Haji Manara: Paul Makonda ulinilaza Korokoroni, acha dunia izunguke kwenye Mhimili wake

Haji Manara: Paul Makonda ulinilaza Korokoroni, acha dunia izunguke kwenye Mhimili wake

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Salaam Wakuu,

Baada ya Paul Makonda kuwalalamikia Polisi kwamba kuna baadhi ya Askari Polisi wanadhalilisha Jeshi la Polisi sababu wanatumiwa na Matajiri.

Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Klabu ya mpira wa Miguu ya Yanga SC ya Tanzania, amesema atulie tuli kama ananyolewa.

Haji kadai Wakati Makonda akiwa Serikalini, alimlaza Korokoroni bila sababu.

Ipo hivi;
20220312_214011.jpg

Leo Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana jana Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu, imeiagiza Serikali kuchunguza mwenendo wa Jeshi la Polisi baada ya wananchi kupoteza imani na Jeshi hilo.

Inadaiwa Maofisa wa Polisi hawaaminiki na wanaonekana kutenda majukumu yao bila kufuata Mwongozo wao wa kisheria (PGO).

Baada ya taarifa hiyo, Paul Makonda Aliandika hivi;

Naunga Mkono hoja ya Kamati kuu ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la Polisi, wanaolipaka tope jeshi la polisi kwa kuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhurumu mali za watu.

Naomba tuanze na Dar Es Salaam na Mimi Paul Makonda nipo tayari kutoa ushirikiano.

Baada ya kuandika Ujumbe huo, Haji Manara alijibu hivi;
Mimi mwenyewe Ushawahi kuniweka ndani bila kosa kwa kutumia Polisi hao hao unao walaumu leo.

Watu wangapi uliwasweka lockup kwa kutumia cheo chako? Wewe leo wa kuwalaumu Polisi?

Acha waseme wengine na tulia Dunia iendelee kuzunguka katika mhimili wake.

Pia soma;

1). Wananchi kukosa imani na Polisi: CCM yaagiza Jeshi la Polisi lichunguzwe

2). Makonda: Baadhi ya Askari Polisi jijini Dar wanawalinda wafanyabiashara matapeli wanaodhulumu mali za watu

7F9A3A0C-8525-465F-BCFF-436CC6847A44.jpeg
 
Chid benzi aliwahi kumshauri Makonda kwamba aangalie pia na Magereza yaweze kukarabatiwa maana kule yeyote anaweza kwenda. (Sina uhakika kama nilimkariri vizuri Chid)

Wengi tulimpuuza tukajua labda ni bange ndiyo inaongea
 
Sasa naona hawa jamaa wanaitumia hii issue ya kiwanja kutafuta public sympathy of a certain kind.

Kwanza wakili Mgongolwa kujitokeza public kutoa clarification kuhusu mmiliki halali wa kiwanja, nikajiuliza wakili ofisi yake ni mahakamani, huyu Mgongolwa barabarani anatafuta nini? ni politics tu.

Then huyu Manara, muajiriwa wa GSM, anakuja mbio mbio nae anamlaumu Makonda, hapa sitaki unafiki, hata kama Makonda alikuwa na madhambi yake lakini huu mchezo unaochezwa ni wa kishamba.

Kama vipi waende mahakamani, kutafuta uungwaji mkono na mashabiki wao kijanja kwa issue zao private ni mchezo wa kishamba uliopitwa na wakati.
 
Sasa anaetakiwa aende mahakamani ni nani? Anaedai au anaedaiwa? Mshauri makonda aende mahakamani na vielelezo vya kununua ardhi, asijekusema kiwanja cha mamia ya mamilioni "amepewa" bure
Wewe ni wakili wa upande upi?

Nimetoa general view kwa upande wangu sitaki kuwa carried away na mambo private ya watu wengine, kwangu hizo zote ni kelele tu.
 
Kwahio tungojee kwanza wamalizane na Makonda alafu ndio tuanze kuwasema ?

Binafsi nadhani kama ni ubaya (na kama kweli kuna ubaya) basi usemwe regardless....; Ilibidi usemwe then..., na inabidi usemwe now...
 
Back
Top Bottom