Haji Manara: Paul Makonda ulinilaza Korokoroni, acha dunia izunguke kwenye Mhimili wake

Haji Manara: Paul Makonda ulinilaza Korokoroni, acha dunia izunguke kwenye Mhimili wake

Manara yupo kazini.

Mnadhani asipoingilia Ugomvi Wa Bosi wake atalipwaje? Kiufupi ni anatekeleza majukumu yake ili watoto waende Chooni...
 
Jiepushe sana na marafiki wenye tabia za manara.
Mtu huyu siku zote anatabia ya kujipendekeza kwa wenye navyo Kati ya madaraka/pesa siku ukiishiwa anaenda kuungana na maadui zako
Kitakacho kusaidia ili asikumalize ni zile silaha ambazo hukumuonyesha enzi za urafiki wenu na Kama ulimuonyesha silaha zote atakumaliza.
 
Habari za swaumu ndugu zangu,

Ni miezi mitukufu kwa waislam na wakristo kwa kila mmoja kwa imani yake wakitekeleza amri ya mungu ya kufunga kwa kujizuia kula na kunywa kwa kulingana na dini husika.

Kwa siku za karibuni kumekuwa na mgogoro au tofauti kati ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam bwana paul makonda na GSM ambao ni wadhamini wa dar young African ila issue sio huo utofauti bali ni mapokezi ya huo utofauti wao,

Katika hali isiyo ya kawaida yule mhamasishaji wa yanga akaingia king moja kwa moja kupambana na makonda ambaye kipindi yupo SIMBA alikuwa swahiba wake ila mambo yamekuwa tofauti baada ya kuhamia jangwani.

Sasa cha kuahangaza ni kitendo cha manara kupost picha au videos za kumkejeli makonda kupitia social network zake kitu ambacho watu walikipokea tofauti maana mpira na siasa haviendani ila manara hajawahi kukubali kushindwa na makonda vile hajawahi kurudi nyuma.

Manara ataiweza vita iliyomshinda ruge na baadhi ya viongozi wakubwa wa serikali hata kama kwa sasa hayupo madarakani ila bado ni mtu hatari kwenye mambo ya siasa na anajua umafia wote ndani na nje ya serikali ngoja tuone nani ataibuka mshindi japo makonda hajaanza kujibu mashambulizi bado.

Manara ataiweza vita ya makonda ngoja tuone nani mtoto wa mjini manara akipita hapa basi kweli yeye atakuwa mtoto wa mjini.
Machawa siku zote wanakuwa na backup
 
Ila manara ajiangalie sana.mdomo uliponza kichwa.
 
Pamoja na mapungufu ya Makonda bado Haji hapaswi kulibeba kombe la kumnanga.

Hivi unatoa wapi nguvu za kumnamga mtu usiyeijua kesho yake ya kisiasa?!

Haji anayo hakika kwamba Makonda mwisho wake kisiasa umefika?!

Ukweli ni kwamba hawa kina Makonda na Sabaya hata wakifungwa binafsi naamini yupo jamaa yao mmoja atachukua madaraka makubwa na atawapa vyeo tena ama atawanyanyua.

Kwa muktadha huo Haji kuwa na akiba ya maneno.
 
Anahaki ya kuongea na kutoa madukuduku ya moyoni Kama ambavyo katiba ya nchi inamruhusu.

Wengi wangetamani kusema lakini hawana platform za kufikia watu wengi, so muacha aseme Kwa niaba ya watu walioonewa na uongozi wa Makonda.
 
Waache wamalizane Makonda mwenyewe mshenzi tu
 
Anahaki ya kuongea na kutoa madukuduku ya moyoni Kama ambavyo katiba ya nchi inamruhusu.

Wengi wangetamani kusema lakini hawana platform za kufikia watu wengi, so muacha aseme Kwa niaba ya watu walioonewa na uongozi wa Makonda.
Lakini naona kama imekuwa too much kwake ,ana attack Sana
 
Lakini naona kama imekuwa too much kwake ,ana attack Sana
Sometimes yes sometimes no maana siasa bwana haieleweki leo Kinana karudi kazini 🤣🤣.
Jambo la msingi kama wewe sio mwanasiasa kaa mbali na wanasiasa.
 
anayemnyanyua binadamu ni mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu akikunyanyua, unapaswa kuwa na busara nyingi sana na kumfurahisha yeye aliyekunyanyua kupitia matendo yako..
 
ameongea nini... weka kiambatanisho chake manara... una feli wapi kiongozi?
 
Pamoja na mapungufu ya Makonda bado Haji hapaswi kulibeba kombe la kumnanga.

Hivi unatoa wapi nguvu za kumnamga mtu usiyeijua kesho yake ya kisiasa?!

Haji anayo hakika kwamba Makonda mwisho wake kisiasa umefika?!

Ukweli ni kwamba hawa kina Makonda na Sabaya hata wakifungwa binafsi naamini yupo jamaa yao mmoja atachukua madaraka makubwa na atawapa vyeo tena ama atawanyanyua.

Kwa muktadha huo Haji kuwa na akiba ya maneno.

Acha uoga. Mbona wenyewe walitesa watu hadharani?. Usizuie watu kuongea ukweli.
 
Back
Top Bottom