Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Naomba twende swali kwa swali ili tuelewane then kama kuna umuhimu wa kuelezea nitaelezea.

Unajuaje kama mtu huyu anakipaji na huyu ana ujuzi au vyote kwa pamoja?
 
Naomba twende swali kwa swali ili tuelewane then kama kuna umuhimu wa kuelezea nitaelezea.

Unajuaje kama mtu huyu anakipaji na huyu ana ujuzi au vyote kwa pamoja?
Mimi naamini hakuna kitu kinachoitwa kipaji, kwa lugha rahisi ni kwamba hakuna mtu anayezaliwa akiwa na uwezo wa kufanya kitu fulani.
 
Utimamu wa afya ya akili na hata ukakamavu wa mwili huimarishwa na mazoezi, usijidanganye kwa vyanzo uchwara ambavyo hata mimi naweza kuviandika na kuvituma hapa mitandaoni.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is the.
Kwa hiyo Messi anafanya mazoezi kama Ronaldo ? 😅 😅 😅 😅
 
uwezo wa asili ambao mtu anazaliwa nao huenda kazaliwa na sauti nzuri,miguu myepesi ya kisoka, miguu yenye kasi, akili yenye uwezo mkubwa, ushupavu wa mwili, ni vitu ambavyo anaviweza kiasili kwasababu amezaliwa na uwezo huo "kipaji", lakini mtu asie na uwezo mkubwa atatumia jitihada kubwa kujifunza na hata akijua hatafikia uwezo wa mwenye kipaji.

Mwenye kipaji anafanya kwa wepesi, asie na kipaji atatumia jitihada kubwa.
 
Huyu sio kipaji ila IQ yake Iko mbele zaid ya wengine uwezo wake wa ubongo uko vizur miaka ya nyuma UDSm ilikua na hao wanafunzi wengi Kuna mmoja badala awe mwanafunzi wakamfanya lecture ila Ile Hali ilimfanya awe kama chizi baadaye alifariki
 
aani mtu anatoka tumboni akiwa na uwezo fulani tofauti na watu waliptoka tumboni kama yeye.
Ni kweli ila
Hakuna zezeta hata mashuleni ila Kuna watu wanaelewa kwa Kasi ya Ajabu jambo/ someone fulani kana kwamba wamezaliwa nalo.
Intelijensia na saikolojia inaleta utofauti katika utendaji was mtu na mtu kupishana, kufungamana na kukaribiana.
Zile hatua nilizokuuliza mwanzo zitarejea Tena huku.
 
Jaribu uwaulize wanajiskiaje ?
Level ya hisia zao katika eneo Hilo ndio mwisho was utendaji wao was miujiza.
Nna uhakika hi ndio sababu wengi ubunifu Hakuna na wengi waliofanya Mambo waliyoyapenda bila kulazimishwa iwe mashuleni kuwa wore tupite hapa na tufanane wameenda mbali.

Wengi nnao wajua hawana furaha ila imewabidi kufanya hayo ili kuishi kesho zao.

Kilichoanza ndani yao kinalia maana nafasi hiyo inadai kujielezea mbele ya hadhira.
 
Hapo umetaja viungo vya mwili ambavo vinaweza kumsapoti mtu kufanya jambo fulani kwa urahisi.

Haya mtu mwenye ulemavu miguu wa kuzaliwa nao anaweza kuwa na kipaji cha mpira/anaweza kuzaliwa na uwezo wa kucheza mpira?
 
We umeshinda bwana wazungu wana msemo "an old dog can't learn new tricks. " Kipaji ni urahisi was mtu kufanya kitu fulani.
Hapana. Mmeshasema mtu mwenye kipaji hahitaji mazoezi bali hutoka na uwezo tumboni mwa mama yake na ku perform better.
 
Hapo umetaja viungo vya mwili ambavo vinaweza kumsapoti mtu kufanya jambo fulani kwa urahisi.

Haya mtu mwenye ulemavu miguu wa kuzaliwa nao anaweza kuwa na kipaji cha mpira/anaweza kuzaliwa na uwezo wa kucheza mpira?
Kwahio mkuu unaunda mfano ambao mtu hana miguu then unataka nijibu kwamba anakipaji kinachotumia miguu, ndio anaweza kuzaliwa ana kipaji cha mpira lakini hatutajua hilo sababu ana ulemavu wa miguu.
 
Hahaha 😂
 
Kwahio mkuu unaunda mfano ambao mtu hana miguu then unataka nijibu kwamba anakipaji kinachotumia miguu, ndio anaweza kuzaliwa ana kipaji cha mpira lakini hatutajua hilo sababu ana ulemavu wa miguu.
Aise we unanifurahisha sana.

Haya tukigundua kuwa ana kipaji cha mpira tutamsaidiaje ili aendeleze kipaji chake maana mnasema kipaji kukivumbuliwa kinaweza kuendelezwa kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…