Hali tete Simiyu, wananchi wanalazimishwa kwenda kwenye ziara ya Rais Samia

Haimaanishi kama wewe hujalazimishwa hilo jambo halipo. Ni sawa na kusema ukimwi haupo, kwasababu wewe hujaupata.
Huo mfano ni batili kiongozi. Pia naweza kukuelewa ukiniambia watu wanarubuniwa na vipande 30 vya fedha.
 
Ni mfano usiokubaliana nao, ila si batili. Mimi ni mmiliki wa shule fulani hapa nchini, nimeshaagizwa zaidi ya mara moja kupeleka watoto wa shule kwenye hiyo mikusanyiko ya rais. Huwa inakuwa kama ni ombi, lakini kiuhalisia ni lazima, na wamiliki wengine wa shule waliokwenda kinyume na maagizo hayo wamekutana na vikwazo vya dola.
 
Poleni kwenu.
Lakini fahamuni kuwa huo ni sehemu ya mkakati kuelekea katika kujitangazia ushindi. Nanyi mtakuwa kithibitisho jinsi mlivyokuwa mstari wa mbele kumkubali Samia Suluhu Hassan.

Jiandaeni kukataa upumbavu huo.
Utakatishaji wa uharamia wa uchafuzi mkuu ndio hii.

Kesho watasema, "si mnaona ile nyomi kila mahali alipokuwa anenda, ndiyo hii imempa kura za kishindo".

CCM ya sasa ni genge la wasio na akili, werevu, busara wala maarifa.
 
Ni mfano usiokubaliana nao, ila si batili. Mimi ni mmiliki wa shule fulani hapa nchini, nimeshaagizwa zaidi ya mara moja kupeleka watoto wa shule kwenye hiyo mikusanyiko ya rais. Huwa inakuwa kama ni ombi, lakini kiuhalisia ni lazima, na wamiliki wengine wa shule waliokwenda kinyume na maagizo hayo wamekutana na vikwazo vya dola.
Aiseeeh poleni sana.
 
Hali ni tete hapa mkoani Simiyu. Raisi Samia atakuwa na ziara hapa.

Sasa maandalizi ya kuonyesha kuwa anakubalika yamekuwa ni maumivu Kwa raia.

Raisi atakapo pita wafanya bihashara wameamliwa kufunga maduka, watumishi wote,Sungusungu ,Mgambo wameamliwa kuhudhuria mikutano ya Samia.

Wenye shule za English medium wameamliwa kutoa magari ya Shule Kwa ajiri ya kusomba raia.

Je hii nguvu kubwa ya Nini, je serikali ya mkoa inawasiwasi kuwa wananchi wanaweza susia mikutano ya Raisi?

Tuombeeni sisi wana Simiyu maana maagizo ni mengi
Hapa mwanza City mitaa ya Kemondo nimeona mabasi ya shule yamejazana

Wazee na vijana walalamika tuuu oo sijui helaaa oo sijui gari langu

Hili sipandi anabembelezwa uelekeo ni Simiyu
 
Kujichanganyaje? U busy utautoa wapi ikiwa Barabara kuu zitapigwa Pini?

Chadomo Huwa mna ujinga sana ,wewe jiulize unaweza acha kazi ukaenda Kwa Samia au Kwa Heche? Nani ana maamuzi ya biashara Yako?
Hata huoni upumbavu wa unayo yaandika? Kwa nini watu walazimishwe kufunga shughuli zo za kazi?
Kuna sheria inayoelekeza hivyo?
Kama kuna sheria ya namna hiyo ni ya kipumbavu kabisa.
 
Watulie Maeneo Waendelee Na Majukumu Yao Ya Kila
Waache Siasa Za Kulazimishana
Kizuri Chajiuza Na Kibaya Chajitembeza Sana
Naelewa unachoeleza hapa; lakini kwa bahati mbaya sana wakifanya hivyo wakati wa uchaguzi itakula kwao!
Ni lazima WAKATAE upumbavu; siyo "watulie"tu mahala walipo.
 
Hali ni tete hapa mkoani Simiyu. Raisi Samia atakuwa na ziara hapa.

Sasa maandalizi ya kuonyesha kuwa anakubalika yamekuwa ni maumivu Kwa raia.

Raisi atakapo pita wafanya bihashara wameamliwa kufunga maduka, watumishi wote,Sungusungu ,Mgambo wameamliwa kuhudhuria mikutano ya Samia.

Wenye shule za English medium wameamliwa kutoa magari ya Shule Kwa ajiri ya kusomba raia.

Je hii nguvu kubwa ya Nini, je serikali ya mkoa inawasiwasi kuwa wananchi wanaweza susia mikutano ya Raisi?

Tuombeeni sisi wana Simiyu maana maagizo ni mengi
poleni ndgu zangu,hata hivo anapita tu kuwaoneni,baada ya dakika kadhaa ataondoka na mtaendelea na kazi za ujenzi wa taifa.
 
Hapana, huyo ni mtumishi wa watu, lazima apite huko.
"Mtumishi" anayewageuza anaowatumikia kuwa watwana ndani ya nchi yao?

"Mtumishi" anaye walazimisha waTanzania kwa nguvu awe "mtumishi" wao?

"Mtumishi" anaye wateka/wapoteza/kuwaua waTanzania anaopaswa kuwatumikia?

"Mtumishi", anaye wapora raslimali waTanzania na kuzigawa hovyo hovyo kwa wageni?

"Mtumishi" asiye waamini watu anaowatumikia kuwa na uwezo wa kujiletea maendeleo yao wenyewe?

Huyu ni "Mtumishi", au "Mtumikiwa"?
 
Huyu ni "Mtumishi", au

Ni muhimu pia kutafuta hoja za msingi na vielelezo kabla ya kutoa tuhuma nzito kama hizi. Badala ya kulaumu kwa jumla, ni vyema kuhoji kwa njia ya kistaarabu, kushiriki mijadala ya wazi, na kuhimiza uwajibikaji kwa misingi ya sheria na katiba. Ndiyo njia bora ya kujenga taifa la haki na maendeleo.
 
Huo mfano ni batili kiongozi. Pia naweza kukuelewa ukiniambia watu wanarubuniwa na vipande 30 vya fedha.
Kaka mzalendo, naomba kujua huyu bwana alichukuliwa hatua gani? Au alichokisema hapa ni sawa?
 
Ni muhimu pia kutafuta hoja za msingi na vielelezo kabla ya kutoa tuhuma nzito kama hizi. Badala ya kulaumu kwa jumla, ni vyema kuhoji kwa njia ya kistaarabu, kushiriki mijadala ya wazi, na kuhimiza uwajibikaji kwa misingi ya sheria na katiba. Ndiyo njia bora ya kujenga taifa la haki na maendeleo.
Akihojiwa anakubali kusikiliza? Ni watu wangapi walipinga swala na bandari kuuzwa? Je ni kweli kwamba watanzania hawawezi kusimamia mapato ya uwanja wa ndege wa KIA mpaka wapewe waoman kusimamia?
Je ni haki kuzuia waumini wa kanisa la ufufuo na uzima kuabudu kwa sababu kiongozi amekemea utekaji?
 
Hizi "lugha za kistaarabu" mnapenda sana kuzihimiza; wakati nyinyi mkitenda mambo yasiyokuwa ya "kistaarabu"!

Mkuu 'Kipangaspecial', hivi kwa nini mnapenda sana kuwa watu walaghai laghai namna hii; mnafunzwa mahali kuwa watu wa namna hii, au ni utamaduni mnaourithi katika jamii mnayo zaliwa na kukulia?
Hebu jaribu kusoma ulicho andika hapo juu, kuhusu "sheria, Katiba, n.k., n.k.. Unapoandika ulaghai wa namna hii unategemea nani atakuamini tena, baada ya nyinyi wenyewe kutoheshimu hayo mnayo wahimiza wengine wayafuate?

Wewe hujasikia watu wakitekwa na kupotea au kuuawa. Unaishi wapi? Nani mwenye jukumu la kuchunguza na kutumia sheria ili mambo haya yasiendelee kuwepo. Unataka ushahidi upi ndipo ujue kuwa haya yanayofanyika yanatendwa na hao hao wenye dhamana ya kulinda usalama wa raia wao?

Kila moja ya hayo unayoyaita wewe "tuhuma" ni mambo ambayo yapo wazi; yanasimamiwa na serikali ya Samia Suluhu Hassan na GENGE lake.
 
Akihojiwa anakubali kusikiliza? Ni watu wangapi walipinga swala na bandari kuuzwa? Je ni kweli kwamba watanzania hawawezi kusimamia mapato ya uwanja wa ndege wa KIA mpaka wapewe waoman kusimamia?
Je ni haki kuzuia waumini wa kanisa la ufufuo na uzima kuabudu kwa sababu kiongozi amekemea utekaji?
Na GESI ya Ntorya, kule Mtwara, wamepewa waOman kimya kimya; hakuna anayejuwa kwa makubaliano ya namna gani?
Na kama waTanzania wakikubali huyu mwanamke kwa njia yoyote ile aendelee kuwepo madarakani kwa miaka mitano mingine, atasababisha uharibifu mkubwa sana ndani ya nchi hii.
 
Hizi "lugha za kistaarabu" mnapenda sana kuzihimiza; wakati nyinyi mkitenda mambo yasiyokuwa ya "kistaarabu"!

Mkuu 'Kipangaspecial', hivi kwa nini mnapenda sana kuwa watu walaghai laghai namna hii; mnafunzwa mahali kuwa watu wa namna hii, au ni utamaduni mnaourithi katika jamii mnayo zaliwa na kukulia?
Hebu jaribu kusoma ulicho andika hapo juu, kuhusu "sheria, Katiba, n.k., n.k.. Unapoandika ulaghai wa namna hii unategemea nani atakuamini tena, baada ya nyinyi wenyewe kuheshimu hayo mnayo wahimiza wengine wayafuate?

Wewe hujasikia watu wakitekwa na kupotea au kuuawa. Unaishi wapi? Nani mwenye jukumu la kuchunguza na kutumia sheria ili mambo haya yasiendelee kuwepo. Unataka ushahidi upi ndipo ujue kuwa haya yanayofanyika yanatendwa na hao hao wenye dhamana ya kulinda usalama wa raia wao?

Kila moja ya hayo unayoyaita wewe "tuhuma" ni mambo ambayo yapo wazi; yanasimamiwa na serikali ya Samia Suluhu Hassan na GENGE lake.
Ndugu yangu mtanzania na mzalendo mwenzangu, naelewa hasira zako na huzuni inayosababishwa na mambo tunayoshuhudia nchini. Hakuna anayepaswa kupuuzia maumivu ya watu waliopotea au dhuluma yoyote ile—na wala siwezi kuzifumbia macho.

Lakini pia, tukitaka kweli mabadiliko ya haki na kudumu, ni lazima tusimame kwenye msingi wa hoja, siyo hasira pekee. Lugha ya staha si udhaifu, bali ni silaha ya watu wanaotaka kushinda kwa uadilifu. Tukitumia maneno ya kejeli au hasira, tunawapa nafasi walioko madarakani kutopokea ujumbe wetu.

Mambo haya tunayoyapinga—utekaji, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka—hayapigwi kwa jazba pekee, bali kwa kujenga umoja wa hoja, kuhamasisha raia, na kuibana serikali kwa njia za kikatiba. Si kila anayekumbusha hayo ni mlaghai, bali wengine tunataka tuone haki ikipatikana bila kuangamiza kile kidogo tulichonacho kama taifa.

Tusikubali hasira zituharibie njia. Badala yake, tuzitumie kuimarisha hoja zetu.
 
Back
Top Bottom