Matawi ya juu
JF-Expert Member
- Mar 5, 2019
- 3,504
- 6,809
Kama target ni Kagame, ni very wrong target na hahusiki, propaganda machines za wakabila wa Congo and probably France zimewaharibu akili kabisa , vita itaisha kama Banyamurenge haki zao za kiraia zitakuwa secured pamoja na usalama wao, lakini tatizo kuna makundi mengine karibu 100 yanapigana Congo, na solution ya Uber driver na wenzake singizia Kagame and everything solvedItakuwa bora, mmoja afe mamilioni waishi.
..viongozi wa Sadc wengi wao, kama sio wote, ni urojo-urojo. Ngoja niwakumbushe kilichotokea wakati DRC inavamiwa kwa mara ya kwanza ili kuelewa hicho nilichokisema.
..mwaka 1998 Sadc walituma fact finding team / mission mara baada ya Rwanda kumvamia Kabila Snr.
..kabla hii mission haijarudi kwa viongozi wa SADC kuna General toka Zimbabwe alituma ripoti kwa Mzee Mugabe kuhusu walichokishuhudia kwamba Rwanda na Uganda walikuwa wanaivamia DRC.
..Mzee Mugabe hakuchelewa kusubiri kikao kizima cha SADC kikae na kufanya maamuzi yeye akaamuru Fifth Brigade ya Zimbabwe iende kuzuia mapinduzi dhidi ya Kabila Snr.
..Ndio maana kipindi kile kulikuwa na makelele ya kùmlaumu Mugabe acting in his capacity as Head of Sadc organ on security kwa ku-act unilaterally kutuma majeshi DRC kwa mgongo wa SADC.
..lakini Mzee Mugabe did the right thing. He saved DRC from being taken over by Rwanda na Uganda. Viongozi wengine wa SADC kipindi hicho ama walidanganywa na Rwanda na Uganda, au walikuwa compromised, au walikuwa cowards.
..makosa yaliyofanywa na SADC kutokuungana na kuzungumza kwa sauti moja dhidi ya uvamizi wa Rwanda na Uganda mwaka 1998 ndio chanzo cha mateso haya wanayopitia Wacongomani leo hii. SADC haijaweza kurekebisha makosa na usaliti waliowafanyia Wacongo mwaka 1998.
..kuna article inaeleza vizuri how things unfolded in 1998 nitaeleta hapa JF.
Cc Nguruvi3
DRC wana tatizo la utawala kutokana na kuwakaribishwa ''Rwanda' wakati wa kumuondoa Mobutu.
Jeshi la DRC limeingiliwa sana na Wanyarwanda kiasi kwamba mipango yao ipo wazi.
Kuna Kamanda Kaberebe alikuwa kiongozi DRC sasa ni kiongozi Rwanda, think about that
Majeneral wa Jeshi la DRC ni ''alligiance' kwa Rwanda , wakifukuzwa DRC wanakuwa ''M23'' wakiripoti Rwanda
Hapa ndipo tunataka kujua, wanakosa haki gani?1
Isipokuwa kuna Ukweli mchungu Sana kwamba Watu/Raia wengi wa DRC wa kutoka kwenye maeneo hayo ya pembezoni mwa nchi hiyo ikiwamo na Majimbo ya Kivu na Katanga huwa wanahesabika Kama Raia wa Daraja Pili au raia wa Daraja la mwisho kabisa kwenye nchi hiyo.
Wanojitambulisha kama Watutsi ni wao wenyewe . Hatakujua jina la Banyamulenge!Kuna tatizo la Siasa za Ubaguzi kwa Watu wa maeneo hayo ya Mashariki mwa nchi hiyo ya DRC na kuwapendelea zaidi Watu wengine wa kutoka katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Watu wengi wa Mashariki mwa DRC kwa kiasi kikubwa Sana wanahesabika Kama siyo WaCongoman, hiki ndio chanzo kikubwa Sana Cha kuwepo kwa huo Mgogoro usiokoma, ukiachana na vyanzo vingine kama vile kuwepo kwa rasilimali nyingi sana za madini ya vito, udhaifu wa Jeshi la DRC, Udhaifu wa Utawala wa nchi hiyo ya DRC, n.k..
