Hali ilivyo Stendi Kuu ya mabasi Chato

Hali ilivyo Stendi Kuu ya mabasi Chato

Pamoja na ubaya wake ila jamaa alipapenda sana kwao

Nenda masasi ukaone maajabu ya hayati unaweza sema eneo Hilo halikutoa kiongozi mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu soma tena ulichoandika kisha tafakari kwa kina.
Kwa hiyo kwako wewe kiongozi bora ni yule anayetumia pesa za umma kujenga kwao hata miradi isiyotumika?
 
Mwendazake amekwenda na stendi yake!!! R.I.P kwa Mwendazake. . .!!! R.I.P Kwa Stendi. . .!!!

Hizo fremu wakipangisha hata kwa Tsh 10,000/= kwa mwezi, hawapati mpangaji ng'o.
Stendi ya Bukoba ikifika saa tano asubuhi...mabasi hayapaki ndani ya stendi kupisha daladala...saa 11 moja ndo daladala nyingi zinakuwa zinaenda vijijinu hivyo yanapata nafasi na haitoshi maana mabasi mengi huishia Bukoba na kulala bukoba...stendi ni ndogo mno

Mvua ikinyesha unatamani usishuke kwenye gari..

Bukoba ingepata japo stendi kama hii nadhani mapato yangeongezeka maradufu na kama ni mkopo wangeshalipa kitambo sana....

Lakin hadi leo pesa za ujenzi wa stendi ya bukoba huwa hazipatikani...juzi tu ndo wamepata bilion 1 tu ya ujenzi wa stendi...nikiwaza stendi ya magufuli mbezi ilitumia billion 71 na bado iko underutilized hadi leo ndo naishiwa pumzi kabisa....

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kwani kuna Wilaya ambayo haikupata Stendi? Tena si bora Chato palichelewa sana hiyo stendi imemalizika mwaka jana?

Juzi nilifika Iringa huko Stand mpya Igumilo sijui wanapaita pamepoa vibaya mno! Nenda Kibaha stand ilipo! Nafikiri walikuwa na malengo ya kutanua miji kwaiyo sion kama ni issue
Bukoba iliachwa kwa kuwa watu wa bukoba walikosea kuchagua upinzani...ndo alivyosema....


Na hii stendi ingekuwa Bukoba hela zingesharudi zote

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Yule jamaa alikuwa anajaza mamiradi wilayani kwake hata kama wananchi hawapo tayari yani alimradi tuu.
 
Ina mabasi manne tu na haisi chache kwa siku, gharama za uendeshaji ni hatari
 
Hio stand bora wangeijenga Shinyanga lakini Chato labda baadae patachangamka.
 
Back
Top Bottom