Haji Manara: Paul Makonda ulinilaza Korokoroni, acha dunia izunguke kwenye Mhimili wake

Uko sahihi, lakini kusema Bashite alikuwa na madhaifu ya kiuongozi kama viongozi wengine siyo sawa, umerahisisha sana, jamaa alikuwa muuaji, katili na asiyeheshimu viongozi wenzake wala kujali mipaka yake.
 
Ila makonda ni mjinga kweli kweli, yaani anang'ang'ania kiwanja cha mtu mwingine na mtu mwenyewe ana adi 'title deed' ya kiwanja building permit, etc, sijui ameanza kuchanganyikiwa?? au amekosa wana sheria wakumshauri nini cha kufanya??
 
Yaani to be Tanzanian ni umbea, majungu, fitna, uwongo, unafiki kama huna sifa hizi ww sio Mtanzania yaani haina haja kuhusisha watu wa Uhamiaji
 
Manara anapenda kutumia trending events ili akiki, yuko tayari kumlamba miguu current boss ili kumchafua mwingine ambaye anatofautina na boss kimsimamo na kimtazamo

Huyu mtu ni wa kumchunga sana hana trend nzuri, ana mdomo usio kuwa na mipaka

Kwasababu watu wengi hatumpendi makonda kutokana na matumizi ya hovyo ya madaraka aliyokuwa akiyatumia kipindi akiwa bado mkuu wa mkoa.

Haji ametumia hiyo kama fursa ya kujisafisha kwenye tukio lake la October 12, 2018 ambapo alifanya udanganyifu kwa kusambaza taarifa za uwongo kwa madai ya kwamba ametumwa na familia ya MO Dewj kipindi ambacho Mo alikuwa ametekwa.

Kwanza tukio la yeye kuwekwa sello kunyea makasha, halikufanywa na makonda bali ni mambosasa ndiye aliyemkamata na kumtia ndani. Afu hata hakukaa sana ilikuwa ni usiku mmoja tu kesho yake akapewa dhamana akatoka

Ikitokea huyu mambosasa yuko katika situation ambayo hana nguvu ya kicheo na watu ambao alikuwa na utofauti nao wakaanza kumzonga, basi tutamuona manara tena akiliibua hili upya na round hii itakuwa critical zaidi kwasababu huyu ndio alihusika moja kwa moja hadi kumsindikiza sello.
 
ila makonda ni mjinga kweli kweli, yaani anang'ang'ania kiwanja cha mtu mwingine na mtu mwenyewe ana adi 'title deed' ya kiwanja building permit, etc, sijui ameanza kuchanganyikiwa?? au amekosa wana sheria wakumshauri nini cha kufanya??
Ujinga wa Makonda ni wazi. Ila iwe funzo kwa watu wenye tabia kama zake mf.Manara
 
Makonda hawezi safishika kwa lolote kwa jik wala steel waya wala kumloweka kwenye sabuni ya Omo na lile bichwa lilobeba meno tuu.

Nakumbuka alivyokaidi ile alivyokuwa akitwa kanisani kwenye msiba wa Mh. Mengi na suruali zake za jeans................. yaani huyu mtu aombe sana maisha yake yako kama sijui hata nifananishe na nini shenzy kabisa yule... huwa namhurumia yule binti mzuri alieolewa na jitu kama lile mnyama sio mnyama fisi sio fisi... acha aanze kurudisha mali za wenyewe moja baada ya nyingine.

Na jinsi hakuwa na akili kichwa ambacho ni hifadhi ya meno pekee anazozana na mali inayoosha sio yake
 
MAISHA ANAYOISHI MANARA KWENYE ILE APARTMENT YAKE NA FAMILIA YAKE HAYAENDANA NA KIPATO CHAKE, NAE NI WA KUCHUNGUZWA
 
Anza kwanza na unafiki wako alfu uje wa Haji
 
MAISHA ANAYOISHI MANARA KWENYE ILE APARTMENT YAKE NA FAMILIA YAKE HAYAENDANA NA KIPATO CHAKE, NAE NI WA KUCHUNGUZWA
Ana ofisi inayijihusisha na maswala ya media.

Mwezi uliopita alitangaza nafasi za kazi.
 
