Mheshimiwa alikua na msimamo sana. Alichokipanga kichwani kwake ilikua lazima akitimize. Najua alitamani sana kuwainua watu wa Chato maana ni kwao. Ni kitu kizuri, ila angewasaidia kwa kufuata utaratibu unaotumika kuinua wilaya zingine hapa nchini na sio kufanya ki upendeleo kama alivyofanya yeye.
Kilichomuharibia, hakua smart kwenye ulimwengu wa siasa na uchumi. Fedha za umma huwezi kuzitumia hivyo. Alishindwa kuset vizuri na kuzisimamia priorities za nchi.
Achana na Chato, ulishawahi kwenda ile Stand kubwa ya Dodoma? Jengo kubwa, vyumba vingi ambavyo havijapangishwa, eneo kuuuubwaaa for what? Kwanza Bus nyingi hazipiti pale. Siku za katikati ya wiki ukiwa unahitaji kusafiri haraka ukaenda kule nanenane ndio umebugi kabisa, hamna kitu. Pamepoa vibaya mno mpaka unajiuliza nini ilikua Motives ya Serikali kuweka nguvu kubwa hivi? Bora hata wangefanya Chuo pangekua utilized vizuri kuliko walivyofanya Stand lile eneo!
Anyway, kila mtu na kichwa chake!