Haji Manara ni nani hapa Tanzania hadi kuwadhalilisha Askari Magereza na wafungwa bila kuchukuliwa hatua?

Haji Manara ni nani hapa Tanzania hadi kuwadhalilisha Askari Magereza na wafungwa bila kuchukuliwa hatua?

Huo ni UNYANYAPAA LIVE kwa sababu alichosema au kufanya Manara kinaweza kusemwa au kufanywa hata na mtu asiye na ulemavu kwa sababu issue hapo ni attitude!! Sasa nini kimekufanya uone Manara kafanya hayo kwa sababu ya ulemavu wake na sio attitude yake?!
Sure....
 
Atajitokeza alie lie hapa ila watu wanamsagia kunguni mnoo kwenye page za Insta za magereza najua hakukuchi atakua kashalia lia
 
Hawa magereza wanatoa onyo kwetu badala ya kuwaonya wafungwa wenzao.
 
Huyu haji manara mdomo wake ni mchafu anajikuta ana mamlaka ya kumtusi na kumdhalilisha yeyote kama kesi ilikuwa na magereza wafungwa wamefuata nini anasahau naye kesho anaweza kuwa mfungwa.

Na hao kituo cha sheria za haki za binadamu hatusikii wakikemea kitu wafungwa wapo kutumikia makosa yao sasa kama haji kakoromewa na magereza ya nini awadhalilishe na wafungwa

Mtu huyu hastahili huruma kwa ule ulemavu wake achukuliwe hatua tu!

Haji Manara ni nani katika nchi hii!
Haji ni mtundu tu
 
Aombe Mungu sana asiende kuwekwa mahabusu ya magereza hata siku 1. Akitoka huko itakuwa 👋👋 yake.

Mungu amsaidie.
Kwanini itakuwa ni "bye bye" yake ?!!

Kwanini baadhi ya watanzania tuna "mentality" ya kupenda KUONA MAUMIVU na MATESO kwa wengine ?!!

Iwe maumivu ya KIHISIA...
Iwe maumivu ya KIUCHUMI...

Mentalities hizi hazina tofauti na "maneno ya ukakasi" yaliyotolewa katika hilo tukio....na ndio maana kila mtu mwenye NGUVU anataka kuonea walio DHAIFU.....na akiwa na NGUVU kukuzidi basi ujue wewe mpenda KUTUMIA MAGUVU iko siku UTADHALILIKA/KUINGIA UNYONGE ukikutana na MWENYE NGUVU mwingine aliyekuzidi NGUVU.....

#Piga vita tabia hizi mbovu!
#Tujifunze kuipenda Tanzania kwa kuheshimia sisi raia wake!
 
Kwa kweli Hajj anatakiwa kuliomba msamaha Jeshi zima la Magereza. Amewadhalilisha sana na amekosa uungwana. Anawakemea askari na kuwaambia waende kwa wafungwa wenzao? Kwamba askari Magereza pia ni wafungwa? Hivi huyo Manara watu wakiamua kumtukania si atakimbia?
Anatakiwa kidogo afundishwe adabu mshike!
 
Huyu haji manara mdomo wake ni mchafu anajikuta ana mamlaka ya kumtusi na kumdhalilisha yeyote kama kesi ilikuwa na magereza wafungwa wamefuata nini anasahau naye kesho anaweza kuwa mfungwa.

Na hao kituo cha sheria za haki za binadamu hatusikii wakikemea kitu wafungwa wapo kutumikia makosa yao sasa kama haji kakoromewa na magereza ya nini awadhalilishe na wafungwa

Mtu huyu hastahili huruma kwa ule ulemavu wake achukuliwe hatua tu!

Haji Manara ni nani katika nchi hii!

Askari magereza alitoa Amri yeye kama Nani?

Kwani ni Gerezani Pale?
 
Back
Top Bottom