Habarini,
Unakutana na mdada unampenda, mnakua kwenye talking stage labda kwa miezi kadhaa, mnaongea vizuri tu mna click, unapenda tabia yake na muonekano wake, unaanza kusema huyu Mungu akipenda tutaishi kama wapendwa, unaanza ku-imagine future nae.
Baada ya muda uhalisia unakupiga na kitu kizito, unakuja kugundua huyo mdada ana mtoto tayari, unajiuliza mda wote huo inakuaje mtongozaji hujawahi muona wala kumsikia baba wa mtoto kwenye maisha ya binti, binti bado anaishi kwao hapo ushaweka matarajio, attention, time etc mwishowe mwanaume unaishia kuvunjika moyo..ingekua ni heri toka mwanzo ujue kua huyu tayari ashatolewa mahari, au yuko kwenye serious relationship, ndo upange kama unasuka au unanyoa..
Kama mmekutana kimjini mjini wadada wengine huenda mbali zaidi na kumficha mwanaume mpya ukweli kua tayari ana mtoto, mwanaume unakuja gundua baadae sana kuwa mdada unae date nae tayari ana mtoto.
Mungu alituagiza ndoa kwanza ndo mengine yafate, tukakaidi amri zake, matunda yake tunaanza yaona.. 🙆🏾♂️
Vijana wa kiume wa hovyo kwenye 1 na 2, kazi kuharibu, hata kama baby mama ni kichomi hudumia mtoto wako, kuwa karibu kwenye maisha ya mwanao, sababu ndo bomu ushalivaa, umaskini si kisingizio