Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Mkuu umenena mengi lakini hapo kwenye kuzaliwa ukiwa na uwezo sikubali hata siku Moja.

Iko hivi wabrazil wengi wana uwezo wa kuuchezea mpira kwa sababu wako huru na kwao kuuchezea mpira ni maisha ya Kila siku tofauti na wachezaji wengi kutoka ulaya ambao kwenye academy wanafundishwa kwa kanuni maalumu kwa kupiga pasi n.k ndiyo maana hawaibui madoido mengine kama wanavyofanya wabrazil.

Kama kweli mtu anazaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani kwa nini wengi wao wanazaliwa sehemu moja kwa mfano unatakiwa kujiuliza kwamba kwa nini wachina na wahindi hawazaliwi na kipaji cha mpira lakini wabrazil wanazaliwa nacho?

Kwa nini wanafalsafa wengi wa zamani wanatokea Ugiriki na siyo Tanzania? Au Ugiriki iliprndelewa na mungu.

Tungekuwa tuanzaliwa na uwezo fulani basi wazungu wasingekuja kututawa maana tungekuwa sawa au tungekaribiana kwa uwezo.

Eti mtanzania anajisifu kuwa na kipaji/ amezaliwa na uwezo wa kusoma haraka haraka wakati maandishi yasingeletwa asingefahamu hata a e i o u.
 
Mkuu habu niambie wewe una kipaji gani na una vipaji vingapi.
 
Alivumbua ndege mwaka gani.
 
Usijifunge kufikiri kutokanana neno 'kuzaliwa nacho'.

Hili neno laweza kuwa: 'ikitokea kumudu kwa urahisi na kwa ufanisi'.

Teknolojia za binadamu zinazaliwa kila leo, kwa mfano hivi sasa kuna teknolojia ya 'AI' na wanapatikana wataalamu wabobezi wanaokuwa na kipaji hicho wakimudu kwa ufanisi na wengine hawatwezi.

Binadamu tumegawanyika kifikra, kimaoni na kiuwezo, kila mtu anapendelea kufanya jambo flani analolimudu lisilofanana na la mwingine, ndiyo vipaji hivyo.
 
Kila mtu ana zaidi ya Kipaji kimoja
Basi duniani hakuna kipaji bali kufanya kitu kwa ufanisi kunatokana jitihada na mchanganyiko wa sababu zingine kama kukipenda kitu, kukifikiria kitu na factors zingine mbalimbli.

Kadiri mchanganyiko wa hizo factors unavyokuwa mkubwa basi ufanisi wako katika kufanya jambo unakuwa mkubwa.

Kwa mfano unapokuwa mchezaji wa mpira ukawa na umbo linalokusapoti kucheza mpira, unapoupenda mpira unapouwazia mpira kwa Kila wakati na kufanya mental exercise kucheza mpira (kwa mfano ukilala usiku una imagine kana kwamba unawapiga watu chenga kwa styles tofauti tofauti) na kisha ukaongeza jitahada (physical exercise) na kuongeza ubunifu basi wewe utakuwa mchezaji mkubwa sana.

Haya mambo ukiyaanza udogoni basi hautashikaka dimbani.
 
Pale kwenye 'kuzaliwa nacho' ndipo ninapopapinga mkuu.

Asante kwa kunielewa kwa kiasi fulani.
 
Ni vizuri kwanza ujiulize kipaji ni nini?, Kuna majina mengi yanayotumika uenda tokana na mazingira ya mtu alipo,, kwingine kinaitwa kipawa,kipaji,kusudi nk nk,,
Sasa ni kwamba kila mtu anazaliwa akiwa na kusudi lake,na tofauti yetu sisi na hao wazungu ni namna yakugundua hilo kusudi,hii tokana hasa na elimu zetu zilivyo..,ivyo kwa kifupi kipaji ni hobi au shauku aliyonayo mtu toka ndani yake, katika kufanya jambo fulani,kama hivyo kuchora,tangu utotoni unajisikia hivyo kufanya,huku afrika unakuta mzazi kwa kutokujua anaona mwanae kapotea kimaarifa au kielimu nk,wazungu ni tofauti nasi.
Unaposema bolt angeonyeshaje kipaji pasipo kuwepo riadha,ni kwamba angeweza kufanya kingine kilichopo!!,, kumbuka kuwa pia watu ufanya kitu kwa kuona au kusikia au kuhisi tokana na mazingira aliomo,aliyeanzisha mpira alianza kwa kuhisi nakufanyia kazi, mtoto mdogo uhisi njaa inayompelekea kuingiza kitu kinywani,anaona ndo atapata nafuu au kuiondoa njaa japo kwa mda.
Hivyo kipaji kipo na mtu anazaliwa akiwa nacho,,wewe hukukatishwa tamaa kwa kuwa hicho ndo kipaji chako,jua pia akukatishaye tamaa pengine huwa si yeye bali ni mitazamo yake inamfanya awe hivyo,sio kwamba ana roho mbaya dhidi yako,pengine hajui kwamba hicho ni kipaji kwako na wala hajui kipaji ni nini,hivyo anasukumwa tu na mihemko yake.
 
