Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Kwanye maelezo ya kwanza umesema mtu mmoja anaweza kuwa na vipaji hata milioni Moja, kwenye comment hii unasema katika vipaji vingi vilivyopo mtu anaweza kuwa na kipaji kimoja wapo.
 
Mkuu nilichokuwa nabishia ni kuaminishana kuwa tunazaliwa na uwezo wa kufanya jambo fulani (kipaji).

Basi tubadili definition ya neno kipaji.
Kila binadamu ana akili, lkn si kila binadamu ana kipaji,ni wachache wanaoonekana wana kipaji kwa kuwa kimejidhihirisha kwa watu wengine,,hivi vyote havipatikani shuleni,bali shule yaweza kuviibua,kuvinoa vikawa na makali,yatakayopelekea kutoa matokeo chanya kwa jamii,watu kama kina Socrates Yasemekana hawakuwa na walimu waliowafundisha, lkn wamefanya mambo makubwa yakifikra ikiwemo pia kuwasomesha akina Aristotle na plato ambao nao wameacha alama hapa duniani, Socrates alikuwa na kipaji sana.
Unataka tutumie neno jingine badala ya kipaji,aayah pendekeza neno unaloona linafaa,, ahsante usiku mwema mkuu.
 
Bado najamaa na msimamo wangu kuwa tunazaliwa tukiwa sawa (tukiwa hatuzidiani). Tukianza maisha ya duniani ndipo tunaanza kuzidiiana due to several factors.

Kwa mfano Socrates alipozaliwa alikuwa sawa na wewe ulivyozaliwa lakini mlipoanza kuishi tofauti ikaanzankuonekana, yawezekana wewe ungezaliwa katika familia ya akina Socrates miaka ile ndo ungekuwa na akili kama zake halafu Socrates angezaliwa katika familia yenu mwaka ambao we ulizaliwa angekuwa a akili kama yako.

That's my point.
 
Nipo na wewe kaka ,aliegundua umeme ni mtoto ambaye shule zote walimkataa kwa sababu alikuwa kichwa maji na barua ya kuachiwa shule alipewa mama lakini mama ndio kama akamwambia mwanawe walimu hawana cha kukusomesha kwa sababu wewe una akili sana kushinda wanafunzi wenzako matokea yake kagundua umeme ,so hakuna kipaji cha kuzaliwa kuna jitahada na nothing imposble kwa binadamu amua tu nini unataka kuwa.
 
Jitihada haziji hivi hivi kirahisi,jitihada nzuri na bora ni zile zinazochochewa na shahuku na matamanio toka ndani yako,zisizo na chembe ya ushawishi au msukumo toka nje yako,ndo utoa matokeo chanya na yenye ufanisi mkubwa sana.hayo yote yatakuwa na msukumo mzuri kama yatatokana na kipaji ulichozaliwa nacho.
 
Kweli kabisa mkuu. Hata Ben Carson aliyefamfanyia mwanadamu oparesheni ya ubongo alikuwa anaitwa kilaza na wanafunzi wenzake lakini mama yake alimtia moyo na kimpandikizia imani kuwa anaweza kuwa bora na hatimaye Leo ameingia katika vitabu vya kihistoria.

Cc Angel Nylon
 
Mkuu kwa nini unakomalia neno 'kipaji ulichozaliwa nacho'?πŸ˜…
 
Mkuu kwa nini unakomalia neno 'kipaji ulichozaliwa nacho'?πŸ˜…
KIPAJI ni Propaganda za wazungu kutaka kuwanya Waafrika kama nyinyi hamna akili au hamna kipaji kuna vitu wazungu ni mbwa na watu wabaya sana .Kwa mfano wakishakuona kijana mweusi ni hodari kwa kila kitu wanaanza kukutengezea zengwe toka mwanzo kuanzia shule ,university,kwenye kozi za polisi au jeshi au popote tu nia yao usionekane ukaja wapita watu weupe.
 
Cha kusikitisha ni kuwa waafrika bado hawajaelewa hii trick.
 
Kwa maana hakuna mtu alitoka tboni mwa mama yake na akili na uwezo wa kufanya jambo kuzidi wengine.

Instincts zinafanana kwa Kila mtu.
Unajuaje sasa kwamba tunapozaliwa tunakuwa hatuna huo uwezo? Kwamba ulitaka mfano kuona mtoto ana uwezo wa kuimba akiwa bado mtoto mchanga ndio uone huo utofauti au kipaji?
 
Unajuaje sasa kwamba tunapozaliwa tunakuwa hatuna huo uwezo? Kwamba ulitaka mfano kuona mtoto ana uwezo wa kuimba akiwa bado mtoto mchanga ndio uone huo utofauti au kipaji?
We unajuaje kwamba tunapoziwa tuna uwezo au kipaji😎.
 
We unajuaje kwamba tunapoziwa tuna uwezo au kipaji😎.
Mimi siwezi kudai kwamba tunakuwa na kipaji toka pale tunapozaliwa tu kwa sababu sina uwezo kujua kiuhakika kuhusu hilo ila najua vipaji vipo. Kwa sababu huo uwezo wa kufanya jambo fulani huonekana kwa watu tokea udogoni kwao na ndio maana kuna hadi familia zenye kujulikana kwa aina fulani ya kipaji yani tokea watoto wakiwa wadogo huonekana kuwa na uwezo wa kufanya jambo fulani.
 
Toa mfano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…