God The Creator yaani Mungu Muumba wa vyote vinavyo onekana na visivyo onekana.
Omniscience, Omnipotent, Alfa na Omega
Omnipresent yuko ndani yetu.
Omniscience
The Creator
True
Kuna vitu kumhusu Mungu, havikuandikwa kwenye vitabu vya dini. Imeandikwa Mungu aliumba kila kitu, sii kweli. Mwanzo wa Mungu ndio mwanzo wa shetani!. Mungu hakumuumba shetani!. Mungu ameumba kila kitu chema hivyo Mungu hakuumba dhambi!. Shetani ndie ameumba dhambi na kila aina ya uovu!.
Mwanzo shetani alikuwa malaika mkuu the 2/ic. Haiwezekani Mungu amuumbe shetani halafu huyo shetani atake kumpindua Mungu yeye awe ndiye Mungu!.
Baada ya shetani kuasi, angekuwa ameumbwa na Mungu, Mungu ange m destroy!. Mwanzo wa Mungu ndio mwanzo wa shetani, the source of powers za Mungu ndio the same source of powers za shetani!. God has powers na the devil has powers.
Tofauti kati ya Mungu na shetani ni tofauti 3 tuu
1. Wote Mungu na shetani wana powers, ila Mungu ana powers zaidi ya shetani. Mungu anaweza kuzuia mipango yote ya shetani lakini shetani hawezi kuzuia mipango ya Mungu anaweza kuitubua tuu na kuichelewesha lakini sio kuizua!.
2. God ndiye the creator yaani Mungu ndie muumba, the giver of life, shetani hawezi kuumba, shetani yeye ni the destroyer wa kile Mungu alichokiumba ili kimuasi Mungu na kumfuata yeye shetani.
3. Pomoja na shetani kuwa the destroyer lakini hana uwezo to end life, uwezo to end life ni uwezo wa Mungu pekee!.
Hivyote ukiondoa vitu vitatu hivyo, vitu vingine vyote that God can do, the devil can do!.
Shetani ni bingwa wa kujigeuza anaweza kujigeuza kiumbe chochote na ni mzuri wa kuji super impose and disguise as God hivyo kuna dini nyingi huku duniani wana mwabudu shetani disguised as God bila wao kujijua wakidhani wanamuabudu Mungu!.
Hivyo shetani baada ya kuasi, Mungu akasemezana na NENO na Roho Mtakatifu "na tuumbe kiumbe cha mfano wetu ambacho kitatutii". Mungu akamuumba Adamu
Shetani akamfuata Mungu na kumwambia ili kuujua utii wa kiumbe hiki, kipe temptation, majaribu, kikishinda majaribu ndipo utathibisha utii wa kiumbe chako.
Mungu akakubali, akamuumba mwanamke, na kumruhusu shetani aweke yale majaribu kwa kuweka ule 'mti' wa katikati na lile 'tunda' pale alipoliweka!. Hivyo ni shetani ndie aliyeumba dhambi.
Mungu akawapa binadamu conscious ya kuamua kumfuata YEYE au shetani kwa kuwapa utashi, akawaonya Adamu na Eva wasimege 'tunda' la 'mti' wa katikati, mti wa mema na mabaya, watakufa!.
Shetani akajigeuza nyoka, huku Mungu anamuona!, akademya bustanini huku Mungu anamuona!. Baada ya kuingia bustanini, akajigeuza a handsome guy na kumtokea Eva!. Eva akashtuka na kushangaa sana kuona binadamu mwingine zaidi ya Adamu mule bustanini!.
Shetani ndipo akamuuliza Eva, hiyo ni nini?, akimuelekezea kwenye 'tunda', Eva akamjibu hili ni tunda Mungu ametukataza tusile!.
Shetani akamuuliza kwa nini Mungu amewakataza msile hili 'tunda' la 'mti' huu wa katikati?.
Eva akamjibu sijui ni kwanini tumekatazwa, Mungu amesema tukila tutakufa!.
Shetani ndipo akamwambia Eva, Mungu ni muongo, amewakataza kula hili tunda kwasababu hataki mfaidi!. Hili ndio tunda tamu kuliko matunda yote, tunda hili likimegwa kisawasawa ndio utapata raha na kusikia utamu kuliko raha zote, na kuliko utamu wote!.
Na kikubwa zaidi katika kumega tunda hili, nyinyi binadamu mtapata uwezo wa ki Mungu wa kuumba viumbe wengine "concepcion". Ngoja nikuonyeshe!.
Shetani akamuonyesha Eva jinsi tunda linavyomegwa kwa kumchumia na kummegea hivyo 'tunda' kumegwa na kweli Eva akalisikia tunda lilivyo tamu kwa utamu alioupata kwa kumegwa lile tunda, hivyo akamfuata Adamu na kwanza kumhadithia utamu wa kumegwa tunda, kumfundisha jinsi tunda linavyomegwa na kumlazimisha Adamu naye lazima amege tunda na kweli Adamu naye akamega na kweli kwa utamu wa tunda, wote wakaishia uzingizini!, ila hapo ndipo wakawa wameitenda dhambi ya asili, the original sin.
Wakati yote haya yakifanyika Mungu anaangalia tuu!. Baada ya kupata mapumziko ya kutosha baada ya kazi kubwa ya kumega tunda, ndipo Mungu akawaamsha na kujishtukia wako uchi baada ya lile tendo!.
Ikafuatia adhabu ya kutimuliwa toka bustanini, mwanamume kula kwa jasho lake, mwanamke kuzaa kwa uchungu. Hapa sasa ndipo neno "zaeni muongezeke muijaze nchi yote lilipokuja!.
Hivyo ili kiumbe kipya kizaliwe ni lazima lile tendo la dhambi ya asili litendeke. Mtu pekee aliyewahi kukingiwa dhambi ya asili ni Bikira Maria kwa kupata ujauzito wa Yesu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huku akiwa bikira bila 'tunda' kumegwa, hivyo Yesu ndiye kiumbe pekee duniani aliyezaliwa bila dhambi ya asili kutendwa!.
Ni shetani ndio aliumba dhambi
Mungu amempa binadamu utashi wa kuchagua.
Kule ni ulimwemgu wa Roho, hakuna mass, distance wala time!. Siku moja ni kama miaka 1000 na miaka 1000 ni kama siku moja!.
Mungu ameumba mbigu ya raha ya milele na shetani ndie ameumbiwa jehanum ya ziwa la moto wa milele. Binadamu amepewa conscious ya utashi wa kuchagua kumfuata Mungu au kumfuata shetani.
Yes pamoja uwezo wa shetani, ni Mungu tuu pekee ndiye pekee muweza wa yote!.
Rejea
1.
Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.
2.
Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?
3.
Kwa mnaojua hebu fafanueni hili naona kama wengi wanapotoshwa
4.
Jee Wajua Dunia Nzima Sote ni Watoto wa Baba Mmoja na Mungu Mmoja?. Krismasi ni Sikukuu ya Wote, Tutoe Kwa Wengine, Tushereheke Pamoja-Merry X-Mass!.
5.
Kumbe Shetani Alikuwa Mwandishi wa Habari!, na Alichomfanya Eva Bustani ya Eden ni Uandishi wa Habari?- Je Media Tuombwewe Msamaha Kuitwa Shetani au?