Leo nimesikia audio ikitembea mitandaoni inayodaiwa kuwa imerekodiwa na Manara akimtuhumu kwa mambo mengi Barbara.Inaonekana hawa watu wana mgogoro wa mda mrefu na hawawezi kufanya kazi tena pamoja. Wewe kama mwanasoka unadhani nini kifanyike? Au ni madhara ya Mo kujimilikisha timu kifamilia?🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kwenye audio hyo Manara kaenda mbali zaidi na kumtishia Barabara sijui Barnaba sorry Barbana,duuh Barbara kwamba ataiacha timu kama alivyoikuta.Sasa hapo sijui nani anaondoka nani anabaki.
Povu ruksa nina nguo chafu hapa.
Najaribu kuapload audio husika hapa inazingua
=====
Afisa Habari wa Simba Haji Manara ameamua kumtolea uvivu Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez.
Haji anadai Mtendaji huyo amekuwa akimuandama sana na kumnyima raha muda wote toka ameshika majukumu hayo.
Pia, soma>
Barbara Gonzalez amkwepa Manara, asema focus yake kushinda game ya Jumapili
View attachment 1862918