Ni wewe Tu unayo muona

mess mbona Mimi namuona Hana kitu ?

Utimamu wa afya ya akili na hata ukakamavu wa mwili huimarishwa na mazoezi, usijidanganye kwa vyanzo uchwara ambavyo hata mimi naweza kuviandika na kuvituma hapa mitandaoni.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is the.
 
Mkuu unachokizungimzia wewe ni instinct yaani kitu ambacho ni natural kwa Kila kiumbe kwa mfano mtoto akizaliwa hafundishwi kunyonya, hafunfundishwi kulia (binadamu tunatofautina lugha lakini wote kwenye kulia wanafanana), tamaa ya mapenzi mtu hufundishwi, njaa hufundishwi pia, hizo zote zinaitwa instincts maana ni uniform kwa bidamu wote.

Hivi vitu vingine unavikuta duniani au katika jamii uliyozaliwa. Mtu aliyekuzwa na wanyama kuna tabia anaziadapt kutoka kwa wanyama lakini instincts ni sawa kwa binadamu wote na inahusu vitu nilivyovitaja hapo juu.

Kwa hiyo hauwezi kuzaliwa au kutoka tumboni mwa mama yako ukiwa na uwezo wa kucheza mpira, kuimba, kuendesha gari bali utakuja kujifunza huku duniani.
 
Unaweza kufundishwa kitu na kujifunza mwenyewe. Kwa hiyo unamaanisha ukijifunza mwenyewe ndo kipaji na ukifindishwa ndo skills, si ndiyo?
HIvi vitu vinachanganya lakin twende taratibu kidogo.

Kitendo cha kujiongeza kwenye jambo fulani na ukawa mwepesi kuki master hiyo ni talent, kwa maana huo ni uwezo wako wa asili ambao upo nao kwenye jambo hilo.

Pia kumbuka kila mtu ana jambo lake ambalo ni mwepesi na hodari wa ku-catch(talent).

Tukija kwenye Skill/Ujuzi, Hali hii inakuja baada ya desire kutamalaki, yaani unajikuta unapenda jambo fulani hivyo itapelekea kulifanya mara kwa mara na mwishowe kubobea kabisa katika jambo hilo,

Skill haijalishi kama una kipaji au hauna isipokuwa mtu mwenye talent/kipaji na akawa na skill/ujuzi anakuwa ahead ya wewe mwenye skill/ujuzi peke yake.

Labda tupate mfano kidogo.
Darasani wanafunzi wote wanasoma kwa bidii, Lakin watatokea wanafunzi wachache ambao hao wanakuwa moto, yaani ni vipanga balaa na ingawa wanafunzi wote wanafundishwa na mwalimu mmoja.

Hapo pia kuna wanafunzi wengine ambao nao wanafosi kusoma kila siku yaani wanajikuta wanapenda kusoma ila ndo hivyo kitabu kinawakataa, sasa hawa wakiendelea kukaza, yaani kusoma na kusoma zaidi ndo wanakuwa nao hodari darasani.

Hapa tunapata wanafunzi wa aina mbili, mmoja hatumii nguvu kubwa kusoma ila ni kipanga, na mwengine anatumia nguvu kubwa kusoma ila nae ni kipanga vile vile.

Mfano no 2.
Katika hao vipanga darasani kuna wengine ndo vilaza kabisa yaani washajikatia tamaa na masomo yenyewe.

Ila upande wa pili wa shilingi hao jamaa wanapiga mpira balaa yaani shule nzima hakuna, hao hata wasipofanya mazoezi ndani ya week nzima ikija mechi wanakiwasha ile ile.

Kwa kifupi mzunguko unabaki kuwa ni hivyo hivyo kwa watu wote.
 
Secretary Bird umeona jibu zuri na la kibabe hili?
Jitihada na imani ndivyo maana halisi ya neno kipaji.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Kitendo cha kujiongeza kwenye jambo fulani na ukawa mwepesi kuki master hiyo ni talent, kwa maana huo ni uwezo wako wa asili ambao upo nao kwenye jambo hilo.
Kwa hiyo hapa tumekubaliana kuwa kipaji/talent is not something inborn siyo? Bali ni kujingenezea au kutafuta namna rahisi ya kufanya jambo kiuwepesi yaani kujitengezea formula fulani ya tofauti kwenye akili yako tofauti na watu wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…