Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Ngoja nikutumie mkuuπŸ€£πŸ˜‚
 
sie kuna jamaa alikuwa anakula chapati 6 za jero jero na maharage bakuli moja kubwaa then anashushia na maji kidumu cha lita 5
 
Hebu tuwekee hapa hizo picha zako ulizochora tuone kama kweli huna kipaji
 
Kauli ya kwamba mtu anazaliwa akiwa anajua kufanya kitu fulani au akiwa na kipaji fulani mie sipendi kuitumia, ila nakubali uwepo wa vipaji.

Mimi sisemi kwamba mtu akiwa bora kuliko wengine basi hiko ni kipaji tu, mtu anaweza kuwazidi wenzake na kuwa bora kutokana na juhudi alizonazo tofauti na wenzake.

Mleta mada anakataa issue ya uwepo wa kipaji anadai ni issue ya juhudi katika mazoezi, ndio maana nauliza kama ni hivyo watu kama akina Messi na Ronaldo ni mazoezi yapi wanayofanya tofauti na wenzao au ni mazingira gani yenye kuwafanya kuibuka kuwa bora kushinda wenzao?
 
Mkuu swali ambalo linatakiwa kujibiwa kwamba ni kitu gani ambacho hufanya mchezaji mmoja kuonekana bora kuliko wenzake na hali ya kwamba watu wapo katika mazingira sawa na hufanya mazoezi sawa?
Hapo awali nilimjibu bird,kuwa hata mapacha walozaliwa toka mfuko mmoja wanaweza fanana sura lkn tabia ni tofauti, we utajiuliza ni kwanini?, Naweza jibu kiimani zaidi,ni kwamba ni hili tutambuane kupitia hizo tofauti,kwa hiyo iko hivyo,na huo utofauti ndo upelekea hata katika fani yoyote , mtu kubobea upande fulani, mfano daktari fulani kubobea upande wa ngozi tu au mwingine upande wa kinywa na meno tu,nk nk,jua tu kwamba utofauti lazima uwepo baasi.
Sasa unapouliza kwanini mchezaji wa hapa tz ni tofauti na wa kule ulaya,sababu ni kwamba mazingira yetu na wao kwanza kielimu yako tofauti,pili kiuchumi,tatu sera,mfano sisi tunakuza kipaji mtu ameshakuwa mkubwa,,lkn wanaanza wakiwa watoto kwanza wanagundua vipaji vyao,then wanaendelezwa hadi ukubwani,kwa akili ya kawaida tu mtu utaona hapo lazima utofauti uwepo,,kiutendaji nk nk,,naishia hapo πŸ«΅πŸ«΅πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kumbuka mwanzoni mlisema aliyezaliwa na kipaji akifanya mazoezi sawa na asiye na kipaji basi mwenye kipaji anakuwa na ufanisi mkubwa haya FEISAL SALUM amezaliwa na kipaji na anapiga mazoezi na CHRISTIANO RONALDO hajazaliwa na kipaji na anafanya mazoezi kama FEI TOTO.

Je ni kwa nini FEISAL aliyezaliwa na kipaji bado ana uwezo mdogo ukimlinganisha na CHRISTIANO ambaye amabeye hakuzaliwa na kipaji na wote wanapiga mazoezi 😎😎😎😎😎😎😎.

Jibu lako nalisubiri kwa hamu na gamu.
 
Uko sahihi, hakuna kipaji, tunazidiana uwezo tu kama ilivyo kwenye akili, mwingine aaonekana mwenye upeo mkubwa mwingine mdogo.

Mfano kama ulivyoeleza; Mpira na vitu vingine vingi, tunabuni sisi wanadamu, lakini inaonekana kipaji/talent iko ndani yako in nature.
Je kama visingewekwa/visingekuwepo ingekuwaje??


Hoja yako naiunga mkono✌
 
CCM inaaminisha watu vitu vya ajabu Mkuu πŸ˜€πŸ˜…
 
Jamaa anatumia nguvu kukataa kipaji ila anaruka ruka na kuji contradict tu.
 
Kungekuwa na messi na Ronaldo wengi yani tungekuwa na wachezaji wenye kiwango bora sawa na hao wachezaji, ni kitu gani sasa kinachofanya wachezaji wengine wasiwe na kiwango sawa na hao wakina Messi na Ronaldo?
 
Kungekuwa na messi na Ronaldo wengi yani tungekuwa na wachezaji wenye kiwango bora sawa na hao wachezaji, ni kitu gani sasa kinachofanya wachezaji wengine wasiwe na kiwango sawa na hao wakina Messi na Ronaldo?
Basi Tanzania hakuna mtu mwenye kipaji na wachezaji wote wanaocheza ligi kuu ya Uingereza wana kipaji maana wachezaji wa Tanzania hawana quality ya kucheza kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Hapo vipi😎.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…