Umesema kweli kabisa,nilisikia Manara aliwekwa ndani kwa sababu alifanya kosa, yani mtu ufanye utapeli huko alafu ukamatwe leo uje umsingizie Bashite ndio alikukamata na hata kama ingekuwa Bashite ndio aliagiza Manara akamatwe bado ni sahihi tu
 
cCM hawarudishagi mali, na hata ikitokea amerudisha zitaliwa na CCM wenzake, kwani zile Range rover zilizookotwa na mwenda zake pale bandarini na akasema zipigwe mnada zilipigwa ? Mali za sabaya zimekamatwa ? Ukiacha ile “vieitee” ambayo ipo Takukuru
 
Ila Manara ni mfalme wa machawa wote! Mo alivyotekwa alijitoa mazima kumpigania, sasa hizi chokochoko zote ni sababu boss wake anapambana na Makonda!

Ni kama Lemutuz, sasa hivi ndio anafafanua urafiki wake na Makonda wakati enzi hizo vita zote za Makonda alisimama na kumpigania. Ila baada ya kuchomolewa madarakani akapiga uturn!

Nafikiri lipo somo kubwa sana kwenye hizi issue ingawa naona vijana wengi bado wanafanya makosa yale yale!

Hizi tawala zinapita, kukosa msimamo ni kufanya usiaminike na washirika makini. Utaishia kutumika kama toilet papers. Hii tabia ya uchawa imepenya serikalini, kwenye vyama, kwenye dini, kwenye michezo kila sehemu na vijana ndio wahanga wakuu.
 
Umesema kweli kabisa,nilisikia Manara aliwekwa ndani kwa sababu alifanya kosa, yani mtu ufanye utapeli huko alafu ukamatwe leo uje umsingizie Bashite ndio alikukamata na hata kama ingekuwa Bashite ndio aliagiza Manara akamatwe bado ni sahihi tu
Na hakuwa peke yake walikuwa wengi waliokamatwa siku ile, wapo wengine waliokuja kuachiwa siku nyingi kupita baada ya Mo kupatikana, sasa hawa nao wasemaje?

Mi nafikiri manara angechagua upande ambao ni default kwake atakaokuwa anasimamia, kama ni soka tulia kwenye idara hiyo huko kwingine waachie wengine asitengeneze umaarufu kwa image mbaya ya kuwachafua wengine

Kama utakumbuka hapo mwaka jana kulikuwa na trend ya kumlinganisha samia na magufuli, jamaa akajitokeza nayeye tena akionekana kumponda magufuli ikiwa ni pamoja na swala la ATCL na wakati alishawahi kumpongeza sana katika kipindi cha uhai wake kwa swala hilo hilo

Point yangu iko hapa, muda utafika atakuja raisi mwingine, manara huyu huyu tutamuona tena akiwa against samia katika vitu hivi hivi ambayo tunaona leo akipongeza

Muda utafika hatakuwa chini ya GSM tena, tutayasikia mambo kibao negative kumhusu GSM dhidi ya manara ambayo hatukuweza kuyajua katika kipindi ambacho alikuwa muajiriwa

Hijalishi ni kiasi gani anonekana kuwa na furaha na kujimwabafai kuwa yuko sehemu nzuri anayoishi kwa raha, note my words siku akiachika hapo atakuja na backup kuondoa mazuri yote aliyokuwa akiwaaminisha anayapata hapo GSM

Hate a liar more than I hate a thief.
A thief is only after my salary,
A liar is after my reality
.
50-Cent​
 
Huyo Manara mbona hazungumzii ile saga yake kule CCM? Watulie tuseme sisi tuliokitaa sio hao ambao matendo yao tofauti ni nafasi tu, pengine wangekaa alipokuwa Makonda wangekuwa worse.
 
Manara aishi kwa akili na sio mihemuko Makonda anaweza rudi tena kwenye uongozi ataificha wapi sura yake? Tunajua anapewa shinikizo na GSM hilo liko wazi.

Ghafla makonda karudi kuwa mkuu wa mkoa manara atauweka wapi uso wake?

Manara ni tapeli mkubwa, ametapeli wengi tu sijajua bifu lake na kigogo limeishia wapi.
 
bila kupepesa macho wewe ni Bashite
 

Nani atamrudisha makonda kwenye ukuu wa Mkoa? Na kashfa zote hizo?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…