Hii ni '' deja vu'' . Tumeishi na kuona mengi sana. Tuliambiwa UNITA wanapendwa sana kule Kabinda.2. Siyo rahisi hata kidogo kulipiga na kulifurusha Jeshi la M23 kwa sababu nyingi sana. Mathalani, Watu/Wananchi wengi Sana waishio kwenye maeneo hayo ya Kivu wanawaunga mkono Wapinzani wa Utawala wa nchi hiyo ya DRC, M23 wanaungwa mkono na Wananchi.
I agreeBad enough, hata Jeshi la nchi hiyo nalo pia ni dhaifu Sana, na pia kuna Mawakala wengi Sana wa M23 ndani ya Serikali na ndani ya Jeshi la Serikali ya DRC.
Huwezi kuilamu Tanzania kwasababu ilipokea watu zaidi ya milioni 2 kutoka maeneo ya Vita.3. Kwa bahati mbaya sana, hata hapa nchini Tanzania, Watu wengi wa kutoka katika mikoa ya pembezoni mwa nchi kama vile Mkoa wa Kigoma, pia wamekuwa wakichukuliwa kama ni 'Wakimbizi.' Tatizo hili lipo sana katika nchi hii, Mimi binafsi nimewahi kushuhudia mara nyingi sana mambo ya namna hii. Kuna ' bad sentiment' miongoni mwa Watu kuwaona Watu wa kutoka Kigoma kuwa ni Wakimbizi kutoka katika nchi za jirani, tatizo hili lipo katika Jamii zetu za Tanzania.
Hawawezi kuwafukuza hao wanyarwanda jeshini kama kuna ulazima huo, kwanini wanakubali kukaa na mamluki? Tangu mwanzo wanaonekana M23 wanapata full support kutoka Rwanda, kuna kigugumizi gani kuwabembeleza, wapigwe wote, M23, na Rwanda akitaka apigwe tupate utulivu.Zitto Kabwe Ruyagwa aliulizwa na hakuweza kujibu. Ikiwa ni Raia wa DRC ni kitu gani wanadhani hawatendewi haki, hakuna mahali wanaeleza. Ndiyo maana naogopa sana huu mzozo kwasababu M23 wakifanikiwa ipo siku wale wa Kigoma wenye asili za huko DRC na Rwanda wataanza madai kama hayo
DRC wana tatizo la utawala kutokana na kuwakaribishwa ''Rwanda' wakati wa kumuondoa Mobutu.
Jeshi la DRC limeingiliwa sana na Wanyarwanda kiasi kwamba mipango yao ipo wazi.
Kuna Kamanda Kaberebe alikuwa kiongozi DRC sasa ni kiongozi Rwanda, think about that
Majeneral wa Jeshi la DRC ni ''alligiance' kwa Rwanda , wakifukuzwa DRC wanakuwa ''M23'' wakiripoti Rwanda
Ni haki gani m23 wanazozikosa kwa sasa mpaka wamue kushika mitutu?Another BS propaganda and nobody cares anymore,wapenda maendeleo na haki, M23 hawarudi nyuma. Ukabila , haki za uraia na usalama haviwezi kumalizwa kwa majadiliano na wakabila
Serious question or umeamua kujitoa akili tuu?Ni haki gani m23 wanazozikosa kwa sasa mpaka wamue kushika mitutu?
Aliwaambia wananchi wake kuwa "adui wengine ni Maputo yaliyojaa upepo, unahitaji sindano tu"!!!PK huwa anadharau vikao vya usuluhishi, leo katua Dar nadhani ni kutokana na vipigo.
Walisha infiltrate sana katika mifumo ya DRC kiasi kwamba ni ngumu kuwajuaHawawezi kuwafukuza hao wanyarwanda jeshini kama kuna ulazima huo, kwanini wanakubali kukaa na mamluki? Tangu mwanzo wanaonekana M23 wanapata full support kutoka Rwanda, kuna kigugumizi gani kuwabembeleza, wapigwe wote, M23, na Rwanda akitaka apigwe tupate utulivu.
Hizo ndo haki wanazozikosa?Serious question or umeamua kujitoa akili tuu?
