namba 0678 977 007.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua hayo kwa kina na hatua za kuchukua ili uweze kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha. Karibu ujifunze na kuchukua hatua.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.
✅👏👏👏🙏
 
Mkuu unamjua Andrew tate?

Kama unamjua, mtazamo wako ni upi kuhusu mafunzo yake ya kuupata utajiri?
Ndiyo mkuu, Tate namjua, lakini sijawahi kufuatilia mafunzo yake kwa kina juu ya utajiri.
Hivyo siwezi kucoment vizuri juu ya mafunzo yake.
Kuna watu kama Alex Hormozi ndiyo nimekuwa najifunza zaidi kwao na naona model zao zinafanya kazi vizuri hata huku kwetu.
 
Utakuwa tajiri kwa kuuza vitabu mzee ulivyoviandika...
Wengine wanasaka utajiri kwa kutafuta mali kuzigeuza pesa
Mimi binafsi hakuna mtu anaye weza kunifundisha au kunipa elimu ya kutafuta utajiri,kwa kusoma vitabu vyaje

Ova
Wazee wa kuhamisha magoli,
Mkijibiwa kitu kimoja, mnakimbilia kingine.
Kafie mbali na akili zako za kimasikini.
Utajiri sahihi unaanza na maarifa, kama unayo maarifa sahihi huwezi kucoment upupu kama huu hapa.
Na kama unaweza kucoment upupu kama huu, huwezi kuwa tajiri.
Panga na chagua.
 
tajiri anazaliwa asikudanganye mtu.

unaweza soma hicho kitabu na kuishia kama mhariri tuh
Mkuu, utaniwia radhi lakini hiki ulichoandika hapa ni ugoro mtupu.
Na kama wewe mtu mwenye access ya teknolojia kubwa kiasi cha kuweza kucoment ujinga kama huu, ni hasra sana kwa taifa, maana mkulima masikini asiyekuwa na rasilimali ulizonazo atakuwa na tumaini gani?
Jitathmini mkuu, unakuwa aibu kwa taifa.
 
Kama ningekisoma mapema kile kitabu cha THE RICHEST MAN IN BABYLON pengine ningekuwa mbali zaid ya nilipo..but sio haba...kile kimeakisi sana uhalisia wa hustling kuliko vitabu vingine
Umesema vyema mkuu,
Kile kinabu kinapaswa kuwa requred reading kwa mtu yeyote kabla hajashika pesa yoyote ile.
Lakini hakuna kuchelewa, unapojifunza ndiyo unafanyia kazi.
 
Keep going dude achana kujibizana na Think tank wa Lumumba buku 7 atakupotezea muda bure,
Focus in your dream umejaribu kitu ambacho hata akipewa miaka elfu hata weza,
Hiyo ni Moja ya kipaji ulichobarikiwa mkuu wapuuzi wakikubeza usitetereke!

Shabhashhhh!
Asante sana mkuu kwa maoni haya mazuri ya kutia moyo kwenye hii harakati kubwa niliyonayo.
Hawa nawajua, hawanisumbui, miaka 10 iliyopita niliweka andiko hapa kuhusu kutajirika kwa elfu moja (Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja), walinikatisha tamaa sana, nilifanya, leo miaka 10 baadaye nafurahia na wao bado wanahangaika.
Kwa hiyo kuwajibu hapa ni sehemu tu ya kuchangamsha hii mada iendelee na siyo kwamba nawachukulia serious kiasi hicho.
Asante na karibu sana mkuu.
 
labda uwe na mtaji kaka but siwezi chimbia milion 10 kwa mwaka kupata 1.5 net achilia inflation kodi
Hili ni somo pana mkuu,
Hesabu siyo rahisi kihivyo, kuna vitu vingi hujazingatia hapo.
Lakini hakuna sehemu nzuri ya kukuza utajiri kama uwekezaji, hasa kwenye masoko ya mitaji.
Nitaendelea kutoa hii elimu hapa, fuatilia ili uweze kufunguka na kuchukua hatua sahihi.
 
Kuna mahali nilikusikia kuwa ulipata straight A kwenye PCB. Imekuaje hukuwa Dr?
Ndiyo mkuu,
Nilipata Division one ya point tatu form six, yaani A Physics, A biology na A Chemistry,
Kitaaluma ni daktari wa binadamu, nimehitimu chuo kikuu cha Muhimbili.
Na niko na harakati za kujenga utajiri mkubwa.
Karibu tuambatene pamoja mkuu.
 
Hongera Kaka, nakumbuka for the first time ulinitumia vitabu bure kabisa kupitia emalil yangu.. hii ilikuwa 2015 ambapo nilikuwa bado mwanafunzi wa Chuo Kikuu.

The richest man in babylon, Poor dad.. uendelee kubarikiwa Kiongozi.
Asante sana mkuu kwa mrejesho.
Naamini vitabu vilikusaidia sana.
Karibu uendelee kupata elimu.
 
Back
Top Bottom