Hakuna baba ambaye hataki kuona watoto wake wote wanamtii, wanamheshimu na wanafanikiwa, tukubali tu kuwa kuna mapungufu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!
Hapa nazungumzia hawa miungu au Mungu maarufu duniani ambao mafundisho yao yameenea sana.
Dini hizi zilizoonea sana zinasema kuwa Mungu ni;
- Baba(mzazi)
-Muweza wa yote
-Yupo kila pahali
-Anajua yote
--Muumba
-Mwenye huruma.
*****Atakayewachoma moto watu wote wasiomtii na watenda dhambi.
Sasa imagine, kama dhambi anaichukia kwanini aliiumba?
Ok, tuseme yeye hajaleta dhambi,je, ni nani huyo mwenye nguvu akaweza kuumba kitu ambacho Mungu hakipendi?.
Ok. Kwanini hakuifanya hiyo dhambi isiwe na uwezo wa kumsogelea mwanadamu na badala yake mwanadamu atawaliwe na good will na uchaji tu mbele za Mungu ili adhma ya Mungu ya kuonyesha upendo ionekane?
Swali linguine: Je, mtu aliyetenda dhambi kwa siku mbili akihukumiwa adhabu ya moto wa milele (trilion and quadrillions of years ) ni sawa tuiite hiyo ni hukumu ya haki?
Mwanadamu yeyote asiye kichaa anatamani awe na watoto bora hivyo hujitahidi kumpeleka shule nzuri, kumchunga awapo nyumbani n.k ili awe mtoto bora ila muda mwingine huharibika kwasababu zilizo nje ya uwezo wake. Je, wanadamu watakapoingia motoni tuseme ni matokeo ya sababu zilizo nje ya uwezo wa Mungu muumba wake, yaani kuna jambo alitamani lakini ameshindwa?
Je, bado tumwite muweza wa yote?
 
Ni upuuzi kinyago cha udongo kilichopata crack kuhoji kwanin mfinyanz hakutumia cement..

Ni upuuzi akili ya siafu kuhitaji kuelewa anachowaza mwanadamu

Mungu akieleweka kwenye akili zetu, anaacha kua Mungu.

Mungu anaaminiwa anatumainiwa tu.
 
Nimejifunza kupitia mmea wa mgomba,ukisha toa mkungu wa ndizi,ile ndizi (nafsi) ikakomaa tayari kwa kuliwa au kwa matumizi mengine,basi,mgomba (mwili) hukatwa na kulazwa chini(kuzikwa) na ndizi tunda (nafsi) huchukuliwa na kwenda kufanyiwa kitu kingine lakini sio kuendeleza uzao wa migomba.
Kizazi cha migomba kitaendelea kwa kung'oa mashina (watoto) na kupanda (kuozesha) pengine kuendeleza kizazi.

Maisha ya duniani kwa mwanadamu ni ya duniani tu,hatuna uspesho wowote kututofautisha na viumbe vingine.
 
Dhambi haikuumbwa,aliyeumbwa ni mwanadamu.
Dhambi ni uasi,1Yohana 3:4.

Aliyekuwa WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ALIWAI KUSEMA MANENO HAYA "ukifanya fujo, unaambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine "

Wewe mwanadamu umeambiwa Oa ili usizini,,wewe hutaki kuoa au kuolewa una zinizini tu, wewe ni muasi..
Uchomwe tu mana umekataa kutii.
 
Mwanamke ambae hajaolewa afanyeje? Na hajapata wa kumchumbia na umri unaenda?
 
Mkuu kutokufanikiwa kununua au kununuliwa gari hai haralishi asiye na gari kuiba gari ya mtu.
Ikibainika kaiba atahukumiwa tu kwa mujibu wa sheria.
Kama hajapata wa mume au wa kumchumbia aombe kwa Mungu atapata,mbona maandiko yako wazi Mkuu,
Aliyesema usiibe,usizini ndiye aliyesema Ombeni nanyi mtapewa.
Lolote ulililokosa na hitaji nalo basi soma hili andiko,simamamia km kifungu Cha sheria kudai haki yako..

Matthew | Mathayo
7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

7:8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

7:9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?