Alimaanisha nini hapa!Aliwaambia wananchi wake kuwa "adui wengine ni Maputo yaliyojaa upepo, unahitaji sindano tu"!!!
Mkuu, msaada tutani, hivi ni nini kilisababisha wimbi la kwanza la wakimbizi wa kinyarwanda miaka ya 60 na 70?Usidhani M23 wataishia DRC, wakimalizana na DRC watahamia Tanzania!
Hii ni expansion ya Himaya!
SADC ina viongozi wapaka makeups..majeshi ya Tanzania, Malawi, na South Africa, yamekutwa flat footed, ndio maana wamepoteza maeneo na ngome zao.
..jeshi la Congo, pamoja na wanamgambo wao, wameonyesha utovu wa nidhamu, na uwezo wa mdogo, katika uwanja wa mapambano.
..pia nchi za SADC hazijaonyesha nia ya dhati kwa kutoa vifaa na askari wa kutosha kuitetea DRC. Mazingira hayo ndiyo yaliyopelekea M23 na Rwanda kujiamini na kushambulia ngome za nchi za SADC.
..DRC na SADC wasipokuwa makini msishangae M23 na Rwanda wakafika Kinshasa.
NB:
..nahisi SADC ya miaka hii imepungukiwa viongozi wenye mioyo ya kishujaa kama Julius Nyerere, Samora Machel, Robert Mugabe, au Sam Nujoma.
Cc Nguruvi3
Mkuu Historia haijawahi kuwa nzuri kwa Rwanda na Burundi. Haikuanza miaka ya 60 na 70, ilianza nyuma ya 1957. Ugomvi wa Watutsi na Wahutu una mizizi ingawa siku hizi wanasema ni ''social class'' kwamba Mhutu anaweza kuwa Mtutsi au vice versa kutokana na Utajiri, sikubaliani na dhana hiiMkuu, msaada tutani, hivi ni nini kilisababisha wimbi la kwanza la wakimbizi wa kinyarwanda miaka ya 60 na 70?
Ukisema kuna halafu ukashindwa kumtaja jina hiyo inakuwa hearsay ama haoxWalisha infiltrate sana katika mifumo ya DRC kiasi kwamba ni ngumu kuwajua
Katika jeshi, wana siri zote za ulinzi na hapo ndipo tatizo lilipo.
Watu kama Kabarebe walishirikishwa serikali kwasababu waliaminiwa wanatoka mashariki ya DRC ili kuondoa hisia za kwamba eneo hilo linatengwa. Hawa akina Kabarebe ni Wazaliwa wa DRC au Raia kwa miaka mingi. Ghafla tunawaona ni viongozi wa serikali ya PK!
Banyamulenge ambao ni Wanyarwanda hata aliyezaliwa DRC mwaka 1920 bado ana link na Rwanda
CDF General J.J. Nkunda aliposema '' kuna watu wasio Rais wamepewa nafasi za maamuzi'' hayo ni kwasababu kama hizi, kwamba, utawaona ni Watanzania lakini wana link na nchi yao!
Majaluo wa Tz ni Mzawa halisi. Mmakonde ni Mzawa halisi, Mngon ini mzawa halisi. Hawana link
Si kila kabila ni hivyo hasa ya Wahamiaji wa magharibi!
Miaka michache iliyopita kuna Afisa wa Jeshi alikimbia baada ya kuhisiwa, unajua alikwenda wapi! Rwanda
Nimekumbuka jina la Jonas Savimbi, kuna siku asubuhi wakati anaendelea kusumbua niliona mzigo mdogo sana ila wa maana mitaa ya kati nikasema Jonas Savimbi kwisha habari yake, niliwaona pia wageni waliotoka mbali ni njia tu walipita wachache wakiwasindikiza ,je yu wapi Lauraa Nkunda ,Joseph Koni? wa wengine,Hapa ndipo tunataka kujua, wanakosa haki gani?
Wanojitambulisha kama Watutsi ni wao wenyewe . Hatakujua jina la Banyamulenge!
Tanzania tuna makabila 120 wakiwemo Watusi, Wahutu n.k. Jambo moja zuri, ukijitambulisha kwa Kabila hutakuwa utaonekana kituko, at least kabla ya kuja kwa JPM.
