✍️Heshimu watu brother...Cheo, Umaarufu na Pesa huondoka... Sponsors hufa!
📌Ni kweli Paul Makonda alikua na madhaifu mengi tu ya kiuongozi kama walivyo viongozi wengine..
Lakini kabla hujamnyooshea kidole jiulize wewe ukiwa Simba uliwatukana wangapi?
Angekuwepo Magufuli na wewe ukaendelea kubaki Simba ungeyasema haya?
📌Wewe sindio ulisema Yanga wenye akili ni Baba yako na Mzee Kikwete? Uliwaumiza wangapi kwa kauli yako hii?
📌Uliwatukana waandishi wa habari wangapi?
Nakukumbusha baadhi yao Shaffih Dauda,Priscar Kishamba ,Maulid Kitenge na wengine wengi tu.
📌Unadhani bila huruma ya GSM wewe ungekuwa wapi leo?
Unadhani GSM asingekuwepo Yanga, ungefanya kazi Yanga wewe?
📌Leo uko Yanga kila siku kumtukana Mohamed Dewji na Barbara Gonzalez hilo huoni kama ni tatizo?
📌Umewaumiza wangapi kibiashara ukiwa Yanga? Dauda, Clouds,Vunjabei na hata GSM mwenyewe kuna sehemu umemuumiza sana sema hataki kusema tu.
📌Kwanini huo uungwana unaouhubiri usiufanye wewe?
📌Ni kweli inafahamika upo Yanga kwa kazi moja tu ya kuitukana Simba (hasa Mo Dewji) na kuwasifia GSM
📌Ni kweli tunajua bado unaipenda Simba ndio maana hujawahi kuwakejeli wala kuwatukana wachezaji wa Simba ispokuwa Mo Dewji na Barbara Gonzalez waliokuondoa kwenye nafasi yako
📌Lakini, unajiskiaje unapomshambulia na kumtukana mtu kila siku ambaye hakujibu? Imani yako inasemaje?
📌Tatizo lako Brother unataka kila kitu uwe wewe...Yaani Diamond uwe wewe,Samatta uwe wewe, Mayele uwe wewe,Rais uwe wewe,Gharib uwe wewe nk
Unataka ku-trend wewe tu....!!
📌Kabla hujamnyooshea kidole mwenzio angalia hivyo vidole vitatu vinavyokuangalia wewe..
Credit Sospeter Ilagila