Habari Njema; Nimeidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kutoa Elimu ya Fedha

Haya kaka wacha tupate darasa sie wagumu kuelewa.
 
Asante

Ova
 
S
Sawa sawa lakini kazi ipo ndugu kuwa tajiri au kupatq elimu juu ya jinsi ya matumizi ya pesa haitoshi hata kiduchu hata kuwa na uwezo wa kununua anyway safari njema
 
tajiri anazaliwa asikudanganye mtu.

unaweza soma hicho kitabu na kuishia kama mhariri tuh
Umeshavisoma vingapi vikashindwa kukusaidia?

Warren Buffett ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani, lakini kama isingelikuwa tabia yake ya kujisomea vitabu kwa wingi, labda angekuwa anausikia tu utajiri kwenye TV.

Never underestimate the power of books.
 
mhaririri wa hicho kitabu ni tajiri kwa sasa kwani natumaini kakisoma pia.

alafu kua kama msomi usilete jazba za vijiweni
 
hujanielewa bado

sijasema vitabu havisaidi lahasha bali si kusoma kitabu ndio kua tajiri.tajiri anazaliwa na anakua na moyo wa utajiri toka utotoni yani ni natural inborn
 
Watanzania wengi ni wajinga ni watu wa juu juu na ni wapuuzi kifupi huwaga hawajielewi. Stamina ya uwekezaji hawaiwezi. Wengi wamezoea njia za mkato kama wizi na utapeli na majungu pia ni wavivu kusoma na kutafuta maarifa wavumilie ndio jamii uliyonayo

Sehemu pekee wanayoweza kupoteza muda wao kujisomea ni kama kuna mtihani mbele yao baas
 
instagram account yako ni ipi na yotube channel yako ni ipi maana wengine tunapenda kujifunza kwa njia ya video zaidi kuliko kwenye webisite na kama huna tafadhali fungua nimejaribu kutafta insta account yako kupitia jina lako sjafanikiwa kuipata
 
Yeye anafikiri watu wanaishi kwa theories

Ova
Inabidi awe tajiri baadaye ndipo aanze kuchukua watu anawaweka katika biashara zake kabisa ili wanajifunza practically.
Yaani binadamu tunaelewa mno kwa kufanya kitendo kuliko kuambiwa maneno tupu. Mie napenda uwe tajiri ili Sasa uwafundishe watu kwa vitendo utawachukua wanafunzi wafanye field kabisa.

Kuna mfundisha ama mwalimu wa vita namna ya kupigana msituni Kila mtu anaweza akaongea Sasa ingia msituni pigana vita halisi yaani zile risasi kweli zinakupata unakufa na sio kuona kwa simulation tu.
Kila mtu ni bingwa wa kutoa ushauri Ila Sasa nani anaweza akaufanyia kazi ndipo kazi ilipo.

Umepata 50k mara tumekutana mtt mkali wa kihabeshi yaani zile nondo zote zimeisha unawaza tu kulala juu ya kifua cha mtt wa kihabeshi.
Ukishalala hapo unatumia 50k ukavuta ka akiba kingine ndio akili unarudi kukumbuka nondo za vitabuni
 
Kama ningekisoma mapema kile kitabu cha THE RICHEST MAN IN BABYLON pengine ningekuwa mbali zaid ya nilipo..but sio haba...kile kimeakisi sana uhalisia wa hustling kuliko vitabu vingine

Niliwahi andika hapa kwamba natamani kingewekwa kama kitabu Cha lazima hatua ya sekondari na chuo. Kila mhitimu apate Ile Elimu.

Kwangu ni kitabu Bora kuliko vyote nilivyowahi kusoma kuhusu mambo ya fedha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…