Watu wa mashriki DRC wanajitambulisha kwa makabila ya Banyamulenge na si Wacongoman
Pili, udhaifu wa jeshi nimeueleza chanzo chake bandiko kabla ya hili
Tatu, kuhusu rasilimali hicho ndicho chanzo cha Rwanda kuitamani Kivu na Goma !
Hii ni '' deja vu'' . Tumeishi na kuona mengi sana. Tuliambiwa UNITA wanapendwa sana kule Kabinda.
Tena UNITA walikuwa na msaada wa Mataifa makubwa ya magharibi kuzuia influence ya Russia na China kupitia MPLA. Nchi za SADC zilipoamua Savimbi aliondoka. Unajua mipango ilipangwa wapi! Tz
Tuliambiwa RENAMO wanapendwa sana, mwisho wa siku waliamua kuweka silaha chini.
Nguvu likuwa ya SADC
I agree
Huwezi kuilamu Tanzania kwasababu ilipokea watu zaidi ya milioni 2 kutoka maeneo ya Vita.
Kuna watu wanaingia na kujifanya ni Watanzania wakikingiwa vifua na wenzao waliotangulia.
Serikali iliamua kuwatawanya Wakimbizi waliopewa Uraia kuzuia hali hiyo
Tuna makabila ya mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga yenye mbadala Kenya.
Hatujasikia malalamiko! sababu kubwa ni ''stability' katika mipaka kama wa Kenya na TZ
Tuna Wawemba wa Zambia na Wangoni wa Malawi, hatujasikia tatizo! sababu ni stability
Upande wa magharibi lazima tuwe waangalifu, ya M23 yanaweza kutusumbua siku zijazo.
Usidhani M23 wataishia DRC, wakimalizana na DRC watahamia Tanzania!
Hii ni expansion ya Himaya!
Muacheni mzee wa kinyakyusa apumzike Alisha maliza ngwe yake ; iliyobaki hao watutsi kumuota usingizini!Apelekwe Major. General Mwakibolwa akamalize kazi period!
Nope Sio Kweli mkuu. Idadi ya vifo vya Askari wa M23 hamaanishi kwamba M23 are defeated.PK huwa anadharau vikao vya usuluhishi, leo katua Dar nadhani ni kutokana na vipigo.
Tatizo kubwa zaidi lililopo DRC ni kuwepo kwa Utawala dhaifu Sana kupita kiasi na Utawala huo kwa kiasi kikubwa umekosa uungwaji mkono kutoka kwa umma/Wananchi walio wengi zaidi.
Kwa Vita vya Mwaka 1997-1998 huko DRC (Zaire), Viongozi wa SADC walifanya vyema kutokutuma Majeshi yao kwenda vitani huko Zaire kwa sababu Dikteta Mobutu Sese Seko alikuwa haungwi mkono kabisa na Wananchi wake wengi zaidi wa nchi hiyo. Hata Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo ya Zaire walikuwa hawampendi Rais Mobutu Sese Seko.
But all in all, Dikteta Mobutu Sese Seko ana mchango mkubwa sana wa kuwepo kwa machafuko na Vita visivyoisha ndani ya nchi hiyo ya Zaire. Yeye ndiye muasisi Mkuu wa kuwepo kwa Utawala dhaifu Sana nchini DRC, yeye ndiye aliyehusika moja kwa moja katika kulifanya Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo kuwa dhaifu Sana kupindukia kama unavyoliona hivi sasa Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo. Ni Mobutu Sese Seko ndiye aliyeanzisha tatizo hili.
Kumbuka: Hatma ya WaCongoman ipo mikononi mwao wao wenyewe.
Nafikiri ni General Kabarebe ndiye alikuwa Mkuu wa Majeshi (CDF) nchini DR Congo na kisha baadaye alikuwa pia Mkuu wa Majeshi (CDF) nchini Rwanda.
Janga kubwa zaidi la udhaifu wa Jeshi la DRC ulipata nguvu kubwa sana kupitia kwa Mtu huyo.
Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo ya DRC hadi leo hii ni dhaifu Sana kutokana na kuwepo kwa Mamluki wengi sana ambao wanawaunga mkono (M23) Wapinzani wa Utawala wa nchi hiyo ya DRC.