7:10 Au akiomba samaki, atampa nyoka?
7:11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
 
Nimejifunza kupitia mmea wa mgomba,ukisha toa mkungu wa ndizi,ile ndizi (nafsi) ikakomaa tayari kwa kuliwa au kwa matumizi mengine,basi,mgomba (mwili) hukatwa na kulazwa chini(kuzikwa) na ndizi tunda (nafsi) huchukuliwa na kwenda kufanyiwa kitu kingine lakini sio kuendeleza uzao wa migomba.
Kizazi cha migomba kitaendelea kwa kung'oa mashina (watoto) na kupanda (kuozesha) pengine kuendeleza kizazi.

Maisha ya duniani kwa mwanadamu ni ya duniani tu,hatuna uspesho wowote kututofautisha na viumbe vingine.
Hii Ndio comment Bora Sana kuwahi kutana nayo katika upande wa haya maswala,big up wasipokuelewa hapa hawatakuja kuelewa kamwe!
Big up mkuu!
 
Mkuu kutokufanikiwa kununua au kununuliwa gari hai haralishi asiye na gari kuiba gari ya mtu.
Ikibainika kaiba atahukumiwa tu kwa mujibu wa sheria.
Kama hajapata wa mume au wa kumchumbia aombe kwa Mungu atapata,mbona maandiko yako wazi Mkuu,
Aliyesema usiibe,usizini ndiye aliyesema Ombeni nanyi mtapewa.
Lolote ulililokosa na hitaji nalo basi soma hili andiko,simamamia km kifungu Cha sheria kudai haki yako..

Matthew | Mathayo
7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

7:8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

7:9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?

7:10 Au akiomba samaki, atampa nyoka?
7:11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Wewe naona unaleta theory kwenye mambo practical, mtu aache kuzaa asubiri kuchumbiwa? Na anakua bibi anajiona? You are joking
 
Siku hizi mungu amekuwa kama chama wa simba tu.hana hadhi kabisa.
 
Dhambi haikuumbwa,aliyeumbwa ni mwanadamu.
Dhambi ni uasi,1Yohana 3:4.

Aliyekuwa WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ALIWAI KUSEMA MANENO HAYA "ukifanya fujo, unaambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine "

Wewe mwanadamu umeambiwa Oa ili usizini,,wewe hutaki kuoa au kuolewa una zinizini tu, wewe ni muasi..
Uchomwe tu mana umekataa kutii.
Unaongeleaje Isaya 45:7
 
Habari!
Hapa nazungumzia hawa miungu au Mungu maarufu duniani ambao mafundisho yao yameenea sana.
Dini hizi zilizoonea sana zinasema kuwa Mungu ni;
- Baba(mzazi)
-Muweza wa yote
-Yupo kila pahali
-Anajua yote
--Muumba
-Mwenye huruma.
*****Atakayewachoma moto watu wote wasiomtii na watenda dhambi.
Sasa imagine, kama dhambi anaichukia kwanini aliiumba?
Ok, tuseme yeye hajaleta dhambi,je, ni nani huyo mwenye nguvu akaweza kuumba kitu ambacho Mungu hakipendi?.
Ok. Kwanini hakuifanya hiyo dhambi isiwe na uwezo wa kumsogelea mwanadamu na badala yake mwanadamu atawaliwe na good will na uchaji tu mbele za Mungu ili adhma ya Mungu ya kuonyesha upendo ionekane?
Swali linguine: Je, mtu aliyetenda dhambi kwa siku mbili akihukumiwa adhabu ya moto wa milele (trilion and quadrillions of years ) ni sawa tuiite hiyo ni hukumu ya haki?
Mwanadamu yeyote asiye kichaa anatamani awe na watoto bora hivyo hujitahidi kumpeleka shule nzuri, kumchunga awapo nyumbani n.k ili awe mtoto bora ila muda mwingine huharibika kwasababu zilizo nje ya uwezo wake. Je, wanadamu watakapoingia motoni tuseme ni matokeo ya sababu zilizo nje ya uwezo wa Mungu muumba wake, yaani kuna jambo alitamani lakini ameshindwa?
Je, bado tumwite muweza wa yote?
Angetuumba hivyo unavyotaka tungekuwa maroboti siyo wanadamu tena. Raha ya maisha ni Uhuru wa kuamua utakacho ingawa wakati unaamua uwe tayari kupokea matokeo ya maamuzi yako. Mimi naona Mungu yupo sahihi kabisa. Kuwa roboti hapana kwa kweli.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom